Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Ismail(a.s)


Kutokana na Historia ya Nabii Ismail(a.r) tunajifunza yafuatayo:

(i) Kila Muislamu anatakiwa kumuomba Allah(s.w) amruzuku mtoto mwema atakayesaidia kupeleka mbele harakati za kuhuisha na kusimamisha Uislamu katika jamii.(ii) Mtoto mwema anayependwa na Allah(s.w) ni yule anayewatii wazazi wake katika mambo ya kheri.(iii) Mtoto mwema hujitahidi kushiriki katika harakati za kuusimamisha Uislamu katika jamii.(iv) Amri ya pili ya Allah(s.w) inayotukabili baada ya ile ya kusoma(kutafuta elimu) ni kusimamisha swala na kutoa katika vile Allah(s.w) alivyoturuzuku, kisha kuamrisha familia zetu na jamaa zetu wa karibu kufanya hivyo kisha tuilinganie jamii nzima kufanya hivyo.(v) Kusema kweli na kutekeleza ahadi ni katika tabia njema anayoiridhia Allah(s.w).(vi) Inatupasa kumuomba Allah(s.w) atupe yaliyo mema katika kila jambo tunalolikusudia kufanya.(vii) Kuwa tayari kutoa nafsi zetu kwa ajili ya Allah(s.w)kama alivyokuwa tayari Ismail(a.s) kuchinjwa na baba yake katika kutekeleza amri ya Allah(s.w)