image

Mapambano Dhidi ya Maadui wa Dola ya Kiislamu

1.

Mapambano Dhidi ya Maadui wa Dola ya Kiislamu

Mapambano Dhidi ya Maadui wa Dola ya Kiislamu
Katika miaka yote kumi ya kipindi cha Madinah,Mtume(s.a.w) alipambana mfululizo na maadui wa Dola ya Kiislamu. Mtume(s.a.w) mwenyewe akiwa Amir Jeshi na kamanda mkuu aliongoza vita 27, vikubwa 7 na vidogo 20 katika kipindi hicho cha miaka kumi. Maadui wakubwa waliopambana na Waislamu katika kipindi cha Madinah ni:



1. Makafiri wa kabila la Kiquraish.
2.Wanafiki.
3.Mayahudi.
4.Makabila mengine ya Waarabu.
5.Warumi (wakristo).



Makafiri wa Kabila la Qiquraish

Pamoja na vitimbi vyao vikubwa walivyovifanya Makka dhidi ya Mtume(s.a.w) na Waislamu, Makuraysh waliamua kuwafuatilia Waislamu Madinah kuendeleza vitimbi vyao kama vifuatavyo:



Kwanza, walimuandikia barua kiongozi wa wanafiki, ‘Abdullah bin Ubayyi, ili amfukuze au kumuua Mtume(s.a.w) na kumtishia vita endapo hatatekeleza:

“Kwa kumpa mtu wetu(Muhammad) hifadhi (ya kiasiasa) tunakutaka kwa jina la Allah ima umuue au umfukuze Madinah lau sivyo, tutakushambulieni, tutakumalizeni na kuwateka wake zenu.”19



Pili, Maquraish waliyatishia vita makabila yaliyokuwa yakiishi kati ya Makka na Madinah ili yasije silimu na kuyachochea yawe dhidi ya Waislamu.



Tatu, Bwana mkubwa wa Maquraish, Kurz bin Jabir na wenzake walikuja kwa siri, Madinah, na kupora mifugo ya ngamia, mbuzi na kondoo na kukimbia nayo Makka.



Nne, mabwana wakubwa wa Maquraish, Habbar bin ‘Aswad na Nafii bin Qays walimchocha chocha mikuki, bibi Zaynab bint Muhammad(s.a.w) alipokuwa akihamia Madinah kumfuata baba yake. Bibi huyu aliyekuwa mja mzito aliathirika sana na ikawa ndio Sababu ya kifo chake.

Hujuma kama hizi za Maquraish za kuhatarisha usalama wa Waislamu na uchumi wao zilikithiri na ikawa ndio Sababu ya Waislamu kuruhusiwa rasmi na Mola wao kuingia vitani dhidi ya maadui zao.



Wameruhusiwa (kupigana) wale waliopigwa, kwa Sababu wamedhulumiwa.Na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia. (22:39)



Na piganeni nao (makafiri) mpaka yasiweko mateso (nyinyi kuteswa na wao kwa ajili ya dini kama wanavyokuteseni sasa); na dini iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.Lakini wakiacha, basi hakika Mwenyezi Mungu anayaona wanayoyatenda. (8:39)



Ruhusa hii iliwafanya Waislamu walijizatiti kivita kupambana na maadui zao hawa na wengine wote walioibuka baadaye.



Mtume(s.a.w) na jeshi lake alipambana na Maquraish katika vita vikubwa vya Badr, Uhud na Ahzab. Waislamu walipata ushindi mkubwa katika vita vya Badr pamoja na udhaifu waliokuwa nao ukilinganisha na nguvu ya jeshi la Maquraish. Ushindi wa Badr ni bishara njema kwa Waislamu wa zama zote kuwa watapata ushindi dhidi ya maadui wa Dini ya Allah(s.w) pale watakapojizatiti kwa kadiri ya uwezo wao kupambana na maadui hao huku wakitegemea msaada kutoka kwa Allah(s.w).



