Navigation Menu



image

Historia ya Vijana wa Pangoni

Makafiri wa Kiquraish walikuwa na tabia ya kumghasi Mtume(s.

Historia ya Vijana wa Pangoni

Historia ya Vijana wa Pangoni


Makafiri wa Kiquraish walikuwa na tabia ya kumghasi Mtume(s.a.w) kwa kumuuliza maswali mara kwa mara. Lengo lao likiwa kumshusha hadhi Mtume(s.a.w) endapo atashindwa kujibu maswali hayo. Mchezo huu walikuwa wakiufanya kwa kushirikiana na Mayahudi. Walikuwa wakijifunza kutoka kwa Mayahudi baadhi ya mambo ya kale kisha hurejea kumuuliza Mtume(s.a.w) maswali. Miongoni mwa maswali waliyomuuliza Mtume(s.a.w) ni juu ya vijana wa Pangoni na habari za Dhulqarnain.



Vitabu vingi vya historia vinabainisha kuwa kisa cha vijana wa pangoni kilitokea katika mji wa Ephesus uliokuwa ndani ya Ufalme wa Urumi. Mji huu ulijulikana sana kutokana na kushamiri sana dini ya ushirikina. Watu wa huo mji waliabudia masanamu, mwezi, jua na sayari.



Baada ya Nabii Isa(a.s) kuja na mafundisho yake ya kumpwekesha Allah(s.w) yalienea hadi Ephesus. Wakatokea vijana wakayaamini na kuachana na ibada za kishirikina. Hili mfalme akaliona ni hatari kwa maslahi yake. Akawaita vijana hao ili kuwatisha warejee kwenye ukafiri na ushirikina. Lakini vijana hawakukubali kuiacha haki. Baada ya kuonyesha umadhubuti wao Mwenyezi Mungu aliwazidishia imani na kuzitia nguvu nyoyo zao. Qur’an inatuambia:

“...........Hakika wao walikuwa ni vijana waliomuamini Mola wao. Basi tukawazidishia uongofu” (18:13).



Na tukazitia nguvu nyoyo zao waliposimama (mbele ya mfalme wao kafiri) wakasema: “Mola wetu ni Mola wa mbingu na ardhi. Hatutamuabudu kabisa Mungu mwingine badala yake. (Hapo) bila shaka tutakuwa tumesema uovu uliopindukia kiasi” (18:14).

Kwa msimamo wao huo mfalme alitaka kuwadhuru, basi vijana wakakimbilia pangoni. Humo walikaa miaka mia tatu (kwa hesabu ya miaka ya jua) au miaka 309 kwa hesabu ya mwendo wa mwezi.




Vijana hao walipokimbilia katika pango na wakasema: “Mola wetu; tupe rehema zinazotoka kwako na tutengenezee uwongofu katika (kila) jambo letu”. Tukaziba masikio yao (wakalala hawasikii habri yoyote) katika pango hiyo kwa idadi ya miaka mingi” (18:10 -11).




“Na walikaa katika pango yao miaka mia tatu na wakazidisha (miaka) tisa” (18:25).



Kisha tukawafufua ili tujulishe ni lipi katika makundi mawili lililohisabu sawa sawa muda waliokaa” (18:12).

Baada ya kulala kwa miaka hiyo 309 ndipo walipozindukana. Mambo yalikuwa yamebadilika katika nchi na mateso kwa ajili ya kufuata mafundisho ya Mwenyezi Mungu yalikuwa hayapo tena. Lakini wao hawakuwa na habari. Walidhani wamelala muda mfupi tu. Hivyo walipoamka wakawa na hofu ile ile iliyowapeleka pangoni. Kuhusu hofu yao na kutokujua muda waliolala Qur’an inasema:



.................Akasema msemaji wao: “Mumekaa muda gani?” Wakasema: “Tumekaa siku moja au sehemu ya siku” (wengine) wakasema: “Mola wenu anajuwa zaidi muda mliokaa. Basi mtumeni mmoja wenu pamoja na fedha yenu hii mjini na akatazame chakula chake kipi ni tahara zaidi akuleteeni katika chakula chake. Na afanye mambo haya kwa busara wala asikutajeni kabisa kwa yoyote. “Kwani wao wakikujueni mlipo watakupigeni mawe au watakurudisheni katika Dini yao; na hapo hamtafaulu abadan” (18:19-20).



Historia imebainisha kuwa kipindi hicho vijana hao wanaamka toka usingizini wenyeji wa mji wa Ephesus na Roma yote, walikuwa na ubishani juu ya ukweli wa kufufuka na siku ya malipo. Basi kwa tukio hili ikawa ni fundisho na uthibitisho wa ukweli wa ahadi ya kufufuliwa.



“Na namna hivi tuliwatambulisha (kwa watu) ili wapate kujua ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu (ya kufufuliwa viumbe) ni kweli, na kwamba Kiama hakina shaka.............” (18:21).

Maelezo zaidi juu ya vijana wa pangoni rejea Qur’an (18:9-26).



