Msimamo wa Nabii Hud(a.s) Dhidi ya Makafiri wa Kaumu Yake

Pamoja na kwamba alipingwa na nguvu za Dola ya makafiri wa kaumu yake, Mtume Hud(a.

Msimamo wa Nabii Hud(a.s) Dhidi ya Makafiri wa Kaumu Yake

Msimamo wa Nabii Hud(a.s) Dhidi ya Makafiri wa Kaumu Yake


Pamoja na kwamba alipingwa na nguvu za Dola ya makafiri wa kaumu yake, Mtume Hud(a.s), hakutetereka katika msimamo wake wa kutangaza Ufalme wa Allah(s.w) na kufikisha ujumbe wake. Hakutetereka kwa sababu alitegemea ulinzi wa yule aliyemtuma, mwenye uwezo juu ya kila kitu kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:



'..........Akasema (Hud) mimi namshuhudia Mwenyezi Mungu, nanyi shuhudieni ya kwamba mimi niko mbali na hao mnaowashirikisha (na Mwenyezi Mungu) mkaacha (kumuabudu)



yeye (pekee). Basi nyote nifanyieni hila (za kunidhuru) kisha msinipe muhula wowote'.(11:54-55).



Mimi nimemtegemea Mwenyezi Mungu, Mola wangu na Mola wenu. Hakuna kiumbe chochote isipokuwa (Mwenyezi Mungu) anamsanifu atakavyo. Bila shaka Mola wangu yuko juu ya njia iliyonyooka.(11:56)





Na kama mkirudi nyuma (hainidhurishi kitu); nimekwisha kukufikishieni niliyotumwa nayo kwenu; na Mola wangu atawafanya Makhalifa (wakazi wa mahala hapa) watu wengine wasiokuwa nyinyi wala nyinyi hamtaweza kumdhuru hata kidogo. Hakika Mola wangu ni mwenye kuhifadhi kila kitu.'. (11:57)



Ushindi wa Nabii Hud(a.s) Juu ya Makafiri


Makafiri walivyozidi kutakabari na kuzidisha fisadi katika ardhi ikiwa ni pamoja na kutaka kumdhuru Nabii Hud(a.s) na wale walioamini pamoja naye, Allah(s.w) alipitisha hukumu yake ya kuwahilikisha makafiri na kuwanusuru waumini kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:



Ilipofika amri yetu ya (kuangamizwa) tulimuokoa Hud pamoja na wale walioamini pamoja naye kwa rehema itokayo kwetu. Na tukawaokoa katika adhabu ngumu.(11:58)




Na hao ndio 'Ad. Walikanusha aya za Mola wao, na wakawaasi
Mitume yake na wakafuata amri ya kila jabari mkaidi.(11:59)



Na wakafuatishiwa laana katika dunia hii na siku ya kiyama. Sikilizeni hakika 'Ad walimkufuru Mola wao. Wakaangamizwa hao
'Ad kaumu ya Hud.' (11:60)

Jeshi la Allah(s.w) lililotumika dhidi ya makafiri katika jamii ya akina 'Ad ni upepo mkali uliovuma mfululizo kwa siku nane (mausiku Sabaa na michana minane) kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:



Basi walipoliona wingu likiyaelekea mabonde yao, walisema: 'Wingu hili la kutunyeshea mvua.' (Wakaambiwa) 'Bali haya ni ile mliyokuwa mkitaka ije kwa upesi, (adhabu ya Mwenyezi Mungu). Ni upepo ambao ndani yake iko adhabu iumizayo.' 'Unaoangamiza kila kitu kwa amri ya Mola wake.' Basi wakawa si wenye kuonekana tena ila nyumba zao tu (ndizo zilizosalia). Hivyo ndivyo tuwalipavyo watu waovu. (46:24-25)




Na bila shaka tuliwastawisha katika yale tusiyokustawisheni nyinyi, na tuliwapa masikio na macho na nyoyo; lakini masikio yao na macho yao na nyoyo zao hazikuwafaa chochote walipokuwa wakikanusha Aya za Mwenyezi Mungu, na yakawazunguka yale waliyoyafanyia mzaha. (46:26)




Na katika (habari za), Adi (ziko alama kadhalika). (Kumbusha) Tulipowapelekea upepo wa papazi uangamizao. Haukuacha chochote ulichokijia ila ulikifanya kama kamba mbovu. (51:41-42)




Walikadhibisha kina Adi (nao); basi ilikuwaje adhabu Yangu na maonyo Yangu! Hakika tuliwapelekea upepo mkali katika siku ya nuhsi iendeleayo (kwao mpaka leo). Ukiwang'oa watu (katika ardhi kisha unawabwata chini, wamelala, wamekufa) kana kwamba ni magogo ya mitende iliyong'olewa. Basi ilikuwaje adhabu Yangu na maonyo Yangu! (54:18-21).



Na majeshi ya mbingu na ardhi ni ya Mwenyezi Mungu; na
Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu; Mwenye hikima. (48:7)



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 138

Post zifazofanana:-

UPUNGUFU WA VYAKULA VYA MADINI
2. Soma Zaidi...

DUA ZENYE MANENO HAYA HUJIBIWA
SIFA ZA (MANENO NA MATAMSHI YA) DUA YENYE KUJIBIWA. Soma Zaidi...

Hifadhi ya Mwanamke na Maadili ya Jamii
(c) Hifadhi ya Mwanamke na Maadili ya JamiiKimaumbile wanaadam kama walivyo wanyama, wamejaaliwa kuwa na mvuto wa kimapenzi kati ya mume na mke ili kuwawezesha kutekeleza wajibu mkubwa wa kuzaana na kuendeleza kizazi. Soma Zaidi...

elimu yenye manufaa
Soma Zaidi...

KULINDA AKAUNT YAKO YA FACEBOOK DHIDI YA WAHALIFU WA KIMTANDAO
Watu wengi wanalalamika kuwa akaunti zao za facebook zimehakiwa, yaani zimeshambuliwa na wahalifu wa kimtandano. Soma Zaidi...

Mafundisho yao kutoathiriwa na mazingira ya jamii zao
Takriban Mitume wote walitokea katika jamii zilizozama katika ujahili, lakini kamwe ujumbe wao haukuathiriwa na mitazamo ya ujahili kwa ujumla, walahawakuingizautamaduni wa kijahili katika dini ya Allah (s. Soma Zaidi...

Je ulaji wa boga unafaa kwa mgonjwa wa kisukari?
Je ulaji wa boga unafaa kwa mgonjwa wa kisukari? Soma Zaidi...

Kitabu Cha Hadithi ya kifo cha Damu
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Bani Israil Kuabudu Ndama
Wakati Nabii Musa(a. Soma Zaidi...

NECTA FORM TWO CHEMISTRY PAST PAPERS
Soma Zaidi...

DUA BAADA YA TAHIYATU, NA KUTOA SALAMU KWENYE SWALA
13. Soma Zaidi...

ADABU ZA KUOMBA DUA
ADABU ZA KUOMBA DUA. Soma Zaidi...