Mchango wa Waislamu Katika Kuleta Uhuru Tanganyika
i.
Mchango wa Waislamu Katika Kuleta Uhuru Tanganyika
i. Harakati zote za kung’oa tawala na serikali za kikoloni Tanganyika ziliongozwa na kusimamiwa na Machifu na waislamu wakiwemo;
- Chifu Mkwawa wa Uhehe, Kalenga, Iringa na vita vya maji maji
- Chifu Isike wa Unyanyembe, Tabora, n.k
- Ali Songea Mbano na Suleman Mamba (Kinjekitile) wa Songea -.Ruvuma
ii. Waislamu ndio walioanzisha migomo kazini kupinga dhulma za serikali za kikoloni katika bandari za Tanga na Dar es Salaam miaka ya 1939 na 1947 mpaka vikaanzishwa vyama vya wafanya kazi ili kutetea haki zao.
iii. Kwa kutumia fursa ya vyama vya wafanyakazi, waislamu walianzisha jumuiya
(vyama viwili) ambavyo ni;
- Al-Jamia’tul Isilamiyya Fiy Tanganyika na
- Da’awat Al-Islamiyya
iv. Mwaka 1929, Tanganyika African Association (TAA) iliyopelekea kuundwa TANU mwaka 1954 kilianzishwa na viongozi wake walikuwa ni wale wale wa Jumuiya mbili za waislamu.
v. Sheikh Suleiman Takadir alikuwa mwenyekiti wa Baraza la wazee la TANU ambapo kabla ya Nyerere kukaribishwa na kuchukua uongozi wa chama ambapo ubaguzi wake ulidhiri dhidi ya Suleiman Takadir na waislamu wenzake.
vi. Mnamo mwaka 1957, waislamu walianzisha chama kingine cha siasa cha Kiislamu kiitwaco “All Muslim National Union of Tanganyika” (AMNUT) kwa lengo la kupigania haki kwa wote baada ya kupoteza imani na TANU.
vii. Kwa vile wakristo wengi ndio walionekana ndio wasomi, walihodhi nafasi nyeti za uongozi serikalini huku wakiwashadidia waislamu kutochanganya “dini na siasa” na kuhakikisha waislamu hawazidiki kamwe.
viii. Waislamu kupitia jumuiya ya East African Muslim Welfair Society (EAMWS) walianzimia kuanzisha chuo kikuu cha kwanza cha Kiislamu Afrika Mashariki baada ya kufanikiwa kumiliki idadi kadhaa ya shule za msingi na sekondari.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 ai web app 👉5 Bongolite - Game zone - Play free game 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Kibri cha Ibilis na Uadui Wake Dhidi ya Binadamu
Ibilis ni katika jamii ya majini aliyekuwa pamoja na Malaika wakati amri ya kumsujudia Adam inatolewa.
Soma Zaidi...Kuanzishwa kwa dola ya kiislamu madinah
Dola ya kiislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mafunzo kutokana na vita vya badri
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...CHANZO CHA VITA VYA VITA VYA AL-FIJAR NA ATHARI ZAKE
MAPIGANO YA AL-FIJAR (MAPIGANO YA UOVU).
Soma Zaidi...