Kuanzishwa kwa Tawala za kifalme baada ya uongozi wa Makhalifa.
Kuanzishwa Ufalme.
Kuanzishwa Ufalme.
Muawiyah kwa kumrithisha mtoto wake, Yazid, uongozi wa Dola, bila kuzingatia utaratibu wa kuchangua viongozi kutokana na sifa stahiki, alivunja maongozi ya Kiislamu na kuasisi utawala wa kifalme au utawala wa kiukoo ambao mpaka leo unaendelezwa katika nchi nyingi za Arabia(Bara Arab), Saud Arabia ikiwa miongoni.
Dola ya kifalme aliyoiasisi Muawiya ilitafautiana na Dola ya Kiislamu aliyoiasisi Mtume(s.a.w) na kuendelezwa na Makhalifa wanne waongofu, Abubakar, βUmar, Uthman na Ali, kwa sababu:
(i) Taasisi ya shura ilivyunjwa na raia walipokonywa uhuru wao wa kutoa maoni na kukosoa viongozi
(ii) Hazina ya Dola β Baitul-Mali, ilifanywa mali ya nyumba ya mfalme ambapo mfalme aliitumia atakavyo kwa maslahi yake binafsi na familia ya kifalme.
(iii)Tabia za kijahili za majivuno ya kikabila na nasaba ziliibuka na kustawishwa na ufalme.
(iv)Watawala (viongozi mbali mbali wa dola) walianza kuishi kwenye mahekalu na nyumba za kifahari za Kifalme.
(v) Suala la kutenganisha maongozi ya Serikali na Dini liliibuka.Masheikh wazuri waliokuwa waadilifu walitengwa na kundi la watawala. Wao wakawa wanajitahidi kuirekebisha jamii lakini wakiwa ndani ya kuta nne za msikiti na nje ya vyombo vya dola.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Kitabu cha Afya π2 Simulizi za Hadithi Audio π3 Kitau cha Fiqh π4 ai web app π5 Bongolite - Game zone - Play free game π6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Mafunzo yatokanayo na kuanzishwa kwa dola ya uislamu madinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Muhutasari wa sifa za wanafiki
Kwa kuzingatia aya zote tulizozipitia juu ya wanafikitunaweza kutoa majumuisho ya sifa za wanafiki kama ifuatavyo:- (1)Hutenda kinyume cha imani wanaodai kuwa nayo.
Soma Zaidi...Mbinu na njia walizotumia maadui wa uislamu dhidi ya waislamu na dola ya kiislamu madinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...