Miujiza Kama Ushahidi wa Utume wa Nabii Musa(a.s)
Allah(s.
Miujiza Kama Ushahidi wa Utume wa Nabii Musa(a.s)
Allah(s.w) alimjaalia Nabii Musa(a.s) miujiza ya kuthibitisha Utume wake. Miujiza si viinimacho kama ilivyo mazingaombwe. Muujiza ni jambo halisi lisilola kawaida ambalo hutokea kwa idhini ya Allah(s.w). Musa alipoulizwa na Allah(s.w) kuwa ameshika nini alisema:
.............Akasema: โHii ni fimbo yangu, ninaiegemea na ninaangushia majani kwa ajili ya wanyama wangu. Tena ninaitumia kwa mambo mengine.(20:18)
Inadhihirika hapa kuwa Nabii Musa alikuwa na fimbo ya kawaida kabisa, lakini Allah(as) anaigeuza kuwa muujiza.
Allah(s.w) akasema: Itupe, ewe Musaโ. Akaitupa. Mara ikawa nyoka anayekwenda mbio. Allah akasema: โIkamate wala usiogope, sasa hivi Tutairudisha hali yake ya kwanza.(20:19-21)
โNa uambatanishe mkono wako katika kwapa lako; utatoka ukiwa mweupe sana pasipo na ubaya wowote. Huu ni muujiza mwingine. Ili Tukuoneshe miujiza mingine mikubwa (20:22-23)
Inabainika wazi kuwa chanzo cha miujiza yote aliyokuwa nayo Musa na Mitume wengine, ni Allah(s.w). Hakuna Mtume au Nabii aliyefanya miujiza kwa uweza wake mwenyewe!
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
๐1 kitabu cha Simulizi ๐2 Dua za Mitume na Manabii ๐3 web hosting ๐4 Bongolite - Game zone - Play free game ๐5 Madrasa kiganjani ๐6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Mtume Muhammad alelewa na mama yake mzazi akiwa na umri wa miaka 4.
Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 8. Hapa utajifunza malezi ya Mtume kutokakwa Halimavkuja kwa mama yake.
Soma Zaidi...Nani alikuwa ni Sahaba wa kwanza kufariki akiwa Shahidi
Sahaba wa kwanz akufariki akiwa shahidi, alifariki kwa sababu ya mateso aliyoyapata kutoka kwa Makafiri wa ki Quraysh
Soma Zaidi...