picha

Mpango wa kumuuwa Khalifa ally na Gavana Muawiya

Mpango wa kumuuwa Khalifa ally na Gavana Muawiya

Kutekwa kwa Makka, Madina na Yemen



Katika mwaka wa 40 A.H. Amir Muawiya alimtuma Busr Ibn Abi Artat na watu elfu tatu kwenda Hijazi ambako aliiteka Madina, Makka na mji wa Sanaa, Yemen na kuwataka wamtii Muawiyah. Huko Yemen aliua watoto wadogo wawili wa Gavana wa jimbo hilo Ubaidullah ambaye alikimbilia Kufa. Vile vile aliwaua wafuasi wengi wa Ali. Jariah Ibn Qudamah akiwa na askari elfu mbili alitumwa kurudisha maeneo yaliyotekwa.


Alifanikiwa kuirejesha Sanaa mikononi mwa Khalifa kwani wakati huu Busr alikwisharudi Syria. Lakini alipofika Makka alipata taarifa ya kuuwawa kwa Ali na huu ukawa ndio mwisho wa Ali. Kuuwawa kwa Ali Baada ya vita vya Nahrwan, Khawarij waliendesha mambo yao chini chini. Inadaiwa waliendelea kuisakama Serikali.


Hawakumpenda Ali wala Muawiyah kwa sababu wao ndiyo chanzo cha kugawanyika kwa Waislamu, katika kundi la Muawiyah na kundi la Ali. Amr bin al As naye walimuona ana makosa kwa vile ndiye mshauri na afisa mipango wa Muawiya. Hivyo walipanga kuwaua wote watatu alfajiri ya mwezi 17 Ramadhan 40 A.H. wakati wa swala ya Alfajiri. Ilipangwa Ali auliwe na Abdur-Rahman Muljam. Muawiya auliwe na Bark Ibn Abdullah na Amr bin al As auliwe na Amr ibn Bark.


Wauwaji hawa walitia sumu kali katika majambia yao na wote wakafanya kazi yao kama walivyopanga Misri, Syria na Kufa. Lakini matokeo hayakuwa mia kwa mia. Ali alijeruhiwa vibaya na jeraha lilisababisha kifo chake kilichotokea jioni ya mwezi 20 Ramadhan 40 A.H. Muljam alikamatwa na kuhojiwa. Kabla hajafa Khalifa Ali aliwaita watoto wake na kuwausia kumcha Mungu. Lakini alipoulizwa kama Hassan atawazwe Ukhalifa alisema, โ€œNawaachia Waislamu waamueโ€. Khalifa Ali alitawala kwa miaka mine na miezi tisa. Alikufa akiwa na miaka 63.



Baada ya Khalifa Ali kuuliwa, mtoto wake, Hassan, alichaguliwa kuchukua nafasi ya Ukhalifa lakini Muawiyah aliasi na kuandaa jeshi dhidi yake. Baada ya mapigano kidogo, Hassan alizidiwa nguvu na akaona amwachie Muawiyah Ukhaifa kwa makubaliano kuwa baada yake uongozi uchukuliwe na ndugu yake, Hussein bin Ali. Kinyume na makubaliano hayo, ambayo pia hayakuwa ya Kiislamu, Muawiyah kabla hajafa, alimteua mtoto wake, Yazid bin Muawiyah kushika uongozi wa Dola baada yake.




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Views 1152

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 ai web app     ๐Ÿ‘‰2 Kitabu cha Afya     ๐Ÿ‘‰3 Dua za Mitume na Manabii     ๐Ÿ‘‰4 Kitau cha Fiqh     ๐Ÿ‘‰5 web hosting     ๐Ÿ‘‰6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zinazofanana:

Kuanzishwa kwa dola ya kiislamu madinah

Dola ya kiislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
HISTORIA YA BANI ISRAIL

Nabii Musa na Harun walikuwa na kazi kubwa mbili; kwanza, kuwakomboa Bani Israil kutokana na dhuluma waliyokuwa wakifanyiwa na Firaun na Serikali yake, na pili, kuwarudisha kwenye nchi yao takatifu ya Palestina.

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa Mtume(s.a.w) na Kufariki kwake

Miezi miwili baada ya Hijjat-al-Wada, Mtume(s.

Soma Zaidi...
tarekh 09

KULELEWA NA BABU YAKE:Mzee โ€˜Abdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana.

Soma Zaidi...
Mtume Muhammad s.a.w analelewa na Babu yako ikiwa na umri wa miaka 6

Sura na historia ya Mtume Muhammad s.a. w sehemu ya 9.

Soma Zaidi...