HISTORIA YA BI KHADIJABi Khadija jinalake halisi ni Khadija bint Khuwald bin Asab baba yake alikuwa ni mfanya biashara.
HISTORIA YA BI KHADIJA
Bi Khadija jinalake halisi ni Khadija bint Khuwald bin Asab baba yake alikuwa ni mfanya biashara. Baadhi ya historia zinataja kuwa alifariki wakati wa vita vya Alfijar mwaka 585 BK, tumetaja muhusu vita hivi kurasa za hapo juu. Nasaba yake pia inakutana na nasaba ya Mtume Muhammad kwa upande wa bab yake na baba yake. Mama yake aliitwa Fatima Bint Za’idah na alikuwa katika kabila la maqurayshi, kabila la Mtume Muhammad (s.a.w). mama yake Khadija alifariki mwaka 575 KK. Khadija aliolewa na Muhammad mwaka 595.
Bi Khadija alishapata kuolewa na wanaume wawili kabla hata ya kuolewa na Muhammad na lishazaa watoto. Khadija alikuwa na katika wafanyabiashara wa Makkah wakubwa sana wakati huo. Historia inaonesha kuwa wakati waarabu wa kikurayshi walipokuwa wakikusanya bishaa zao ili kwenda kuziuza maeneo ya Syria na Yemen, msafara wa Khadija ulikuwa ni sawa misafara ya maquraysh wote ikusanywe pamoja. Hii inaonesha alikuwa ni tajiri zaidi wakati huo.
Tofauti na biashara Hadija alifahamika kuwa ni katika wanawake wazuri na wenye akili zaidi kuliko wanawake wote wa Makkah wakati huo. Watu wenye vyeo vyao na utajiri walikuwa wakienda kutoa posa lakini walikuwa wakirudi patupu. Hadija alikuwa ni katika wanawake waliokuwa wakiheshimika sana. Alikuwa ni mkarimu na mwenye kusaidia sana masikini na wasio na kitu. Na aliendeleza tabia hii hata baada ya kuolewa na Muhammad.
Hadija alipewa majina mbalimbali kutokana na cheo chake mbele za watu wa Makkah. Waarabu walimuita Ameerat-Quraysh (princess of quraysh) pia walimuita Khadija al-Kubra (Khadija the great). ijapokuwa Makkah wakati huo watu walikuwa wakiabudu masanamu lakini Khadija katu hajapatapo kusujudia masanamu.
Ijapokuwa Khadija alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa lakini hajapatapo kusafiri na biashara zake ili kwenda kuuza. Alikuwa akiajiri wanaume waendde kumfanyia biashara na anawalipa kwa makubaliano maalumu. Mwaka 595 Khadija alihitaji mtu wa kwenda kumfanyia biashara zake maeneo ya Syria. Kwa kuwa alipatapo kusikia sifa za Muhammad kuwa ni Mwaminifu na ni mkweli hivyo akamtafuta na wakakubaliana kuwa atamlipa zaidi kuliko ambavyo anawalipa watu wengine.
Nafisa alikuwa ni rafiki wa karibu sana wa Khadija, hata wakati Khadija alipotaka kuolewa na Muhammad alimtumia nafisa ili aende kuzungumzana Muhammad kuhusu jambo hili. Tumeshazungumza khabari hii hapo kurasa za nyuma. Mjomba wake Khadija alifahamika kwa jina la Waraqa bin Nawfal. Huyu alikuwa ni mkristo na ni mchamungu na alitambua vyema ujio wa Mtume wa Mwisho. Hata wakati watu wote wa Makkah hawakujuwa kuwa Muhammad atakujakuwa Mtume Waraqa alishatambua jambo hili. Waraqa ndiye aliyesimamia ndoa ya Khadija na Muhammad. Dada yake alifahamika kwa jina la Hala bint Khuwayld.
Bi Khadija anajulikana kwa kuwa ndiye Mtu wa kwanza kutamka shahada ya kuamini utume wa Mtume Muhammad s.a.w. Khadija alitumia mali zake katika kuendeleza harakati za dini mpaka alipofariki mwaka wa 10 baada ya utume (yaani Miladiya) ni sawa na 620 katika mji wa Makkah. Khadija alifariki akiwa na umri wa miaka 65. na alizikwa sehemu iitwayo jannat al-Mu’allah mjini Makkah. Bi kahdija alishapataga kuolewa na ‘Atiq bin ‘Aidh Al-Makhzum na Abu Hala Malak ibn Nabash. Na alizaaa pamoja na waume wote hao watoto. Alizaa na Mtume Muhammad (s.a.w) watoto sita.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 3251
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉2 kitabu cha Simulizi
👉3 Kitabu cha Afya
👉4 Simulizi za Hadithi Audio
👉5 Kitau cha Fiqh
👉6 Madrasa kiganjani
MTUME MUHAMMAD (S.A.W) AANALELEWA NA BABU YAKE MZEE ABDUL-ALMUTALIB AKIWA NA UMRI WA MIAKA SITA (6)
KULELEWA NA BABU YAKE:Mzee ‘Abdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana. Soma Zaidi...
CHANZO CHA VITA VYA VITA VYA AL-FIJAR NA ATHARI ZAKE
MAPIGANO YA AL-FIJAR (MAPIGANO YA UOVU). Soma Zaidi...
Kuanzishwa kwa Polisi na magereza kati uislamu wakati wa Makhalifa
Kuanzishwa kwa Polisi. Soma Zaidi...
Ijuwe Dua ya Ayyuub(a.s)
Nabii Ayyuub(a. Soma Zaidi...
HISTORIA YA MTUME YUNUS(A.S)
Nabii Yunus(a. Soma Zaidi...
NASABA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KABILA LAKE, UKOO WAKE NA FAMILIA YAKE
NASABA YA MTUME (S. Soma Zaidi...
Chanzo cha vita vya Ngamia Vita Kati ya Bibi Aisha na Khalifa Ali
Soma Zaidi...
Yusufu Aokotwa na Kuuzwa nchini Misri
Huko nyuma wapita njia walikisogelea kisima kwa lengo la kuteka maji. Soma Zaidi...
Bara arabu enzi za jahiliyyah, jiografia ya bara arabu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Zakaria(a.s) Akabidhiwa Ulezi wa Maryam
Baada ya kupigwa kura juu ya nani awe mlezi wa Maryam, Nabii Zakaria akachaguliwa kuwa mlezi wa Maryam. Soma Zaidi...
Mtume kumuoa bi khadija
Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 15. Hapa utajifunza kuhusu chimbuko la ndoa ya Mtume s.a.w na bi Khadija. Soma Zaidi...
Mawazo Tofauti Kuhusiana na Uchaguzi wa Abubakar
Soma Zaidi...