image

Imam Muhammad Idris al-Shafii

Imam Muhammad Idris al-Shafii

Imam Muhammad Idris al-ShafiiImam Shafii alizaliwa mwaka (150 A.D.) huko Gaza katika ukanda wa Pwani ya bahari ya Meditteranean. Yeye ni wa kabila la Quraysh. Akiwa bado kijana, Imam Shafii alihifadhi Qurโ€™an na Kitabu cha Imam Malik, al-Muwata. Alisoma elimu ya sheria ya Kiislamu toka kwa mwanachuoni mashuhuri na Mufti wa Makka Muslim bin Khalid al-Zanji. Baada ya kifo cha Khalid, alikwenda Madinah ambapo alisoma kwa Imam Malik bin Anas. Wakati Imam Malik anafariki tayari Imam Shafii alikuwa ashavuma ndani ya Arabuni na kwingineko kwa ujuzi wake wa elimu ya sheria na Uislamu kwa ujumla.


Kutokana na elimu na uadilifu wake, Imam Shafii aliteuliwa kufanya kazi Serikalini. Hata hivyo hakudumu kwani kwa uadilifu na utendaji wake wa kazi kwa haki aligongana na wakuu wa Serikali wasiotaka haki. Alikamatwa na kuhamishiwa Iraq akiwa amefungwa minyororo kwa tuhuma kuwa anafanya uchochezi dhidi ya Serikali. Huo ulikuwa mwaka 187 A.H. (803 A.D.) wakati wa utawala wa Harun al-Rashid. Baadae aliachiwa huru kwa kuonekana hana hatia. Alibaki kwa muda Baghdad akisoma chini ya wanafunzi wa Imam Abu Hanifah. Alifanya kazi ya kudarasisha Makka na akapata wasikilizaji wengi akiwemo Imam Ahmad bin Hambal ambaye wakati huo alikuwa anasoma Makka. Pamoja na kuwa alikuwa na maoni ya kifiqh tofauti na yale ya Imam Malik na Abu Hanafi, aliwaheshimu na kuthamini juhudi na michango yao. Hakujenga kundi la Shafii dhidi ya Maimamu wengine kama ambavyo baadhi ya Masheikh hufanya hivi leo.


Maimamu ambao tunajinasibisha nao hivi leo wao walikuwa wamoja katika Uislamu. Pale walipokuwa na maoni tofauti katika ufahamu wa baadhi ya mambo walikubaliana kutofautiana, wakazikubali tofauti zao, lakini walibaki kuwa wamoja walioshikamana katika kamba (dini) ya Allah(s.w).


Kazi kubwa ya kufundisha na uandishi, Imam Shafii aliifanyia Misri katika mji wa Cairo ya leo. Huko alizungukwa na wanafunzi na wanachuoni toka sehemu mbalimbali. Walijifunza na kuandika kila alichosema. Imam Shafii alikuwa na kawaida ya kuwaamrisha wanafunzi wake kusoma kwa sauti kila walichoandika ili apate kusahihisha. Kazi kubwa muhimu za Imam Shafii ambazo zinaendelea kutoa mchango mkubwa katika elimu ya Fiqh na sheria ya Kiislamu mpaka hivi leo ni Kitab al-Umm na Kitab al- Risalah Fi-Usul-al Fiqh (al-Risalah). Imam Shafii alifariki na kuzikwa Cairo mwezi Rajabu mwaka 204 A.H/20/1/820 A.D.
                   
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 572


Download our Apps
๐Ÿ‘‰1 Kitau cha Fiqh     ๐Ÿ‘‰2 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰3 Madrasa kiganjani     ๐Ÿ‘‰4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Nabii Yunus(a.s) Amuomba Allah(s.w) Msamaha
Ndani ya tumbo la samaki, Nabii Yunus(a. Soma Zaidi...

TAREKH, HISTORIA NA SIRA YA UISLAMU NA MTUME MUHAMMAD KUTOKA KUZALIWA MPAKA KUFARIKI NA HARAKATI ZAKE
1. Soma Zaidi...

MTUME MUHAMMAD (S.A.W)ANAKUTANA NA BAHIRA (MTAWA WA KIYAHUDI)
KUKUTANA NA BAHIRA (MTAWA) WA KIYAHUDIMzee Abu talib alikuwa ni mfanya biashara, hivyoslikuwa akimchukuwa kijana wake kwenda kwenye biashara. Soma Zaidi...

KUCHIMBWA UPYA KWA KISIMA CHA ZAMZAMA NA KUNYWA MAJI YA ZAMZAMA KISIMA KILICHO BARIKIWA
KUCHIMBWA UPYA KISIMA CHA ZAMZAMKwa kifupi ni kuwa Abdul-Muttalib alipata agizo kutoka ndotoni kuwa achimbe kisima cha zamzam, na akaelekezwa sehemu ya kupachimba. Soma Zaidi...

Uchaguzi wa Abubakari kuwa Khalifa wa kwanza baada ya kufariki Mtume Muhammad (s.a.w)
Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME ZAKARIA(A.S) NA YAHYA(A.S)
Zakaria(a. Soma Zaidi...

historia na maisha ya Mtume IS-HAQ(A.S.) NA YAโ€˜AQUUB(A.S.)
Is-haq(a. Soma Zaidi...

Imam Ahmad bin Muhammad bin Hambal
Soma Zaidi...

Mapambano ya waislamu dhidi ya maadui wa kiyahudi madina
Mayahud Mwanzoni Mayahud walipoona kuwa Waislamu wanafunga siku ya Ashura pamoja nao na wanaelekea Qibla cha Baitul- Muqaddas pamoja nao hawakuonyesha chuki ya dhahiri dhidi ya Mtume(s. Soma Zaidi...

Mapambano ya Mtume Muhammad dhidi ya Wanafiki na hila zao Madina
Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Ismail(a.s)
Kutokana na Historia ya Nabii Ismail(a. Soma Zaidi...

Imam Bukhari na Sahihul Bukhari
Soma Zaidi...