KUPASULIWA KWA KIFUA MTUMEWAKATI AKIWA MTOTO.
KUPASULIWA KWA KIFUA MTUMEWAKATI AKIWA MTOTO.
Mtume alipokuwa mtoto tukio hili la kupasuliwa kwa kifua chako na kutolewa moyo wake na kusafishwa. Yote haya yalitokea kipindi akiwa analelewa na bi Halima katika kabila la bani Saβad. Wanazuoni wa sirah wameeleza kwa urefu tukio hili jinsi lilivyotokea. Na hapa tutaangalia kwa ufupi tu.
Ni kuwa siku moja mtume (s.a.w) alikuwa anacheza na watoto wenzie. Ghafla akatokea mtu mmoja naye ni Jibrib akamshika Muhammad na kumlaza chini kisha akamtoa moyo wake na kuuosha kwa maji ya zamzam na aliondoa uchafu wa shetani kisha akaurudisha kwenye kifua na kukifunika.
Watoto walokuwa wakicheza na Mtume (s.a.w) wakakimbia na kwenda kumueleza bi Halima kuwa Muhammad kauliwa. Bi Halima akatoka kwa haraka kufika akamkuta Muhammad akiwa amebadilika rangi. Muhammad alikuwa ni mzima wa afya, hapa bi Halima alipata mashaka makubwa mpaka akawa na hofu juu ya kuendelea kumlea kijana Muhammad.
Katika maelezo mengine waandishi wa sirah wameeleza tukio hili kama kupasuliwa kwa tumbo. Kwani zimekuja nukuu kuwa sikumoja waroto walipokuwa wakisheza pamoja nao alikuwepo Muhammad (s.a.w) basi ghafla wakaja wanaume wawili walovaa nguo nyeupe (Malaika) wakaulizana ni hyu? Basi yule mwingine akajibu ndio ni huyu, wakamlaza kisha wakampasua tumbo lake na kutoa uchafu wa shetani kisha wakafunika kama lilivyo. Basi watoto walokuwa wakicheza nae wakaenda mbio kusema wa bi halima na alipokuja kuulizwa Muhammad (s.a.w) akasema kuwa watu wawili wamekuja na kunipasua tumbo langu. Utapata maelezo zaidi ya kisa hiki kwenye kitabu kiitwacho Nurul- Yaqin.
Bi Halima aliendelea kumlea Mtume (s.a.w) kwa muda wa miaka miwili mingine hata alipotimiza miaka minne aliamuwa kumrudisha mtoto kwa mama yake. Alihofia kuendelea kumlea mtoto huyu huenda akapatwa na jambo. Miaka minne alikuwa imemtosha mtoto huyu kuwa na mwili imara na kuweza kuzungumza lugha ya kiarabu wa ufasaha tofauti na watoto walolelewa maeneo mengine.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
βNa wasomee khabari za watoto wawili wa Adam kwa kweli, walipotoa sadaka, ikakubaliwa ya mmoja wao na ya mwingine haikukubaliwa Akasema (yule asiyekubaliwa sadaka yake): βNitakuuaβ.
Soma Zaidi...Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 13. Hapa utajifunza historia ya Mkataba wa al fudhul na makubaliano yake.
Soma Zaidi...Huko nyuma wapita njia walikisogelea kisima kwa lengo la kuteka maji.
Soma Zaidi...Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W, sehemu ya 7
Soma Zaidi...Upinzani dhidi ya Dola ya Kiislamu Madinah.
Soma Zaidi...Uendeshaji wa Dola ya Kiislamu Madinah.
Soma Zaidi...