image

Kuanzishwa kwa vitenge vya ulinza na Usalama, na usalama wa taifa

Kuanzishwa kwa vitenge vya ulinza na Usalama, na usalama wa taifa

Ulinzi na Usalama


Wakati wa Ukhalifa wa Makhalifa wanne ulinzi uliimarishwa kwa kiwango kikubwa. Wakati wa Mtume(s.a.w) hakukua na jeshi maalum. Kila mtu alikuwa askari na vita ilipofika Waislamu walijitokeza wakapewa mafunzo na kwenda vitani. Ni kweli pia kuwa katika Dola ya Kiislamu kila Muumin ni askari wa Allah(s.w) na wakati wowote anapotakiwa ni lazima awe tayari kupigania dini ya Mwenyezi Mungu.β€œEnyi mlioamini Je! Nikujulisheni biashara itayokuokoeni na adhabu iumizayo(61:10).


Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na piganieni dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu.......” (61:11)


Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waislamu nafsi zao na mali zao ili nae awape Pepo. Wanapigana katika njia ya Mwenyezi Mungu wanauwa na wanauwawa.............” (9:111)


Ni dhahiri Waislamu ni askari wa Mwenyezi Mungu. Pamoja na hivi tangu wakati wa Khalifa wa pili Umar, liliundwa jeshi kama yalivyo majeshi ya kileo. Khalifa ndie aliyekuwa mkuu wa majeshi, aliteua kamanda wa jeshi na makamanda wa mikoa na wilaya.


Idara ya ulinzi ilianzishwa na askari wote waliorodheshwa na utaratibu wa mshahara na posho ulianza kutumika kwa askari wa kudumu, wakujitolea na wale waliopigana vita vya awali kama Badr, Uhud, n.k.


Nchi iligawanywa kwenye maeneo ya kiulinzi, makao makuu ya maeneo haya yakawa Madina, Kufa, Basra, Mosul, Fustat, Damaskas, Hems, Jordan na Palestine. Katika sehemu zote hizi kambi zilijengwa kwa ajili ya askari. Mashamba ya mifugo yalipanuliwa kwa matumizi ya farasi na ngamia wa vita.


Pamoja na askari wa farasi na wa miguu jeshi la maji lilianza katika Ukhalifa wa Uthman. Vita vya kwanza vya majini vilipiganwa na Muawiya alipovamia Cyprus mnamo mwaka wa 28 A.H. Makao makuu ya Jeshi la maji yalikuwa Alexandria Misri.Usalama wa TaifaIdara ya usalama ilikuzwa. Ilianza tangu wakati wa Mtume(s.a.w) na kuendelezwa wakati wa Makhalifa wanne. Walitumika wanajeshi na wasio wanajeshi katika kazi ya kupata habari ndani na nje ya Dola na hasa kujua mwenendo wa adui. Wapo Machief, kwa mfano Syria, waliochaguliwa kuwa wanausalama, kuchunguza mwenendo wa Warumi. Palestine lilikuwepo kundi la Wayahudi lililojulikana kwa jina la Samara lilijizatiti katika upelelezi. Khalifa Umar(r.a) aliweka wapelelezi ndani ya jeshi (military intelligence) ili apate habari zote. Hivyo idara hii nayo ilisaidia sana katika ulinzi na usalama wa Dola ya Kiislamu.


Hivi ndivyo Serikali ya Kiislamu ilivyoendeshwa kwa muda wa miaka 40 kuanzia kwa Mtume(s.a.w) hadi Makhalifa wake wanne na imekuwa ndio msingi wa uendeshaji wa Serikali zote za leo Duniani.
                   
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 170


Download our Apps
πŸ‘‰1 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰2 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰3 Madrasa kiganjani     πŸ‘‰4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Mafunzo yatokanayo na upinzani wa maquraish dhidi ya uislamu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Nasaba ya Mtume Muhammad S.A.W na familia yake.
Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 1 Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Musa(a.s) na Harun(a.s)
Kutokana na Historia ya Nabii Musa na Harun(a. Soma Zaidi...

Mbinu za Da’wah Alizotumia Nuhu(a.s)
Katika kufikisha ujumbe huu kwa watu wake Nuhu(a. Soma Zaidi...

Mitihani aliyopewa Nabii Ibrahimu kutoka kwa Allah
Tumeona katika historia yake kuwa Nabii Ibrahiim(a. Soma Zaidi...

Kibri cha Ibilis na Uadui Wake Dhidi ya Binadamu
Ibilis ni katika jamii ya majini aliyekuwa pamoja na Malaika wakati amri ya kumsujudia Adam inatolewa. Soma Zaidi...

tarekh
MAPIGANO YA AL-FIJAR (MAPIGANO YA UOVU). Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Adam(a.s)
(i) Utukufu wa mtu katika Uislamu hautokani na nasaba, rangi,kabila,utajiri ila uwajibikaji kwa Allah(s. Soma Zaidi...

Je waislamu walishindwa vita vya Uhudi?
Katika vita vya Uhudi waislamu walikufa wengi kulinganisha na makafiri. Lakini makafiri walikimbia uwanja wa vita baada ya kuzidiwa. Je ni nanibalishindwa vita vya Uhudi kati ya waislamu na makafiri? Soma Zaidi...

Miujiza Kama Ushahidi wa Utume wa Nabii Musa(a.s)
Allah(s. Soma Zaidi...

Nabii Ibrahiim(a.s) Kuulingania Uislamu kwa Jamii Yake
Nabii Ibrahim(a. Soma Zaidi...

Yusufu Aokotwa na Kuuzwa nchini Misri
Huko nyuma wapita njia walikisogelea kisima kwa lengo la kuteka maji. Soma Zaidi...