Uchaguzi wa Omar (Umar) kuwa khalifa wa Pili baada ya Mtume

Uchaguzi wa ‘Umar bin Khattab kuwa Khalifa wa Pili.

Uchaguzi wa Omar (Umar) kuwa khalifa wa Pili baada ya Mtume

Uchaguzi wa ‘Umar bin Khattab kuwa Khalifa wa Pili.

Mtume(s.a.w.) kumchagua Abubakar kuwa Imam wa msikiti na kutoruhusu mtu mwingine kuswalisha na aliposwalisha mtu mwingine swala ilirudiwa ni dhahiri, kwa maoni yetu, Mtume(s.a.w.) aliashiria kuwa kiongozi awe Abubakar na akawaachia Waislamu waamue kumkubali au kumkataa. Tunaamini kuwa Abubakar alimuelewa hivi Mtume(s.a.w.) ndio maana alipokuwa anakaribia kutawafu aliwaita wajumbe wa Shura na kushauri kuwa yeye anampendekeza Umar awe ndiye Khalifa baada ya kifo chake. Wajumbe wa Shura walipokubali ndipo akamwambia Ali aandike usia huo. Abubakar alifanya hivi kwa jitihadi yake ambayo inakubalika katika Uislamu na hasa akizingatia hali ilivyokuwa mara Mtume alipofariki, Waislamu walipogawanyika makundi matatu yaani ukoo wa mtume, Muhajirin na Answari.

Hivyo alitumia njia hii ambayo ni ya Kiislamu, hakuiburuza Shura na kulikuwa na mjadala kabla ya kukubalika rai hiyo. Wajumbe maarufu wa Shura walikuwa ’Umar, Uthman, Ali,Talha, Abdul Rahman bin Auf, Muadh bin Jabal, Ubay bin Kaab, Zaid bin Thabit na wajumbe wengine mashuhuri kutoka Muhajirin na Ansar. Abubakar alitoa pendekezo lake la kumteua Umar kuwa Khalifa wa pili, wote walikubali ila walieleza wasi wasi wao juu ya ukali wa Umar, hii ndio hoja pekee iliyotolewa na Ali na Talha. Abubakar aliikataa hoja hii kwa kuwafahamisha kuwa Ukhalifa utamfanya asiwe mkali. Kwa kuwa hoja dhidi ya Umar ilikuwa hii tu basi pendekezo likakubalika.

Hatua iliyofuata ambayo imeimarisha uhuru wa kuchagua viongozi ni kuwahutubia waumini katika msikiti wa Mtume, akisaidiwa na jamaa zake, alisimama kwenye mimbari, kwanza alitaka ule usia usomwe mbele ya watu wote waliokuwa msikitini na yeye azungumze nao.9 Usia wenyewe ulikuwa kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahiim. Hili ni tamko linalofanywa na Abubakar bin Abi Qahafu ambaye yuko karibu ya kwenda akhera. Wakati wa kuwa katika hali ya kufa hata kafiri humuamini Mwenyezi Mungu, na hata mfanya madhambi hutubia (hurudi kwenye imani yake) na kafiri humtegemea Mwenyezi Mungu. Nimefanya kila jema kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kwa kuboresha dini yake na kwa manufaa ya Waislamu na kwa mimi mwenyewe katika kumteua Umar kuwa Khalifa. Nategemea atakuwa muaminifu na mtekelezaji haki lakini akibadilika na kuwa dhalimu mimi sina lawama kwa kuwa sina elimu ya ghaibu. Kila mmoja anawajibika kwa afanyayo.24


Baada ya usia huu kusomwa, Abubakar alipanda kwenye mimbari huku akisaidiwa na kuuhutubia umma kama ifuatavyo:-

Enyi ndugu zangu, sikumchagua kuwa Khalifa ukoo wangu au ndugu zangu. Nimemteua aliyebora miongoni mwenu mnakubaliana na uteuzi wangu? Wote waliitikia kwa kukubali.11



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1115

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Historia ya Watu wa Mahandaki ya Moto.

Katika Suratul Buruj, kumetajwa kisa cha makafiri waliowatesa wafuasi wa Mitume waliotangulia kabla ya Mtume Muhammad(s.

Soma Zaidi...
Msafara wa vita vya Tabuk Dhidi ya Warumi

Ukombozi wa mji wa Makka (Fat-h Makka) mwaka 8 A.

Soma Zaidi...
NINI MAANA YA SWALA (SALA AU KUSWALI), KILUGHA NA KISHERIA KATIKA UISLAMU

Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno Swalaat lina maana ya ombi au dua.

Soma Zaidi...
Historia ya Dhulqarnain

Dhulqarnain sio jina la mtu bali cheo, maana yake ikiwa: “Mwenye Pembe Mbili”.

Soma Zaidi...
Watu waliovunja amri ya kuheshimu siku ya Jumamosi.

Katika zama za kale Mayahudi walikatazwa kufanya kazi siku ya Jumamosi.

Soma Zaidi...