Kuibuka kwa Khawarij
Baada ya makubaliano, Ali aliwatangazia makubaliano haya wapiganaji wake. Lakini ndugu wawili wa kabila la Azza walisimama kupinga suluhu kwa hoja kuwa wanazo hukumu za Mwenyezi Mungu katika Qurβan hivyo hawahitaji wasuluhishi. Watu wengi waliunga mkono rai hii na kufikia 12,000. Wao hawakurudi Kufa, walipiga kambi mahali paitwapo Harorah. Walimteua Sheikh bin Rabi kuwa kamanda wao na Abdullah bin Kawa kuwa Imam wa kuongoza Swala. Walitangaza imani yao ambayo ilikuwa:
βBaβiyah iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu, yeye tu ndiye wa kutiiwa. Kuhubiri mema na kukataza mabaya. Hakuna Khalifa au Amir. wote Ali na Muawiya wana makosa, Muawiyah anamakosa kwa kutomtii Ali, na Ali anamakosa kwa kukubaliana na Muawiyah juu ya suluhu. tutaposhika mamlaka tutaanzisha mfumo wa maisha ya jamii uliojengwa juu ya Qurβanβ.
Ali aliporudi Kufa alimtuma Abdullah bin Abbas, Harorah kuzungumza na Khawarij. Aliweza kuwavuta na wakakubaliana na Khalifa baada ya mazungumzo ya muda mrefu. Hata hivyo kukubali huku kulikuwa kwa muda tu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mtume aliyemfuatia Nabii Idrisa(a.
Soma Zaidi...Yiomyokea khalid Ibn al walid katika vita vya Muta
Soma Zaidi...Kuanzishwa kwa Dola ya Kiislamu Madinah.
Soma Zaidi...