Upinzani Dhidi ya Dola ya Kiislamu Wakati wa Makhalifa

Katika kipindi cha Makhalifa wanne wa Mtume (s.a.w), maadui wa Dola ya Kiislamu ni wale wale waliokabiliana na Mtume na kuainishwa katika Qur-an japo walitofautiana kimbinu kulingana na mazingira. Maadui wakubwa walioainishwa katika Qur-an ni:

(i) Adui mkubwa – Sheitwaan (katika Majini na Watu) anayepambana kwa kuishawishi na kuipambia nafsi ya mtu ili imuasi Mola wake.

(ii) Makafiri na Washirikina – Wanaotaka mifumo yao ya maisha iwe juu ya Uislamu.

(iii) Wanafiki – wanaotaka kuishi maisha ya mseto baina ya Uislamu na ukafiri kwa ajili ya maslahi ya dunia.

(iv)Mayahudi - husuda na chuki yao dhidi ya Uislamu ilibainika tangu wakati wa Mtume(s.a.w) - kwa ajili ya kuipenda dunia kuliko akhera.

(v) Wakristo wanachuki na husuda dhidi ya Uislamu kama Mayahudi.