Mafunzo yatokanayo na kisa cha vijana wa Pangoni
Kutokana na kisa cha vijana wa pangoni tunajifunza yafuatayo:



(i) Alama ya kuwepo Allah(s.w) na Uwezo wake.


Suala la vijana wa pangoni kulala miaka 309 kisha wakaamka ni la muujiza kama Qur’an yenyewe inavyobainisha:

Je! Unafikiri ya kwamba (wale) watu wa pangoni na (wenye habari) zile zilizoandikwa (vitabuni) walikuwa ajabu katika ajabu zetu”? (18:9).



Si jambo la kawaida mtu kulala kwa muda mrefu (miaka 309) hali wala hanywi na bado akawa hai. Siku 20 zaweza kuwa kiwango cha juu ambazo aweza kukaa mtu bila kula wala kunywa na bado akawa hai. Lakini tunaambiwa vijana wa pangoni walikaa siku 309. Na sio kwamba walikufa wakaoza ndio wakafufuka. Bali walikuwa wazima wakigaragara pangoni.



“Na unadhani wamacho na hali wamelala. Na tunawageuza upande wa kulia na upande wa kushoto (wanapogaragara usingizini). Na mbwa wao kanyoosha mikono yake kizingitini. Kama ungewaona hakika ungegeuka upesi kuwakimbia na hakika ungejazwa khofu juu yao” (18:18).



Huu ni muujiza wa kuonesha kuwepo kwa Allah na Uwezo wake. Aya tuliyoinukuu inatubainishia kuwa Allah(s.w) alijaaliya mazingira walimokuwa wamelala yakawa ni ya kutisha. Kwa hivyo

kwa muda wote wa miaka 309 hakuna aliyethubutu kufika karibu yao, hivyo kutogundila.



(ii) Ujasiri


Imani ya kweli juu ya Allah(s.w) hujenga ujasiri wa hali ya juu. Mtu akishamkubali Allah(s.w) kuwa ndiye Muumba wake na Mwenye Mamlaka yote juu ya Uhai wake hana sababu tena ya kumuogopa na kumtetemekea mwingine. Kufanya hivyo itakuwa ni kwenda kinyume na imani yenyewe ya Kiislamu.



(iii) Uwingi na Uzee si Hoja.


Mara nyingi maadui wa Uislamu wamekuwa wakitumia kisingizio cha vijana na uchache wa watu kutaka kuendesha udhalimu na ukandamizaji dhidi ya Waislamu. Wamekuwa wakisema hao ni vijana wachache. Kana kwamba jambo lolote lifanywalo na vijana ni baya. Lakini habari hizi za vijana wa pangoni zinaweka wazi kuwa vijana walikuwa na imani thabiti na Mwenyezi Mungu akawaongezea uongofu. Aidha wametajwa katika Qur’an ili iwe mfano kwetu.



(iv) Uthibitisho wa Utume wa Muhammad (s.a.w).

Ukizingatia ukweli kwamba habari za vijana wa pangoni zilitokea zaidi ya miaka 309 kabla ya kuja Mtume(s.a.w) na kwamba sehemu ya tukio lenyewe ni mbali sana na mazingira alimokulia Mtume(s.a.w); maelezo ya Mtume ni ushahidi tosha wa utume wake. Katika mazingira alimokulia Mtume(s.a.w) hatutegemei apate taarifa sahihi za vijana wa pangoni kwingine zaidi kuliko kwa Allah(s.w). Na hili Qur’an yenyewe inalishuhudia katika aya ifuatayo:

“Ni sisi tunakusimulia habari zao kwa kweli. Hakika wao wlaikuwa ni vijana waliomuamini Mola wao. Nasi tukawazidisha uwongofu” (18:13).



                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1440


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Madhumuni ya dola ya uislamu
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

HISTORIANA MAISHA YA MTUME ISA(A.S)
Nabii Isa(a. Soma Zaidi...

Kuangamizwa kwa jeshi la tembo mwaka alizaliwa Mtume Muhammad s.a. w
Sura na historia ya Mtume Muhammad s.sa. w sehemu ya 4. Hapa utajifunza kuhusu historia ya kuangamiza kwa jeshi la tembo. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Daud(a.s)
Kutokana historia ya Nabii Daud (a. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Zakaria(a.s) na Yahya(a.s)
Kutokana na Historia ya Nabii Zakaria (a. Soma Zaidi...

Historia ya kujengwa kwa Alkabah (Maka)
Kama tulivyoona katika maisha ya Mtume Ibrahim(a. Soma Zaidi...

Ghasia na chokochoko za Makhawariji na kuuliwa kwa Ally
Soma Zaidi...

Hali za bara arab zama za jahiliya karne ya 6 kabla ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad
7. Soma Zaidi...

TAREKH, HISTORIA NA SIRA YA UISLAMU NA MTUME MUHAMMAD KUTOKA KUZALIWA MPAKA KUFARIKI NA HARAKATI ZAKE
1. Soma Zaidi...

Maswali kuhusu hali ya bara arabu zama za jahiliyyah
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII SULEIMAN
Soma Zaidi...

Sifa za waumini zilizotajwa katika Surat Ar-Raad (13:19-26)
Soma Zaidi...