image

Historia ya maimam Wanne wa fiqh

Historia ya maimam Wanne wa fiqh

Maimamu Wanne wa Fiq-hi



Pamoja na kutokea mara kwa mara viongozi wema waliojitahidi kuirejesha jamii ya Kiislamu katika sura yake asilia, kama alivyojitahidi ‘Umar bin Abdul Aziz, viongozi wengi waliendelea kuutawala ulimwengu wa Waislamu kwa kuimarisha Ufalme na Udikteta zaidi kuliko Uislamu. Lakini, pamoja na kuwepo hawa watawala waovu, bado palikuwepo watu wema katika miji mbali mbali ya Dola hizo za Kifalme. Kwamfano, mji wa Baghdad ulijaa watu ambao walikamatana na Uislamu. Aidha walikuwepo viongozi wa dini ambao, pamoja na kutotambuliwa na watawala, walisimama imara kuwaongoza Waislamu. Pamoja na maguvu na vyombo vya Dola vya kutisha walivyokuwanavyo watawala bado, raia waliwaheshimu na kuwatii zaidi viongozi wao wa kiislamu.


Katika kupanuka dola ya Kiislamu, tangu wakati wa Makhalifa wanne wa Mtume(s.a.w), matatizo kadhaa yaliibuka ambayo yalihitaji ufumbuzi. Dola ilipanuka toka mashariki ya kati hadi Asia yote, sehemu za Afrika ya kaskazini na Hispania (Spain) huko Ulaya. Yaliibuka matatizo ya kisheria, taratibu za kibiashara na uchumi kwa ujumla na mila na desturi za watu mbalimbali . Uislamu ulitakiwa utoe fa-twa. Vinginevyo zingeibuka sheria na kanuni tofauti na Uislamu. Juhudi za mwanzo zilizofanywa ilikuwa ni utungaji na utoaji wa Fat’wa juu ya masuala mbalimbali kulingana na Qur’an na Sunnah. Hiki ndicho kipindi cha “Tabiina” ambacho waliibuka Maimamu wanne waliotumia uhai wao wote katika kutoa ufafanuzi, rai na Fat’wa juu ya sheria za Kiislamu katika mas’ala mbalimbali ya maisha. Hawa ni mabwana: Nu’man Ibn Thabit Abu Hanifa, Malik Ibn Anas, Muhammad Ibn Idris al- Shafii na Abu Abdallah bin Muhammad Ahmad Ibn Hambal. Wote hawa walitoa mchango mkubwa sana katika sheria ya Kiislamu na walikubaliana katika mambo yote ya msingi (Usul). Hawakufarakana kwa tofauti za maoni zilizojitokeza katika mambo madogo madogo.


Imam Abu Hanifa (80-150 A.H) na Imam Malik Ibn Anas (93-179 A.H) walirithi elimu ya moja kwa moja toka kwa masahaba iliyoegemea Qur’an na Sunnah. Aidha wao wenyewe walifanya juhudi kuongeza ujuzi wao kulingana na mazingira mapya yaliyokuwa yakijitokeza.


Imam Shafii (150 - 204 A. H) aliendeleza juhudi za Abu Hanifah na Malik kwa kufanya utafiti zaidi wa ukusanyaji na uchujaji wa Hadith, na maoni ya wataalamu mbalimbali wa sheria.


Imam Ahmad bin Hambal (164-204 A.H) aliandika Musnad ambacho ndicho kitabu mashuhuri kabisa cha Sunnah.



Maimamu wote hawa ama wamesoma na kufundishana au kusoma kwa Waalimu sawa. Imam Malik na Abu Hanifa wote walisoma Hadith kutoka kwa Imam Muhammad Ibn Shihab al-Zuhr.


Imam J’afar al-Sadiq aliwahi kuwa mwalimu wa wote Imam Abu Hanifa na Imam Malik. Aidha, wote hawa walisomeshwa pia na “Tabii” mashuhuri Muhammad bin al-Mukadir al-Madani.


Imam Abu Hanifah pamoja na utu uzima wake, alikuwa akihudhuria darasa hasa la Hadith la Imam Malik. Imam Shafii pia alisoma kwa Imam Malik. Kwa ujumla Maimamu wote wanne walihusiana sana katika kusoma kwao na japo walitofautiana katika maoni juu ya mambo kadhaa, walikuwa wamoja katika Uislamu na wakiheshimiana.


Hivi leo wapo watu wanaojinasibisha na madhehebu ambao hudai yapo madhehebu manne ndani ya Sunni wal-Jamaa, kila madhehebu ikinasibishwa na mmoja wa Maimamu hao wanne. Na japo haisemwi wazi wazi, lakini zipo hisia kwa mfano wanaojiita Shafii kuwaona wale wa Hambal, Hanafi na Malik kuwa hawapo sawa. Pengine na kinyume chake. Lakini hakika ya mambo na ushahidi wa vitabu vya historia haioneshi popote mabwana hawa kuhusika na fikra hizi za kuwa na madhehebu yasiyochanganyika. Kazi yao kubwa waliyofanya ni kutoa ufafanuzi wa kifiqh juu ya mas’ala mbalimbali na sio kuwagawa Waislamu kwenye madhehebu. Katika Uislamu suala la madhehebu ni uzushi. Labda ni vyema tuangalie kwa ufupi maisha na mchango wa kila Imam katika kuhuisha Uislamu.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1418


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

HISTORIA YA MTUME ILYASA(A.S)
Mtume Ilyasa ni mmoja wa Mitume waliotumwa kupitia kizazi cha Bani Israil. Soma Zaidi...

Kuandaliwa Mtume(s.a.w) maandalizi ya kimafunzo na maandalizi ya ki ilham
Mitume huzaliwa Mitume. Soma Zaidi...

Chanzo cha vita vya Ngamia Vita Kati ya Bibi Aisha na Khalifa Ali
Soma Zaidi...

Yusufu(a.s.) Akutana na Ndugu Zake
Njaa ilitokea na ikawa hapana sehemu nyingine yoyote yenye chakula ila Misri. Soma Zaidi...

Maswali kuhusu Quran
Quran (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII IBRAHIIM(A.S) NA KUANDALIWA KWAKE:
Nabii Ibrahiim(a. Soma Zaidi...

Nini maana ya tabii tabiina
Soma Zaidi...

Historia ya Dhana ya Kudhibiti Uzazi
Soma Zaidi...

Hatua ya Serikali Dhidi ya Waanzilishi wa Fitna na Farka wakati wa khalifa
Soma Zaidi...

Jifunze historia ya uislamu toka mitume na manabii, kuja kwa makhalifa na maimamu hadi leo
Soma Zaidi...

NAMNA MTUME(S.A.W) ALIVYOSIMAMISHA DOLA YA KIISLAMU MADINAH
Safari ya Mtume(s. Soma Zaidi...

Waliomshambulia na kumuuwa Ali, makhawariji na si muawiya
Soma Zaidi...