Ulinzi na Usalama
Wakati wa Ukhalifa wa Makhalifa wanne ulinzi uliimarishwa kwa kiwango kikubwa. Wakati wa Mtume(s.a.w) hakukua na jeshi maalum. Kila mtu alikuwa askari na vita ilipofika Waislamu walijitokeza wakapewa mafunzo na kwenda vitani. Ni kweli pia kuwa katika Dola ya Kiislamu kila Muumin ni askari wa Allah(s.w) na wakati wowote anapotakiwa ni lazima awe tayari kupigania dini ya Mwenyezi Mungu.
“Enyi mlioamini Je! Nikujulisheni biashara itayokuokoeni na adhabu iumizayo(61:10).
Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na piganieni dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu.......” (61:11)
Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waislamu nafsi zao na mali zao ili nae awape Pepo. Wanapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu wanauwa na wanauwawa.............” (9:111)
Ni dhahiri Waislamu ni askari wa Mwenyezi Mungu. Pamoja na hivi tangu wakati wa Khalifa wa pili Umar, liliundwa jeshi kama yalivyo majeshi ya kileo. Khalifa ndie aliyekuwa mkuu wa majeshi, aliteua kamanda wa jeshi na makamanda wa mikoa na wilaya.
Idara ya ulinzi ilianzishwa na askari wote waliorodheshwa na utaratibu wa mshahara na posho ulianza kutumika kwa askari wa kudumu, wakujitolea na wale waliopigana vita vya awali kama Badr, Uhud, n.k.
Nchi iligawanywa kwenye maeneo ya kiulinzi, makao makuu ya maeneo haya yakawa Madina, Kufa, Basra, Mosul, Fustat, Damaskas, Hems, Jordan na Palestine. Katika sehemu zote hizi kambi zilijengwa kwa ajili ya askari. Mashamba ya mifugo yalipanuliwa kwa matumizi ya farasi na ngamia wa vita.
Pamoja na askari wa farasi na wa miguu jeshi la maji lilianza katika Ukhalifa wa Uthman. Vita vya kwanza vya majini vilipiganwa na Muawiya alipovamia Cyprus mnamo mwaka wa 28 A.H. Makao makuu ya Jeshi la maji yalikuwa Alexandria Misri.
Usalama wa Taifa
Idara ya usalama ilikuzwa. Ilianza tangu wakati wa Mtume(s.a.w) na kuendelezwa wakati wa Makhalifa wanne. Walitumika wanajeshi na wasio wanajeshi katika kazi ya kupata habari ndani na nje ya Dola na hasa kujua mwenendo wa adui. Wapo Machief, kwa mfano Syria, waliochaguliwa kuwa wanausalama, kuchunguza mwenendo wa Warumi. Palestine lilikuwepo kundi la Wayahudi lililojulikana kwa jina la Samara lilijizatiti katika upelelezi. Khalifa Umar(r.a) aliweka wapelelezi ndani ya jeshi (military intelligence) ili apate habari zote. Hivyo idara hii nayo ilisaidia sana katika ulinzi na usalama wa Dola ya Kiislamu.
Hivi ndivyo Serikali ya Kiislamu ilivyoendeshwa kwa muda wa miaka 40 kuanzia kwa Mtume(s.a.w) hadi Makhalifa wake wanne na imekuwa ndio msingi wa uendeshaji wa Serikali zote za leo Duniani.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 407
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 kitabu cha Simulizi
👉3 Kitau cha Fiqh
👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉5 Simulizi za Hadithi Audio
👉6 Kitabu cha Afya
Khalifa ‘Umar bin Abdul Aziz
Soma Zaidi...
Vipengele vya mkataba wa Hudaibiya na faida zake katika Ukombozi (ufunguzi) wa mji wa Makkah
Soma Zaidi...
HISTORIA YA BANI ISRAIL
Nabii Musa na Harun walikuwa na kazi kubwa mbili; kwanza, kuwakomboa Bani Israil kutokana na dhuluma waliyokuwa wakifanyiwa na Firaun na Serikali yake, na pili, kuwarudisha kwenye nchi yao takatifu ya Palestina. Soma Zaidi...
HISTORIA NA SIRA YA UISLAMU NA MTUME MUHAMMAD KUTOKA KUZALIWA MPAKA KUFARIKI NA HARAKATI ZAKE
Soma Zaidi...
Ibrahiim(a.s) Aomba Kupata Kizazi Chema
Nabii Ibrahiim na mkewe Sarah walikaa mpaka wakawa wazee bila ya kupata mtoto. Soma Zaidi...
Yunus(a.s) Kulingania Uislamu kwa Watu Wake
Nabii Yunus(a. Soma Zaidi...
NINI MAANA YA SWALA (SALA AU KUSWALI), KILUGHA NA KISHERIA KATIKA UISLAMU
Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno Swalaat lina maana ya ombi au dua. Soma Zaidi...
Mafunzo ya sura zilizochaguliwa
Quran (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Vita vya Badr: Chanzo na sababu za vita vya Badr, Mafunzo ya Vita Vya Badr
Vita vya Badri. Soma Zaidi...
HISTORIA YA NABII ISA
Soma Zaidi...
Uteuzi wa Uthman bin Al-'Afan khalifa wa Tatu baada ya Mtume
Soma Zaidi...
tarekh 01
NASABA YA MTUME (S. Soma Zaidi...