Luqman ni katika watu wema kabisa waliopita zama za nyuma.
Luqman ni katika watu wema kabisa waliopita zama za nyuma. Ingawa zipo simulizi nyingi juu yake katika fasihi na tamaduni za Uarabuni; lakini hapana maelezo ya uhakika juu ya mahali alipoishi wala wakati. Qur’an na Hadith za Mtume(s.a.w) nazo hazigusii lolote juu ya kabila lake, wakati na mahali alimoishi. Hata hivyo muhimu si kujua haya. Ila ujumbe unaopatikana kutokana na mwenendo wake mzuri ndio jambo la msingi.
Luqman ni kigezo cha hikma. Anatubainishia kuwa maisha ya busara yenye kheri na mja ni yale yenye kujengwa juu ya msingi wa kumpwekesha na kumtii Muumba. Kumtambua na kumpwekesha Muumba ndio chimbuko la hikima ya kweli:
Na kwa yakini Tulimpa Luqman hikma tukamwambia: “Mshukuru Mwenyezi Mungu: na atakayeshukuru, kwa yakini anashukuru kwa ajili ya nafsi yake; na atakayekufuru, Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Asifiwaye” (31:12).
Ni jambo la lazima watu waelewe uhusiano wao na Mwenyezi Mungu na wamwabudu ipasavyo:
Na (wakumbushe) Luqman alipomwambia mwanawe; na hali ya kuwa anampa nasaha. Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu, maana kushirikisha ndio dhulma kubwa” (31:13).
Katika aya hii kupitia kwa Luqman akimnasihi mtoto wake; Mwenyezi Mungu anatutanabahisha tuepukane na shirki. Vipi uumbwe na Mwenyezi Mungu umwabudu mwingine!
Kumuabudu Mwenyezi Mungu kunaandamana vile vile na kufanya wema kwa wanadamu, wazazi wakishika nafasi ya kwanza. Lakini kinyume na utii kwa Allah(s.w); utii kwa wazazi una mipaka. Wazazi na watu wengine hutiiwa tu pale ambapo kutii huko hakumpelekei mtu kumuasi Mwenyezi Mungu:
“Na tumemuusia mwanadamu (kuwafanyia ihsani) wazazi wake mama yake ameichukua mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu; na (kumnyonyesha na kuja) kumwachisha kunyonya katika miaka miwili – ya kwamba unishukuru Mimi na Wazazi wako, marejeo yenu ni Kwangu” (31:14).
“Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na (yale) ambayo huna ilimu nayo, usiwatii; lakini kaa nao kwa wema hapa duniani; shika njia ya wale wanaoelekea Kwangu, kisha marejeo yenu ni Kwangu; hapo Nitakwambieni mliyokuwa mkiyatenda” (31:15).
Akiendelea kumnasihi mwanawe, Mzee Luqman alimsisitizia umuhimu wa swala, kuamrisha mema, kukataza mabaya na kufanya subira katika kuyafanya yote hayo. Aidha alimfahamisha juu ya Ujuzi wa Mwenyezi Mungu kwamba hapana jambo lolote linaloweza kufanyika bila kufahamika mbele ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo mwanadamu hawezi kumdanganya wala kumfanyia hila Mwenyezi Mungu.
Ewe mwanangu! “Kwa hakika jambo lolote lijapokuwa na uzito wa chembe ya hardali, likawa ndani ya jabali au mbinguni au au katika ardhi, Mwenyezi Mungu atalileta (amlipe aliyefanya); bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mambo yaliyofichikana (na) Mjuzi wa mambo yaliyo dhahiri” (31:16).
Ewe mwanangu! “Simamisha Sala, na uamrishe mema; na ukataze mabaya, na usubiri juu ya yale yatakayokusibu. Hakika hayo ni katika mambo yanayostahiki kuazimiwa (na kila mtu)” (18:17).
Mwisho Mzee Luqman anamuusia mwanawe asiwe na kibri, jeuri wala dharau. Bali awe mtu mpole na mwenye mwendo wa kati na kati:
“Wala usiwatazame (usiwafanyie watu jeuri) kwa upande mmoja wa uso, wala usende katika nchi kwa maringo, hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila ajivunae, ajifaharishaye” (31:18).
“Na ushike mwendo wa kati na kati, na uteremshe sauti yako, bila shaka sauti ya punda ni mbaya kuliko sauti zote” (31:19).
Kwa muhtasari Mzee Luqman amempa nasaha mwanawe juu ya mambo ya msingi yafuatayo:
1. Kumtambua Allah(s.w) na sifa zake na kumpwekesha ipasavyo.
2. Kushukuru neema za Allah kwa kumtii ipasavyo.
3. Kufanya jitihada za makusudi za kusimamisha Uislamu katika jamii na kudumu katika jitihada hizo.
4. Kujipamba na tabia njema.
Luqman amekuwa ni mfano kwetu juu ya malezi ya watoto. Mzazi pamoja na kuhangaika kumpatia mtoto chakula, malazi na nguo; lakini la msingi zaidi ni kumpa malezi mazuri. Malezi ambayo yatampelekea mtoto kumjua Muumba wake. Malezi ambayo yatamfanya mtoto aelewe na kukifanyia kazi cheo chake cha ukhalifa hapa duniani.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1138
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Simulizi za Hadithi Audio
👉3 Kitau cha Fiqh
👉4 Madrasa kiganjani
👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6 Kitabu cha Afya
Darsa za sira (maisha ya mtume jaribio la 01
Soma Zaidi...
Kuandaliwa Mtume (s.a.w) Kulingania Uislamu katika mji wa Makkah
7. Soma Zaidi...
Imam Tirmidh na Jami'u At-Tirmidh
Soma Zaidi...
Hitimisho juu ya Historia ya maimam wanne
Soma Zaidi...
Kupigwa vita Uislamu Tanganyika na Afrika Mashariki
Soma Zaidi...
HISTORIA YA NABII ISHAQA NA YAQUB
Soma Zaidi...
HISTORIA YA MTUME ILYASA(A.S)
Mtume Ilyasa ni mmoja wa Mitume waliotumwa kupitia kizazi cha Bani Israil. Soma Zaidi...
HISTORIA YA NABII IBRAHIIM(A.S) NA KUANDALIWA KWAKE:
Nabii Ibrahiim(a. Soma Zaidi...
Mchango wa Waislamu Katika Kuleta Uhuru Tanganyika
i. Soma Zaidi...
tarekh 5
KUZALIWA KWA MTUME (S. Soma Zaidi...
Mafunzo kutokana na vita vya badri
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
NINI MAANA YA SWALA (SALA AU KUSWALI), KILUGHA NA KISHERIA KATIKA UISLAMU
Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno Swalaat lina maana ya ombi au dua. Soma Zaidi...