Imam Ahmad bin Muhammad bin Hambal
Imam Abu Abdallah Ahmad bin Muhammad bin Hambal alizaliwa huko Marwa mwezi 20 Rabi-al-Awwal 164 A.H. Baba yake Muhammad alikuwa mujahid aliyesifika wakati akiishi Basra, Iraq. Baba yake alihamia Baghdad ambapo alifariki muda mfupi baadae na kumuacha Ahmad bin Muhammad akiwa bado mchanga. Pamoja na uyatima wake, kijana Ahmad alikuwa mwenye akili na akautumia ujana wake wote katika kujielimisha. Alisoma zaidi Hadith na akawa mwanasheria na mtaalam wa fiqh katika zama zake. Kwa hiyo Imam Shafii na Imam Ahmad Hambal walikuwa karibu sana. Imam Hambal alimheshimu mwalimu wake Shafii, na Imam Shafii alimheshimu mwanafunzi wake mashuhuri Hambal.
Imam Ahmad Hambal alikuwa mwanachuoni Mcha Mungu sana aliyejitoa maisha yake yote kusoma na kufundisha Hadith na Fiqh. Kwa ucha Mungu wake alikataa kufanya kazi Serikalini, kwani aliona Serikali ilikuwa haiongozwi kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah. Zaidi ya hivyo alivunja uhusiano wa karibu na wote wale waliokubali kuwa ndani ya Serikali ya kidhalimu. Alikataa hata kupokea fedha au chakula kutoka kwa mtoto wake ambaye alikuwa akifanya kazi katika Serikali ile ya kidhalimu. Hata wakati alipokabiliwa na hali ngumu ya uchumi hakukubali kupokea msaada wowote ila kwa kuufanyia kazi.
Katika kipindi cha uhai wa Imam Ahmad waliibuka wanafalsafa waliokuja na falsafa iliyoitwa Mu’tazili. Falsafa hii iliwaita watu wawe huria katika fikra. Walichanganya imani na kufr hata kufikia kuleta hoja kuwa Qur’an imetengenezwa tu. Harakati hizi za kuleta kufr ndani ya Uislamu zilitokana na athari ya falsafa za Wagiriki zilizowalevya baadhi ya Waislamu wa zama hizo.
Bahati mbaya watawala wa zama hizo nao waliathiriwa na falsafa hizo za Kigiriki na wakataka kuifanya kuwa imani rasmi ya dola ya Kiislamu. Viongozi waliotaka kuisimika imani hiyo ni Khalifa Ma‘mun al-Rashid; Mu’taslim Billah na Al-Wathiq. Imam Ahmad bin
Hambal alikataa kuikubali imani hiyo mpya ya watawala na akaendesha harakati kuipinga. Mtawala Mu’taslim alitoa amri akamatwe afungwe minyororo na kuhamishiwa Tarsus toka Baghdad. Huko alitupwa gerezani na kuteswa sana mpaka viungo vyake vingi vikavunjika. Imam Ahmad aliachwa adumu amefungwa minyororo mizito ndani ya chumba chenye giza gerezani. Pamoja na kuteswa sana ikiwa ni pamoja na kuchapwa mpaka kutoka damu, Imam Ahmad hakutetereka katika msimamo wake. Msimamo huu wa Imam Ahmad ulimstua Khalifa Mu’taslim. Aliikumbuka Akhera akahofia khatima yake. Aliamuru Imam Ahmad atolewe gerezani mwezi 25 Ramadhan mwaka 221 A.H na akamuomba msamaha, Imam Ahmad akamsamehe.
Miongoni mwa kazi muhimu alizofanya Imam Ahmad ni kuandika vitabu vifuatavyo: Kitab al-Amal al-Tafsir; Kitab al- Nasikh wal-Mansukh na kadhalika. Lakini kazi muhimu zaidi aliyoiacha Imam Ahmad ni ukusanyaji wa Hadith elfu nyingi na kuandika kitabu cha Hadith cha Musnad ya Ibn Hambali. Ulipofika mwaka wa 241 A.H Imam Ahmad alifariki dunia. Maelfu ya watu wa Baghdad walifurika kumzika.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1234
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Kitabu cha Afya
👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4 Madrasa kiganjani
👉5 Kitau cha Fiqh
👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Mapambano ya Mtume Muhammad dhidi ya Wanafiki na hila zao Madina
Soma Zaidi...
Historia ya Watu wa Mahandaki ya Moto.
Katika Suratul Buruj, kumetajwa kisa cha makafiri waliowatesa wafuasi wa Mitume waliotangulia kabla ya Mtume Muhammad(s. Soma Zaidi...
Khalifa na Utungaji Sheria, na utiifu juu ya sheria na usimamiaji wa haki
Soma Zaidi...
Kuhajiri Waislamu wa Makka Kwenda Madinah
Baada ya mikataba miwili ya ‘Aqabah na baada ya Waislamu 75 kufika Yathrib salama, Mtume(s. Soma Zaidi...
HISTORIA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KATIKA HARAKATI ZA KULINGANIA DINI
Soma Zaidi...
Uteuzi wa Uthman bin Al-'Afan khalifa wa Tatu baada ya Mtume
Soma Zaidi...
HISTORIA YA KUPASULIWA KWA KIFUA AU TUMBO CHA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) AKIWA MTOTO KWA BI HALIMA
KUPASULIWA KWA KIFUA MTUMEWAKATI AKIWA MTOTO. Soma Zaidi...
Maadui wa uislamu na mbinu zao: wanafiki, makafiri, mayahudi, wakristo,
Upinzani dhidi ya Dola ya Kiislamu Madinah. Soma Zaidi...
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Nuhu(a.s)
(i) Tuanze kulingania kwa Tawhiid – kumjua Allah(s. Soma Zaidi...
Makubaliano ya Mkataba wa Al Fudhul
Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 13. Hapa utajifunza historia ya Mkataba wa al fudhul na makubaliano yake. Soma Zaidi...
Bara la Arabu Zama za Jahiliyyah
Wakati Mtume(s. Soma Zaidi...