HISTORIA YA MTUME SULAIMAN(A.S)
Sulaiman(a.
HISTORIA YA MTUME SULAIMAN(A.S)
Sulaiman(a.s)alikuwa mtoto wa Nabii Daudi(a.s) na pamoja na kuwa Mtume alirithi pia kiti cha ufalme wa baba yake. Ufalme wake ulidumu kati ya mwaka 965 B.C. hadi 926 B.C. Ufalme wake ulienea Palestina ya leo, Transjordan na baadhi ya eneo la Syria. Qur'an inamtaja Sulaiman kuwa mrithi wa Nabii Daudi(a.s) katika aya zifuatazo:
"Na Sulaiman alimrithi Daudi na akasema: Enyi watu! Tumefundishwa (hata kutambua) usemi wa ndege na tumepewa kila kitu, hakika hii ni fadhila iliyo dhahiri" (27:16).
"Na tukampa Daudi (mtoto anayeitwa) Sulaiman, aliyekuwa mtu mwema, na alikuwa mnyenyekevu mno" (38:30).
Nabii Sulaiman(a.s) anatajwa katika historia kama mfalme ambaye haujapata kutokea uflame mkubwa kama wake. Mwenyezi Mungu alimpa uwezo hata wa kumiliki majini. Walimtumikia katika
kazi zake mbali mbali. Ufalme huu unatajwa kuwa Nabii Sulaiman(a.s)aliupata baada ya kumuomba Mola wake ampe ufalme ambao hataupata mwingine yoyote baada yake.
"Akasema: Mola wangu! Nisamehe na unipe ufalme, asiupate yoyote baada yangu. Bila shaka wewe ndiwe Mpaji" (38:35).
Dua hii Nabii Sulaiman(a.s) anaiomba akiwa tayari ni mfalme. Lakini baada ya hapo ndio ufalme wake ukapanuka, kama aya zinazofuatia aya zinavyobainisha:
"Basi tukamtiishia upepo unaokwenda pole pole kwa amri yake, anakotaka kufika. Pia na (Tukamtiishia) mashetani, kila ajengaye na azamiaye (lulu). Na wengine wafungwao minyororoni (wanapokhalifu amri zake)" (38:36-38).
Pamoja na ufalme na mamlaka makubwa kiasi hiki aliyopewa Sulaiman,lakini pia alipewa elimu ya kumtambua Allah(s.w) na kupewa utume. Kwa hiyo alikuwa ni mja mwenye shukrani kwa neema hizo alizofadhilishwa:
Na bila shaka tuliwapa Daudi na Sulaiman ilimu (kubwa kabisa na wakamshukuru Mwenyezi Mungu) wakasema: "Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Aliyetufadhilisha kuliko wengi katika waja wake waliomuamini" (27:15).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 ai web app 👉3 Madrasa kiganjani 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 Dua za Mitume na Manabii 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
MTUME MUHAMMAD (S.A.W) AANALELEWA NA BABU YAKE MZEE ABDUL-ALMUTALIB AKIWA NA UMRI WA MIAKA SITA (6)
KULELEWA NA BABU YAKE:Mzee ‘Abdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana.
Soma Zaidi...Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Ismail(a.s)
Kutokana na Historia ya Nabii Ismail(a.
Soma Zaidi...