Kuanzishwa Ufalme.Muawiyah kwa kumrithisha mtoto wake, Yazid, uongozi wa Dola, bila kuzingatia utaratibu wa kuchangua viongozi kutokana na sifa stahiki, alivunja maongozi ya Kiislamu na kuasisi utawala wa kifalme au utawala wa kiukoo ambao mpaka leo unaendelezwa katika nchi nyingi za Arabia(Bara Arab), Saud Arabia ikiwa miongoni.


Dola ya kifalme aliyoiasisi Muawiya ilitafautiana na Dola ya Kiislamu aliyoiasisi Mtume(s.a.w) na kuendelezwa na Makhalifa wanne waongofu, Abubakar, ‘Umar, Uthman na Ali, kwa sababu:(i) Taasisi ya shura ilivyunjwa na raia walipokonywa uhuru wao wa kutoa maoni na kukosoa viongozi


(ii) Hazina ya Dola – Baitul-Mali, ilifanywa mali ya nyumba ya mfalme ambapo mfalme aliitumia atakavyo kwa maslahi yake binafsi na familia ya kifalme.


(iii)Tabia za kijahili za majivuno ya kikabila na nasaba ziliibuka na kustawishwa na ufalme.


(iv)Watawala (viongozi mbali mbali wa dola) walianza kuishi kwenye mahekalu na nyumba za kifahari za Kifalme.


(v) Suala la kutenganisha maongozi ya Serikali na Dini liliibuka.Masheikh wazuri waliokuwa waadilifu walitengwa na kundi la watawala. Wao wakawa wanajitahidi kuirekebisha jamii lakini wakiwa ndani ya kuta nne za msikiti na nje ya vyombo vya dola.