Imam Abu Hanifah
Imam Abu Hanifah ndiye anayenasibishwa na madhโhab ya Hanafi. Jina lake kamili ni Nuโman bin Thabit Abu Hanifah. Imam Abu Hanifah alizaliwa Kufa, Iraq katika mwaka wa 80 baada ya Hijrah. Yeye ni katika watu wa kipindi cha Tabiin kwani aliwashuhudia maswahaba wa Mtume ikiwa ni pamoja na Khalifa bin Abu Taalib, Anas bin Malik na Sahl bin Saโd. Alipata elimu katika miji ya Kufa na Basra kisha Makka na Madinah. Miongoni mwa waalimu wake alikuwa Abdallah bin Umar mtoto wa Khalifa Umar bin Khattaab. Pamoja na kujikusanyia elimu nyingi na umaarufu kutokana na elimu na ucha Mungu wake; Imam Abu Hanifah alibakia kuwa mnyenyekevu na mwenye msimamo usiotetereka.
Mwaka 146 A.H Khalifah Mansur alimteua Abu Hanifah awe Kadhi; lakini alikataa akitoa hoja kuwa nafasi hiyo ni nzito kuliko uwezo wake. Mansur alikasirika na kumwambia Imam Abu Hanifah kuwa ni mwongo. Imam Abu Hanifah alimjibu, โkama mimi ni mwongo basi kauli yangu kuwa sifai ni sahihi kwani mwongo hawezi kuchaguliwa kuwa Kadhiโ. Mansur alikasirika zaidi na kumtupa gerezani Imam Abu Hanifah.
Hata hivyo, kutokana na vilio vya watu ilibidi Mansur aruhusu Imam Abu Hanifah aendeshe darsa hapo hapo jela. Lakini alivyoona watu wanazidi kufurika jela kuhudhuria darsa, alimpa sumu Abu Hanifah akafa katika mwezi wa Rajab 150 A.H., miaka kumi na nane (18) tangu Abbasids kushika mamlaka.
Jeneza lake liliswaliwa mara sita na kila mara watu zaidi ya hamsini elfu walisimama kumswalia. Na hata baada ya kuzikwa watu toka sehemu mbalimbali duniani walifurika kuja kuswali swala ya jeneza.
Umeionaje Makala hii.. ?
Tumeona katika historia yake kuwa Nabii Ibrahiim(a.
Soma Zaidi...Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Katika Qur,an tukufu, Mwenyezi Mungu aliye muweza na mjuzi wa mambo anathibitisha kuwa aliyesulubiwa si Nabii Isa(a.
Soma Zaidi...Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 13. Hapa utajifunza historia ya Mkataba wa al fudhul na makubaliano yake.
Soma Zaidi...KULELEWA NA BABA YAKE MDOGOBaada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake.
Soma Zaidi...KAZI ALIZOKUWA AKIFANYA MUHAMMAD (S.
Soma Zaidi...