Mafunzo yatokanayo na kuanzishwa kwa dola ya uislamu madinah

Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Kutokana na mambo ya msingi aliyoyafanya Mtume (s.a.w) katika kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah tunajifunza yafuatayo;

 

  1. Hatunabudi kuanzisha na kuendesha vituo vya harakati, msikiti ukiwa ndio kitovu cha msingi.

 

  1. Mshikamano, kuhurumiana na kupendana kwa vitendo baina ya waislamu ndio nyenzo pekee katika kuhuisha na kuendeleza harakati za Kiislamu.

 

  1. Hatunabudi kuishi vizuri, kuwahesimu na kuwatendea haki, wasiokuwa waislamu hasa wale wasiopiga vita waislamu na Uislamu wazi wazi.

 

  1. Ni wajibu kwa kila muislamu kuwa mkakamavu, jasiri na kujifunza mafunzo ya kijeshi na kuwa tayari kulinda na kuupigania Uislamu katika jamii.

 

  1. Hatunabudi kuwajua vema maadui wa Uislamu na Waislamu, mbinu na silaha zao na kuchukua tahadhari dhidi yao.

 

  1. Ni wajibu kuimarisha uchumi wetu kwani ndio nyenzo muhimu na ya msingi katika kuendesha harakati za Kiislamu. 

 

  1. Uongozi bora, makini na uwajibikaji wa kila mmoja kulingana nafasi yake ndio kiungo muhimu katika kuendesha harakati za Kiislamu.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 2212

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana: