Tukio la kupasuliwa kifua Mtume Muhammad S.A.W
Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W, sehemu ya 7
KUPASULIWA KWA KIFUA MTUMEWAKATI AKIWA MTOTO.
Mtume alipokuwa mtoto tukio hili la kupasuliwa kwa kifua chako na kutolewa moyo wake na kusafishwa. Yote haya yalitokea kipindi akiwa analelewa na bi Halima katika kabila la bani Sa’ad. Wanazuoni wa sirah wameeleza kwa urefu tukio hili jinsi lilivyotokea. Na hapa tutaangalia kwa ufupi tu.
Ni kuwa siku moja mtume (s.a.w) alikuwa anacheza na watoto wenzie. Ghafla akatokea mtu mmoja naye ni Jibrib akamshika Muhammad na kumlaza chini kisha akamtoa moyo wake na kuuosha kwa maji ya zamzam na aliondoa uchafu wa shetani kisha akaurudisha kwenye kifua na kukifunika.
Watoto walokuwa wakicheza na Mtume (s.a.w) wakakimbia na kwenda kumueleza bi Halima kuwa Muhammad kauliwa. Bi Halima akatoka kwa haraka kufika akamkuta Muhammad akiwa amebadilika rangi. Muhammad alikuwa ni mzima wa afya, hapa bi Halima alipata mashaka makubwa mpaka akawa na hofu juu ya kuendelea kumlea kijana Muhammad.
Katika maelezo mengine waandishi wa sirah wameeleza tukio hili kama kupasuliwa kwa tumbo. Kwani zimekuja nukuu kuwa sikumoja waroto walipokuwa wakisheza pamoja nao alikuwepo Muhammad (s.a.w) basi ghafla wakaja wanaume wawili walovaa nguo nyeupe (Malaika) wakaulizana ni hyu? Basi yule mwingine akajibu ndio ni huyu, wakamlaza kisha wakampasua tumbo lake na kutoa uchafu wa shetani kisha wakafunika kama lilivyo. Basi watoto walokuwa wakicheza nae wakaenda mbio kusema wa bi halima na alipokuja kuulizwa Muhammad (s.a.w) akasema kuwa watu wawili wamekuja na kunipasua tumbo langu. Utapata maelezo zaidi ya kisa hiki kwenye kitabu kiitwacho Nurul- Yaqin.
Bi Halima aliendelea kumlea Mtume (s.a.w) kwa muda wa miaka miwili mingine hata alipotimiza miaka minne aliamuwa kumrudisha mtoto kwa mama yake. Alihofia kuendelea kumlea mtoto huyu huenda akapatwa na jambo. Miaka minne alikuwa imemtosha mtoto huyu kuwa na mwili imara na kuweza kuzungumza lugha ya kiarabu wa ufasaha tofauti na watoto walolelewa maeneo mengine.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
HISTORIA YA BANI ISRAIL
Nabii Musa na Harun walikuwa na kazi kubwa mbili; kwanza, kuwakomboa Bani Israil kutokana na dhuluma waliyokuwa wakifanyiwa na Firaun na Serikali yake, na pili, kuwarudisha kwenye nchi yao takatifu ya Palestina.
Soma Zaidi...Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Adam(a.s)
(i) Utukufu wa mtu katika Uislamu hautokani na nasaba, rangi,kabila,utajiri ila uwajibikaji kwa Allah(s.
Soma Zaidi...Mtume kumuoa bi khadija
Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 15. Hapa utajifunza kuhusu chimbuko la ndoa ya Mtume s.a.w na bi Khadija.
Soma Zaidi...Yusufu Aokotwa na Kuuzwa nchini Misri
Huko nyuma wapita njia walikisogelea kisima kwa lengo la kuteka maji.
Soma Zaidi...Kulingania watu wake na Miujiza Aliyoonyesha Nabii Isa(a.s)
Mwenyezi Mungu pekee ndiye aliyewawezesha Mitume na Manabii kufanya miujiza.
Soma Zaidi...Chokochoko na Upinzani wakati wa khalifa uthman khalifa wa Tatu
KUPOROMOKA KWA DOLA YA KIISLAMU ALIYOICHA MTUME(S.
Soma Zaidi...