Baada ya miaka mitatu ya Utume, Muhammad(s.
Baada ya miaka mitatu ya Utume, Muhammad(s.a.w) aliamuriwa na Mola wake kuutangaza ujumbe kwa uwazi kwa watu wote.
“Basi yatangaze uliyoamrishwa (wala usijali upinzani wao) na ujitenge mbali na hao washirikina. Hakika sisi tunatosha kukukingia (shari ya) wanaofanya dhihaka”. (15:94-95)
Na uwaonye jamaa zako walio karibu (nawe). Na uinamishe bawa lako kwa yule anayekufuata katika wale walioamini. Na kama wakikuasi, basi sema: “Mimi ni mbali na hayo mnayoyafanya.” Na umtegemee (Mola wako) Mwenye nguvu, Mwenye rehema. (26:214-217)
Mtume(s.a.w) alianza kutekeleza amri hii kwa kutumia nyenzo ya “tabia yake njema”. Aliita kwa jina ukoo moja moja mpaka kumaliza koo zote kumi na nne za kabila la Quraysh akiwa juu ya kilima cha Safa, karibu na Ka’abah. Baada ya koo zote kuhudhuria chini ya kilima cha Safa, Mtume(s.a.w) aliwaomba jamaa zake wa karibu, banu ‘Abdul-Manaf, wasogee karibu naye kisha akaanza kutoa khutuba yake ya kwanza:
“Mnaonaje! Kama nikiwapa taarifa kuwa kunajeshi kubwa linalokuja kukupigeni kutoka chini ya mlima huu, je, mtaniamini?” Wakajibu wote kwa pamoja, “Naam, bila shaka tutakuamini, kwani hatujawahi kusikia kutoka kwako ila ukweli”. Kisha Mtume(s.a.w) akasema, “Hakika mimi kwenu ni kama mtu aliyemuona adui, kwa hiyo akaenda kuwaonya watu wake, lakini akahofu kwamba adui anaweza kumuwahi kabla hajafikisha habari kwa watu wake, kwa hiyo akaanza kupiga kelele:
‘Tahadharini na mashambulizi ya asubuhi’. Hakika mimi ni muonyaji kwenu juu ya adhabu kali iliyo mbele yenu. Enyi wana wa Abdul-Muttalib, Enyi wana wa ‘Abdul-manaf, Enyi wana wa Zuhr, (mpaka akamaliza kuziita koo zote za Quraysh), hakika Allah ameniamrisha kuwaonya jamaa zangu wa karibu. Na hakika mimi sina cha kuwanufaisha katika maisha haya ya dunia na ya huko akhera ila mtakapokiri kuwa “Hapana Mola ila Allah” 5
Baada ya kwisha kwa khutuba hii, Maquraish walikasirika sana wakawa wanapiga kelele “umekuwa mwendawazimu!” Ami yake Mtume, Abu Lahab, alimuapiza: “Iangamie mikono yako miwili siku ya leo. Hili ndilo ulilotuitia hapa? Heshima yote tuliyokuwa tukikupa sasa umeikosa. Ondokeni, mwacheni mpuuzi huyu.”
Mtume(s.a.w) alihuzunishwa sana na maneno ya Abu Lahab, ami yake. Allah(s.w) alimfariji Mtume wake kutokana na hali ile kwa kumshushia Suratul-Lahab:
Pana kuangamia mikono miwili ya Abu Lahab! Naye amekwisha angamia. Hayatamfaa mali yake wala alivyovichuma. (Atakapokufa) atauingia Moto wenye mwako (mkubwa kabisa). Na mkewe, mchukuzi wa kuni (za fitina, fattani, anayefitinisha watu wasiingie katika Dini; ataungia naye Moto huo). (Kama kwamba) shingoni mwake iko kamba iliyosokotwa (anayochukulia kuni za fitina hizo). (111:1-5)
Siku chache baada ya tukio la Safa, Mtume(s.a.w) aliwaalika jamaa zake wa karibu kwa chakula. Baada ya kumaliza kula Mtume(s.a.w) alisimama na kuwafikishia ujumbe ufuatao:
“Enyi kizazi cha wana Abdul-Muttalib, hakika Allah amenituma kuwa Mtume kwenu nyinyi na kwa watu wote kwa ujumla. Kwa hiyo ameniamrisha: “Na uonye jamaa zako walio karibu.” Na ninawaiteni kwenye maneno mawili ambayo ni mepesi sana katika ulimi na mazito sana katika mizani, nayo ni “Kushuudia kuwa hapana Mola ila Allah na kwamba mimi ni Mtume wake.” Nani atakayeniitikia na kunisaidia katika kazi hii? Alijibu ‘Ali (r.a), “Nitakusaidia Ewe Mtume wa Allah”. Mtume akamwambia: “Kaa chini”. Mtume(s.a.w) alirudia tena kuuliza swali lile. Lakini wote walinyamaza kimya, ila ‘Ali bin Abu-Talib alisimama tena akasema: “Nitakusaidia Ewe Mtume wa Allah. Kisha alimuamuru tena kukaa chini. Kisha alirudia tena swali lile kwa mara ya tatu. Lakini hapana aliyejibu. Ndipo ‘Ali alisimama tena na kujibu, ‘Nitakusaidia Ewe Mtume wa Allah. Mtume akamwambia: “Kaa chini, wewe ndugu yangu.” 6?
