Hitimisho juu ya Historia ya maimam wanne
Hitimisho
Maimamu wote wanne walikuwa wanachuoni wacha Mungu na waadilifu katika zama zao. Walifanya juhudi kubwa kusoma na kufanya ijtihada ya kutafsiri na kutoa maoni yao juu ya sheria na masuala mbalimbali ya Fiqh. Ni vizuri tunufaike na matunda ya juhudi zao, lakini tusigawike wala kubaguana kutokana na maoni tofauti ya Maimamu hao juu ya masuala mbalimbali. Wao wenyewe walisoma pamoja au kusomesha na wakaheshimiana na wakaafikiana kutofautiana katika mambo ya msingi bila ya kugombana.
Jambo jingine la msingi la kuzingatia ni kuwa Maimamu hawa walipata mateso makubwa kutokana na misimamo na juhudi zao katika kuuhuisha na kuusimamisha Uislamu katika
jamii. Walichapwa viboko, walifungwa gerezani na kufungwa minyororo na watawala madhalimu. Zaidi ya hivyo hawakukubali kununuliwa na Serikali. Walikataa kabisa kuwa vibaraka wa Serikali. Je, wakati tunafuata Fiqh na Fatβwa zao tunao pia uadilifu kama wao? Misimamo yetu juu ya Serikali za kidhalimu ni kama wao? Je, hatununuliwi na Serikali na kuifanyia kazi kinyume na maslahi ya Uislamu? Je, tupo tayari kufungwa na kuchapwa viboko kwa ajili ya kusimamisha haki kama Imam Abu Hanifa, Malik, Shafii na Hambal?
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Kitabu cha Afya π2 kitabu cha Simulizi π3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) π4 Bongolite - Game zone - Play free game π5 Madrasa kiganjani π6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Mbinu na njia walizotumia maadui wa uislamu dhidi ya waislamu na dola ya kiislamu madinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...NI UPI MKATABA WA AL-FUDHUL NA ASILI YAKE, ATHARI ZAKE NA WALOHUSIKA
MKATABA WA AL-FUDHULBaada ya vita hivi viongozi wa pande mbili hizi waliamuwa wakae chini na wakubaliane kuweka kanun i na utaratibu utakaozuia kutotokea uonevu kama huuu tena.
Soma Zaidi...Nani alikuwa ni Sahaba wa kwanza kufariki akiwa Shahidi
Sahaba wa kwanz akufariki akiwa shahidi, alifariki kwa sababu ya mateso aliyoyapata kutoka kwa Makafiri wa ki Quraysh
Soma Zaidi...