Wapinzani wa Ujumbe wa Hud(a.s)


Waliomuamini Mtume Hud(a.s) walikuwa watu wachache na wengi walipinga ujumbe wake. Waliongozwa na Wakuu wa jamii.“Wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake, sisi tunakuona umo katika upumbavu na tunakuona u miongoni mwa waongo.” (7:66).Katika kuupinga ujumbe wa Mtume Hud (a.s), makafiri walitoa hoja zifuatazo:Kwanza,walidai kuwa hawako tayari kuacha kuabudu yale waliyokuwa wakiabudu wazee wao.
Wakasema: “Je! umetujia ili tumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na tuache waliyokuwa wakiabudu baba zetu? Basi tuletee unayotuahidi ikiwa ni miongoni mwa wasemao kweli.” (7:70).Pili,walidai kuwa Hud(a.s) alikuwa mzushi kama wazushi wengine waliotokea katika zama mbali mbali na hasa pale alipowaambia watu watafufuliwa baada ya kufa na kulipwa kwa yale waliyoyafanya hapa duniani.“Hayakuwa haya (ya kuja watu kusema kuwa wao ni Mitume) ila ni tabia ya watu wa (tangu) kale. Wala sisi hatutaadhibiwa (kama unavyodai na walivyodai hao).” (26:137-138)“Je anakuahidini ya kwamba mtakapokufa na mkawa udongo na mifupa, kuwa mtatolewa, (mtafufuliwa)?” Hayawi hayo mnayoahidiwa.(23:35-36).Hakuwa huyu (anayejiita Mtume) ila ni mtu anayemzulia Mwenyezi Mungu uwongo, wala sisi si wenye kumuamini. “(23:38)Tatu,walidai kuwa Hud (a.s) alikuwa mpumbavu au mjinga.

“Wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake, “Sisi tunakuona umo katika upumbavu na tunakuona u miongoni mwa waongo”. (7:66).Nne, walidai kuwa hakuwa Mtume kwa kuwa alikuwa mtu ana yekula na kunywa kama wao:
Na wakubwa katika watu wake waliokufuru na kukadhibisha makutano ya akhera, na tuliwatajirisha katika maisha ya dunia, walisema: “Hakuwa huyu ila ni mtu kama nyinyi, anakula katika vile mnavyokula na anakunywa katika vile mnavyokunywa.” (23:33)