(Kumbukeni) mlipokuwa mkiomba msaada kwa Mola wenu, naye akakujibuni kuwa: “Kwa yakini Mimi nitakusaidieni kwa Malaika elfu moja watakaofuatana mfululizo (wanaongezeka tu)(8:9)




Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya ila iwe bishara (habari ya furaha) na ili nyoyo zenu zitue kwayo. Na hakuna msaada (wa kufaa) ila utokao kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu (na) Mwenye hikima. (8:10)




Na Mwenyezi Mungu alikunusuruni katika (vita vya) Badri, hali nyinyi mlikuwa dhaifu. Basi mcheni Mwenyezi Munguili mpate kushukuru (kila wakati kwa neema zinazokujieni).(3:123)

(Alikunusuruni katika vita vya badr) ulipowaambia Waislamu: “Je! Haitakutosheni Mola wenu atapokusaidieni kwa Malaika elfu tatu watakaoteremshwa?” (3:124)




Hamkuuwa nyinyi lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaua; na hukutupa wewe (Mtume ule mchanga wa katika gao la mkono wako), ulipotupa (ukawaingia wote machoni mwao); (hukufanya wewe haya) walakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyeutupa, (yaani ndiye aliyeufikisha katika macho yao wote yakawa yanawawasha kuliko pilipili, wakenda mbio) Alifanya haya Mwenyezi Mungu ili awape walioamini hidaya nzuri itokayo kwake. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye asikiaye na ajuaye. (8:17)



Pamoja na udhaifu wa baadhi ya Waislamu walioonyesha kwa kuhalifu amri ya Mtume(s.a.w) katika vita vya Uhud bado Waislamu baada ya kurudi katika twaa ya Mtume(s.a.w) waliwashinda Maquraish na kuwarejesha Makka mbio mbio.



Katika vita vya Ahzab, maquraish walikusanyana na makundi mengine ya maadui wa Uislamu ili kuunda nguvu kubwa itakayo wafuta Waislamu na Uislamu kwenye uso wa dunia. Waislamu walifanya jitihada kubwa ya kujihami kwa kuchimba handaki kubwa kuzunguka mji wa Madinah. Angalia ramani ya uwanja wa vita vya Handaq.



Maadui kwa uwezo wa Allah walishindwa kulivuka lile handaki, wakabakia wakiwazingira Waislamu kwa takriban mwezi mmoja. Baadaye Allah(s.w) alileta majeshi yake ya mbinguni na ardhini kuwanusuru Waislamu. Allah(s.w) anatukumbusha:




Enyi mlioamini! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yenu; lilipokujieni jeshi; basi tukatuma upepo dhidi yao na majeshi msiyoyaona; na Mwenyezi Mungu amekuwa ni mwenye kuyaona mnayoyatenda. (33:9)
Hali ngumu ya Ahzab, iliwafanya Waislamu kuwa imara na wagumu zaidi kwa maadui zao:



Na Waislamu (wa kweli) walipoyaona majeshi (ya makafiri yamewashambulia hivyo), walisema, “Haya ndiyo Aliyotuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (kuwa tutapata misukosuko, kisha tutashinda). Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wamesema kweli;” na (jambo hili) halikuwa zidishia ila imani na utii. (33:22)



Hivyo Maquraish hawakuwa na uwezo tena wa kukabiliana na Waislamu na hatimaye wenyewe waliomba suluhu iliyopelekea kupatikana kwa mkataba wa amani wa Hudaybiya uliopelekea kuwashinda Maquraish na kupatikana “Fat-h Makkah”..



                   



           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 243


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Kuanzishwa kwa dola ya kiislamu madinah
Dola ya kiislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Maandalizi ya Kimafunzo aliyoandaliwa Mtume Muhammad
(i) Suratul- ‘Alaq (96:1-5)“Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba Aliyemuumba mwanaadamu kwa ‘alaq. Soma Zaidi...

Kuhifadhiwa kwa Quran
Quran (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Historia ya Dhulqarnain
Dhulqarnain sio jina la mtu bali cheo, maana yake ikiwa: “Mwenye Pembe Mbili”. Soma Zaidi...

Historia ya bi Khadija na familia yake na chanzo cha utajiri wake.
Sira na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 17. Historia ya Bi Khadija na familia yake. Soma Zaidi...

Historia ya Luqman mtu aliyesifika kuwa na Hikma
Luqman ni katika watu wema kabisa waliopita zama za nyuma. Soma Zaidi...

MASWALI MUHIMU KUHUSU HISTORIA NA MAISHA YA MTUME (S.A.W)
1. Soma Zaidi...

Kisa cha Malkia wa Sabaa.
Sabaa ulikuwa mji katika nchi inayojulikana leo kama Yemen. Soma Zaidi...

Je waislamu walishindwa vita vya Uhudi?
Katika vita vya Uhudi waislamu walikufa wengi kulinganisha na makafiri. Lakini makafiri walikimbia uwanja wa vita baada ya kuzidiwa. Je ni nanibalishindwa vita vya Uhudi kati ya waislamu na makafiri? Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Isa(a.s)
Kutokana na Historia ya Nabii Isa(a. Soma Zaidi...

Sifa au vigezo vya dini sahihi
Dini sahihi anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Vita vya badri
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...