Kama tulivyoona katika maisha ya Mtume Ibrahim(a.
Kama tulivyoona katika maisha ya Mtume Ibrahim(a.s.), Nabii Ismail (a.s.) alishirikiana na baba yake kuinua kuta za Ka’abah ambayo ndiyo nyumba kongwe ya kufanyia Ibada na kituo kikuu cha kwanza cha harakati za Kiislamu duniani.
“...........Na tulimwusia Ibrahim na Ismail (tukawaambia): Itakaseni nyumba yangu kwa ajili ya wale wanaoyoizunguka kwa ajili ya kutufu na wanaokaa hapo na (kwa ajili ya) wanaorukuu na kusujudu hapo pia” (2:125).
“Na (kumbukeni khabari hii) Ibrahim alipoinua kuta za nyumba (hii ya Al-Ka’bah) na Ismail (pia) (wakaomba, wakasema): “Ee Mola wetu! Tutakabalie (amali yetu hii ya kujenga huu msikiti). Hakika wewe ndiwe Mwenye kusikia, na Mwenye kujua”. (2:127).
Nabii Ismail(a.s) ndiye chimhuko la kabila la Quraysh. Baada ya kuachwa katika bonde la Makka lililokavu, Allah(s.w) alijaalia kupatikana maji na hatimaye watu kuhamia pale. Uhai wa mji ukaanza na kutokana na kizazi cha Ismail(a.s) wakapatikana Waarabu wa Hijaz (Saudi Arabia) ambao hufahamika kwa jina mashuhuri Banu Quraysh. Qur’an imemtaja Ismail(a.s) kuwa alikuwa Mtume mkweli wa ahadi aliyewausia watu wake swala na zakat.
“Na mtaje katika kitabu (hiki) Ismail. Bila shaka yeye alikuwa mkweli wa ahadi, na alikuwa Mtume, Nabii. Na alikuwa akiwaamrisha watu wake Sala na Zakat na alikuwa mridhiwa mbele ya Mola wake”. (19:54-55).
Qur’an hapa haimtaji Ismail kwa wema kwa vile alikuwa mtoto wa Mtume Ibrahim(a.s.), bali kwa vile alikuwa mtumishi wa Allah aliye mkweli, muamrisha mema na mkataza maovu. Nasaba hapa haikutajwa kabisa.
Baada ya MtumeIbrahiim(a.s) na mwanae Ismail kujenga upya Ka’bah na kutangaza Hija, walimwomba Allah(s.w) alete Mtume atokanaye na kizazi chao ambaye ataendeleza harakati za Kiislamu kama walivyofanya wao. Aidha walikiombea kizazi chao kiwe ni cha watu wanyenyekevu:
“Ee, Mola wetu! Utufanye tuwe wanyenyekevu kwako. Na miongoni mwa kizazi chetu (pia ufanye) umma mnyenyekevu
kwako. na utuonyeshe njia ya Ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.(2:128)
“Ee, Mola wetu! Waletee Mtume anayetokana na wao, awasomee Aya zako, na kuwafundisha kitabu (chako) na hikma na awafundishe kujitakasa (na kila mabaya). Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu Mwenye hikima” (2:129).
Dua hii ilikuwa kabuili. Ilipofika zama za kuletwa Mtume wa mwisho, Allah(s.w.) akamleta kupitia kizazi cha Bani Quraysh ambao wanatokana na Ismail(a.s). Ndiye Mtume wetu Muhammad (s.a.w.).
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 622
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh
👉2 kitabu cha Simulizi
👉3 Simulizi za Hadithi Audio
👉4 Kitabu cha Afya
👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6 Madrasa kiganjani
Upinzani Dhidi ya Ujumbe wa Mtume(s.a.w)
Mtume(s. Soma Zaidi...
HISTORIA YA FAMILIA YA MTUME MUHAMMAD S.A.W
Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 02. Soma Zaidi...
Si Yesu Aliyesulubiwa (yesu hakufa msalabani wala hakusulubiwa
Katika Qur,an tukufu, Mwenyezi Mungu aliye muweza na mjuzi wa mambo anathibitisha kuwa aliyesulubiwa si Nabii Isa(a. Soma Zaidi...
tarekh 3
KUCHIMBWA UPYA KISIMA CHA ZAMZAMKwa kifupi ni kuwa Abdul-Muttalib alipata agizo kutoka ndotoni kuwa achimbe kisima cha zamzam, na akaelekezwa sehemu ya kupachimba. Soma Zaidi...
Historia ya Vijana wa Pangoni
Makafiri wa Kiquraish walikuwa na tabia ya kumghasi Mtume(s. Soma Zaidi...
Mbinu za Mtume Salih(a.s) Katika Kulingania Uislamu
Kama Mitume waliotangulia, Nabii Salih(a. Soma Zaidi...
Vitimbi vya Wapinzani Dhidi ya Ujumbe wa Nabii Shu’ayb(a.s)
Kama ilivyokuwa katika kaumu zilizotangulia, waliomuamini Shu’ayb(a. Soma Zaidi...
Imam Malik Ibn Anas
Soma Zaidi...
Ugonjwa wa Mtume(s.a.w) na Kufariki kwake
Miezi miwili baada ya Hijjat-al-Wada, Mtume(s. Soma Zaidi...
Maana ya kusimamisha uislamu katika dini
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
HISTORIA YA KUZALIWA KWA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) NA MAMA AMINA MKE WA ABDALLAH MTOTO WA ABDUL-AL MUTALIB
KUZALIWA KWA MTUME (S. Soma Zaidi...
Hatua ya Serikali Dhidi ya Waanzilishi wa Fitna na Farka wakati wa khalifa
Soma Zaidi...