image

Mpango wa kumuuwa Khalifa ally na Gavana Muawiya

Mpango wa kumuuwa Khalifa ally na Gavana Muawiya

Kutekwa kwa Makka, Madina na Yemen



Katika mwaka wa 40 A.H. Amir Muawiya alimtuma Busr Ibn Abi Artat na watu elfu tatu kwenda Hijazi ambako aliiteka Madina, Makka na mji wa Sanaa, Yemen na kuwataka wamtii Muawiyah. Huko Yemen aliua watoto wadogo wawili wa Gavana wa jimbo hilo Ubaidullah ambaye alikimbilia Kufa. Vile vile aliwaua wafuasi wengi wa Ali. Jariah Ibn Qudamah akiwa na askari elfu mbili alitumwa kurudisha maeneo yaliyotekwa.


Alifanikiwa kuirejesha Sanaa mikononi mwa Khalifa kwani wakati huu Busr alikwisharudi Syria. Lakini alipofika Makka alipata taarifa ya kuuwawa kwa Ali na huu ukawa ndio mwisho wa Ali. Kuuwawa kwa Ali Baada ya vita vya Nahrwan, Khawarij waliendesha mambo yao chini chini. Inadaiwa waliendelea kuisakama Serikali.


Hawakumpenda Ali wala Muawiyah kwa sababu wao ndiyo chanzo cha kugawanyika kwa Waislamu, katika kundi la Muawiyah na kundi la Ali. Amr bin al As naye walimuona ana makosa kwa vile ndiye mshauri na afisa mipango wa Muawiya. Hivyo walipanga kuwaua wote watatu alfajiri ya mwezi 17 Ramadhan 40 A.H. wakati wa swala ya Alfajiri. Ilipangwa Ali auliwe na Abdur-Rahman Muljam. Muawiya auliwe na Bark Ibn Abdullah na Amr bin al As auliwe na Amr ibn Bark.


Wauwaji hawa walitia sumu kali katika majambia yao na wote wakafanya kazi yao kama walivyopanga Misri, Syria na Kufa. Lakini matokeo hayakuwa mia kwa mia. Ali alijeruhiwa vibaya na jeraha lilisababisha kifo chake kilichotokea jioni ya mwezi 20 Ramadhan 40 A.H. Muljam alikamatwa na kuhojiwa. Kabla hajafa Khalifa Ali aliwaita watoto wake na kuwausia kumcha Mungu. Lakini alipoulizwa kama Hassan atawazwe Ukhalifa alisema, “Nawaachia Waislamu waamue”. Khalifa Ali alitawala kwa miaka mine na miezi tisa. Alikufa akiwa na miaka 63.



Baada ya Khalifa Ali kuuliwa, mtoto wake, Hassan, alichaguliwa kuchukua nafasi ya Ukhalifa lakini Muawiyah aliasi na kuandaa jeshi dhidi yake. Baada ya mapigano kidogo, Hassan alizidiwa nguvu na akaona amwachie Muawiyah Ukhaifa kwa makubaliano kuwa baada yake uongozi uchukuliwe na ndugu yake, Hussein bin Ali. Kinyume na makubaliano hayo, ambayo pia hayakuwa ya Kiislamu, Muawiyah kabla hajafa, alimteua mtoto wake, Yazid bin Muawiyah kushika uongozi wa Dola baada yake.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 214


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Mtume kumuoa bi khadija
Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 15. Hapa utajifunza kuhusu chimbuko la ndoa ya Mtume s.a.w na bi Khadija. Soma Zaidi...

historia na maisha ya Mtume IS-HAQ(A.S.) NA YA‘AQUUB(A.S.)
Is-haq(a. Soma Zaidi...

Mtume amezaliwa mwaka gani?
Na tumemuusia mwanaadamu afanye wema kwa wazazi wake. Soma Zaidi...

Ibrahiim(a.s) Aomba Kupata Kizazi Chema
Nabii Ibrahiim na mkewe Sarah walikaa mpaka wakawa wazee bila ya kupata mtoto. Soma Zaidi...

Mawazo Tofauti Kuhusiana na Uchaguzi wa Abubakar
Soma Zaidi...

Watu wa Mji Waliomuua Muislamu kwa Kuwa Amewasadikisha Wajumbe wa Allah(s.w)
Katika Suratul Yassin Allah(s. Soma Zaidi...

NI IPI FAMILIA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) NA NI IPI NASABA YAKE, UKOO WAKE NA KABILA LAKE
FAMILIA YA MTUME (S. Soma Zaidi...

NUHU(A.S) NA WATU WAKE NA UOVU WALIOKUWA WAKIUFANYA WATU WAKE
Mtume aliyemfuatia Nabii Idrisa(a. Soma Zaidi...

Kazi na wajibu wa khalifa katika dola ya kiislamu
Kazi na Wajibu wa KhalifaKhalifa katika Serikali ya Kiislamu ndiye mtendaji mkuu wa Serikali kama alivyokuwa Mtume(s. Soma Zaidi...

Khalifa ‘Umar bin Abdul Aziz
Soma Zaidi...

MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KULELEWA NA BABA YAKE MDOGO MTUME (ABU TALIB)
KULELEWA NA BABA YAKE MDOGOBaada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake. Soma Zaidi...

Upinzani Dhidi ya Ujumbe wa Mtume(s.a.w)
Mtume(s. Soma Zaidi...