tarekh 3
KUCHIMBWA UPYA KISIMA CHA ZAMZAMKwa kifupi ni kuwa Abdul-Muttalib alipata agizo kutoka ndotoni kuwa achimbe kisima cha zamzam, na akaelekezwa sehemu ya kupachimba.
KUCHIMBWA UPYA KISIMA CHA ZAMZAM
Kwa kifupi ni kuwa Abdul-Muttalib alipata agizo kutoka ndotoni kuwa achimbe kisima cha zamzam, na akaelekezwa sehemu ya kupachimba. Basi akachimba na ndipo akakuta chini ya kisima vitu ambavyo vilifukiwa pamoja na kisima. Walofukia vitu hivi ni watu kutoka kabila la Jurhum. Hawa pindi walipolazimika kuondoka Maka walikifukia kisima cha zamzam na kufukia baadhi ya vitu vya thamani kama mapanga, nguo za vita, na dhahabu. Baada ya hapo mlango wa alkaβaba ukatengenezwa kwa hii dhahabu waloipata. Na unyweshwaji wa maji ya zamzam kwa mahujaji ukarudi upya.
Basi kisima cha zamzam kilipoanza kutoa maji, watu kutoka kabila la quraysh walitaka kufanya makubaliano juu ya maji yale lakini Abdul Al-Muttalib alikataa kwa kudai kuwa Allah amempa mamlaka yeye tu. Basi wakakubaliana wakamuulize kuhani kutoka ukoo wa Bani Saβad juu ya swala hili. Basi Allah akawaonesha alama za ukweli juu ya madai ya Abdul Al-Muttalib. Baada ya hapo mzee Abdul Al-Muttalib kwa shukran yake kwa Allah akaapa kumtoa kafara mtoto wake kwa Mwenyezi Mungu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Dua za Mitume na Manabii π2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina π3 Simulizi za Hadithi Audio π4 ai web app π5 Madrasa kiganjani π6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
HISTORIA YA MTUME ILYASA(A.S)
Mtume Ilyasa ni mmoja wa Mitume waliotumwa kupitia kizazi cha Bani Israil.
Soma Zaidi...Sababu za makafiri wa kiqureish kuupinga ujumbe wa uislamu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...NI UPI MKATABA WA AL-FUDHUL NA ASILI YAKE, ATHARI ZAKE NA WALOHUSIKA
MKATABA WA AL-FUDHULBaada ya vita hivi viongozi wa pande mbili hizi waliamuwa wakae chini na wakubaliane kuweka kanun i na utaratibu utakaozuia kutotokea uonevu kama huuu tena.
Soma Zaidi...