Mafunzo:
Kutokana na hatua hii ya Mtume(s.a.w) kufikisha ujumbe kwa uwazi na kwa watu wote tunajifunza yafuatayo:
Kwanza, baada ya kuuhuisha Uislamu katika nafsi zetu na watu wetu wa karibu, familia, ndugu na rafiki, hatuna budi kutanua wigo wa ulinganizi mpaka kufikia ngazi ya Kitaifa na hatimaye ya Kimataifa. Uislamu ni Dini ya ulimwengu mzima na waumini wote ni ummah mmoja na ndugu moja.
Pili, hapana yeyote wa kumchelea katika kutekeleza amri ya Allah(s.w). Baada ya Mtume(s.a.w) kupewa amri ya kufikisha ujumbe kwa kila mtu wa kabila lake (jamaa zake wa karibu), alifanya hivyo bila ya kujali upinzani aliokuwa akiutarajia.
Tatu, subira na kutokata tamaa ni nyenzo muhimu mno katika kulingania Uislamu. Baada ya kupuuzwa ujumbe wake katika hadhara ya mlima Safa, Mtume(s.a.w) aliendelea mbele na kazi yake kwa kuwaita peke yao watu wake wa karibu zaidi – Wana Abdul-Muttalib.
Nne, hatunabudi kutumia mbinu mbali mbali katika kulingania Uislamu. Mtume(s.a.w) alitumia mbinu ile ya kuwaita Maquraish wote kwenye kilima cha Safa na kuchagua kuwafikishia khutuba ile. Kisha akatumia mbinu ya kuwaalika chakula watu wa ukoo wake wana Abdul-Muttalib.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 632
Sponsored links
👉1
Madrasa kiganjani
👉2
kitabu cha Simulizi
👉3
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4
Kitau cha Fiqh
👉5
Simulizi za Hadithi Audio
👉6
Kitabu cha Afya
Uchaguzi wa Abubakari kuwa Khalifa wa kwanza baada ya kufariki Mtume Muhammad (s.a.w)
Soma Zaidi...
MJADALA JUU YA NDOA YA MTUME S.A.W NA BI KHADIJA (HADIJA)
LAKINI UMRI WANGU MKUBWABaada ya kuwaza na kufikiri muda mrefu, bibi Khadija (Radhiya Llahu anha) akafikia uamuzi wa kutaka kuolewa na Muhammad (Swalla Laahu alayhi wa sallam). Soma Zaidi...
HISTORIA YA NABII ADAM
Soma Zaidi...
Watu wa Mji Waliomuua Muislamu kwa Kuwa Amewasadikisha Wajumbe wa Allah(s.w)
Katika Suratul Yassin Allah(s. Soma Zaidi...
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Hud(a.s)
(i) Tuanze kulingania kwa kuonesha upweke wa Allah(s. Soma Zaidi...
HISTORIA YA NABII LUTI
Soma Zaidi...
Yusufu(a.s.) Akutana na Ndugu Zake
Njaa ilitokea na ikawa hapana sehemu nyingine yoyote yenye chakula ila Misri. Soma Zaidi...
Historia ya Vijana wa Pangoni
Makafiri wa Kiquraish walikuwa na tabia ya kumghasi Mtume(s. Soma Zaidi...
Historia ya Kuzuka Imani ya Kishia waliodai kuwa ni wafuasi wa Ally
Soma Zaidi...