image

Kisa cha Malkia wa Sabaa.

Sabaa ulikuwa mji katika nchi inayojulikana leo kama Yemen.

Kisa cha Malkia wa Sabaa.

Kisa cha Malkia wa Sabaa.


Sabaa ulikuwa mji katika nchi inayojulikana leo kama Yemen. Watafiti wa mambo ya historia na geografia wanasema Sabaa ilikuwa kiasi cha umbali wa maili hamsini kutoka mji wa Sanaa. Watu wa Sabaa walikuwa wakiabudu Jua na walimfanya mtawala wao kuwa ni mwanamke - malikia.



Pamoja na ushirikina wao, Allah(s.w) aliwaneemesha watu wa Sabaa kwa kila kitu walichohitajia katika maisha yao. Nabii Sulaiman aliwafahamu watu wa Sabaa kupitia kwa ndege Hud-Hudi kama aya zifuatazo zinavyobainisha:



"Na akawakagua ndege (na usimuone kidege Hud-Hud) akasema: "Imekuwaje mbona simuoni Hud-Hudi, au amekuwa miongoni mwa wasiokuwepo (hapa leo)". "Kwa yakini nitamuadhibu adhabu kali au nitamchinja au ataniletea hoja iliyo wazi (ya kumzuilia kuja hapa leo)." "Basi hakukaa sana mara (Hud-Hudi akafika) akasema (kumwambia Nabii Suleiman) Nemegundua usilogundua, na ninakujia hivi kutoka (nchi inayoitwa) Sabaa na (nakuletea) habari yenye yakini"."Hakika nimekuta mwanake anawatawalia; naye amepewa kila kitu na anacho kiti cha enzi kubwa"."Nimemkuta yeye na watu wake wanalisujudia jua badala ya Mwenyezi Mungu; na shetani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia njia (ya kheri), kwa hivyo hawakuongoka" (27:20-24).



Baada ya taarifa hizo Nabii Sulaiman alituma ujumbe kumnasihi malkia aingie katika Uislamu. Awali malkia baada ya kushauriana na mawaziri wake aliona apoteze lengo la Sulaiman kwa kumpa zawadi. Lakini lengo la Mitume ni kufikisha ujumbe wa Allah si kuchuma. Kwa hiyo Nabii Sulaiman alimrejeshea zawadi zake na akaendeleza harakati za kumvuta malkia katika haki mpaka akasilimu. Habari hizi zimebainishwa kwa urefu katika aya Qur’an(
27:27-44).



Jambo tunalotakiwa tulizingatie hapa ni ule msimamo thabiti wa Nabii Sulaiman katika kazi ya kuwalingania watu. Mara nyingi watawala hulewa tamaa ya kujilimbikizia madaraka na mali wakasahau wajibu wao mbele ya Muumba wao. Malkia wa Sabaa alidhani kwa kutumia mali angemtoa Nabii Sulaiman kwenye lengo lake. Lakini haikuwa hivyo.



Hali hiyo si kwa viongozi tu na wakuu wa nchi, bali hata sisi tulio katika harakati za Da'awah tuwe makini tusitolewe kwenye lengo kwa hongo ya mali au wadhifa.



                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 697


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Msimamo wa Nabii Nuhu(a.s) Dhidi ya Makafiri
Pamoja na upinzani mkali alioupata kutoka kwa viongozi wa makafiri, Nabii Nuhu(a. Soma Zaidi...

Hijra ya Mtume(s.a.w) Kwenda Madinah
Njama za Kumuua Mtume(s. Soma Zaidi...

Kulingania Uislamu kwa Jamii Nzima
Baada ya miaka mitatu ya Utume, Muhammad(s. Soma Zaidi...

Yusufu Aokotwa na Kuuzwa nchini Misri
Huko nyuma wapita njia walikisogelea kisima kwa lengo la kuteka maji. Soma Zaidi...

Maadui wa uislamu na mbinu zao: wanafiki, makafiri, mayahudi, wakristo,
Upinzani dhidi ya Dola ya Kiislamu Madinah. Soma Zaidi...

Mbinu za Mtume Salih(a.s) Katika Kulingania Uislamu
Kama Mitume waliotangulia, Nabii Salih(a. Soma Zaidi...

Sababu za makafiri wa kiqureish kuupinga ujumbe wa uislamu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Chanzo cha Mapato katika serekali ya Kiislamu wakati wa Makhalifa
Soma Zaidi...

Darsa za sira (maisha ya mtume jaribio la 01
Soma Zaidi...

Historia ya Watoto Wawili wa Nabii Adam
“Na wasomee khabari za watoto wawili wa Adam kwa kweli, walipotoa sadaka, ikakubaliwa ya mmoja wao na ya mwingine haikukubaliwa Akasema (yule asiyekubaliwa sadaka yake): “Nitakuua”. Soma Zaidi...

Yusufu(a.s) Atupwa afungwa Gerezani
Mkewe Al-Aziz hakumkatia tamaa Yusufu(a. Soma Zaidi...

Vipengele vya mkataba wa Hudaibiya na faida zake katika Ukombozi (ufunguzi) wa mji wa Makkah
Soma Zaidi...