Mbinu walizotumia Makafiri wa Kiqureish katika kuupinga Uislamu Makkah.
Mbinu walizotumia Makafiri wa Kiqureish katika kuupinga Uislamu Makkah.
- Maqureish wa Makkah walitumia kila mbinu kuhakikisha kuwa ujumbe wa Uislamu haufiki na kukubalika katika jamii yao, miongoni ni hizi zifuatazo;
a)Kumkatisha tamaa Mtume (s.a.w) na wafuasi wake.
        -  Makafiri walimdhihaki Mtume (s.a.w) na waumini wachache kwa
        kumuita majina mabaya kama; mwendawazimu, mtunga mashiri,
        aliyepagawa na mashetani, mchawi, n.k.
-  Pamoja na kusimangwa huko Mtume (s.a.w) na waislamu hawakukata
        tamaa, waliendelea kuutangaza Uislamu katika jamii yote.
b)Mbinu ya Vitisho na Kumkataza Mtume (s.a.w) kuulingania Uislamu kwa kumtumia Ami yake, Abu Talib.
-  Wakuu wa Maquraish walimuagiza Abu Talib amkataze Muhammad
        (mwanae) kuendelea kuutangaza Uislamu kwa kumbadilishia mtoto
        mwingine la sivyo watamshambulia yeye na Muhammad (s.a.w).
-  Mbinu hii haikufanikiwa badala yake Abu Talib alimuunga mkono
        Mtume (s.a.w) kwa kazi yake baada ya kujua msimamo wake.
c)Mbinu ya Kumhonga na kumrubuni Mtume (s.a.w).
        -  Maquraish walitumia diplomasia kwa kumtaka Mtume (s.a.w) aache
        kazi ya kuutangaza Uislamu kwa kumpa kati ya vitu vifuatavyo;
        utajiri, mwanamke mzuri, madaraka au yote kama akitaka.
-  Mtume (s.a.w) aliwakatalia vyote hivyo kwa kumsomea aya za Qur’an
        (41:1-37) mjumbe aliyetumwa kazi hiyo, Utbah bin Rabi’ah.
d)Mbinu ya kutaka kumlaghai Mtume (s.a.w).
        -  Maqureish walimletea Mtume (s.a.w) pendekezo kuwa washirikiane
        katika ibada kwa awamu, mwaka mmoja wamuabudu Mungu mmoja
        kwa pamoja na mwaka unaofuatia waabudu miungu yao pamoja pia.
-  Hapo ndipo iliposhuka suratul-Kafiruun kuvunja pendekezo lao hilo la
        kushiki katika ibada na Mtume akawasomea aya za Qur’an kukataa.
        Rejea Qur’an (109:1-6) na (10:15).
e)Mbinu ya Kuwatesa na kuwaua Waislamu.
        -  Baada ya Maqureish kuona mbinu zote zimefeli, walianza kutumia
        nguvu na mabavu kuwatesa, kuwanyonga na kuwaua Waislamu
        waliong’ang’ani imani yao kama akina; Bilal bin Rabbah, Sumaiyya,     
        Ammar bin Yasir na baba yake, n.k.
- Pamoja na mateso na mauaji, waislamu walibakia na msimamo wao 
        bila kutetereka na kukata tamaa.
f)Mbinu ya fitina, kuipinga Qur’an na kuzuia watu kukutana na Mtume (s.a.w).
        -  Maquraish kwa kuhofia ujumbe wa Qur’an kuenea kwa watu,
        walianza kuzuia watu kwenda kuonana na Mtume (s.a.w) kwa
        kuwashawishi kuwa wasisikilize aya za Qur’an kwani ni uchawi,
        mashairi ya Muhammad.
-  Walizidi kufitinisha kwa kumzuia Mtume (s.a.w) kuswali na
        kuwaambia watu kuwa Muhammad anapinga ibada na miungu wenu,
        lakini mbinu na ushawishi wao ulifeli pia.
        Rejea Qur’an (31:6), (41:26), (10:38), (11:13) na (96:9-19).
g)Mbinu ya kuwatenga na kila huduma ya kijamii.
        -  Maquraish walizidi kuongeza mateso kwa waislamu kwa kutenga na
        kuwafukuza Makka na kwenda kuishi katika jangwa la Shi’ab miaka
        mitatu bila chakula wala mahusiano mengine ya kijamii.
-  Mbinu pia ilifeli baada ya baadhi ya Maquiesh kuona huruma kwa
        ndugu zao waliotengwa bila sababu za msingi, hivyo wakavunja 
        mkataba wa kuwatenga.
h)Mbinu ya kutaka kumuua Mtume (s.a.w).
        -  Maquish waliazimia kumuua Mtume (s.a.w) na rafiki yake Abubakar
        (r.a) walipogundua kuwa waislamu wamehamia mji wa Madinah.
-  Mbinu hii pia ilifeli baada ya Allah (s.w) kuwanusu katika pango yeye
        na sahibu yake Abubakar (r.a).
        Rejea Qur’an (9:40).
        Mafunzo yatokanayo na Upinzani wa Maquraish dhidi ya Uislamu (Qur’an).
        i.Upinzani wa Makafiri dhidi ya ujumbe wa Uislamu upo nyakati na muda wote na hautaisha.
ii.Hatuna budi kuufikisha ujumbe wa Uislamu kwa kuanzia familia, ndugu na jamaa zetu wa karibu kabla ya wengine ili kupata wasaidizi wa karibu.
iii.Waislamu hawana budi kuwa tayari na kutokata tamaa katika kuusimamisha Uislamu bila ya kumchelea yeyote yule.
iv.Makafiri siku zote wako tayari kutumia kila mbinu na njia kuhakikisha kuwa wanabaki katika utawala na itikadi za ibada zao ili kuendeleza na kuimarisha maslahi yao kupitia unyonyaji na ukandamizaji.
v.Mbinu za Makafiri za kutaka kuuhilikisha Uislamu na waislamu zinafanana katika zama zote za historia ya maisha ya mwanaadamu.
vi.Mtume (s.a.w) na maswahaba wake waliweza kuhimili vitimbi vya makafiri na hatimaye kuweza kuusimamisha Uislamu katika jamii ni baada ya wao kufuata na kutekeleza kikamilifu mafunzo ya Qur’an (96:1-5), (73:1-10) na (74:1-7).
vii.Suala la kuulingania na kuutangaza ujumbe wa Uislamu ni zito, lenye misukosuko na gharama kubwa ya kutoa mali na nafsi (uhai).
viii.Siku zote makafiri na maadui wengine wa Uislamu hawakotayari kuona Uislamu unasimama katika jamii na waislamu wanautekeleza vilivyo.
ix.Tusitarajie matunda ya kusimama Uislamu kupatikana kwa muda mfupi na kwa urahisi, kwani linahitaji mipango ya muda mrefu na kujitoa muhanga.
x.Wakati wowote Waislamu watakapojizatiti katika kuulingania na kuupigania Uislamu kwa mali na nafsi zao, Allah (s.w) atawapa nusura dhidi ya maadui wao.
        Rejea Qur’an (61:8, 10-13).
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Jitihada alizozifanya Khalifa wa Tatu katika kuilinda Quran
Soma Zaidi...