Maandalizi ya hijrah ya mtume na waislamu kuhamia madinah

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

 

 

  1. Walipanga kuwa watajificha katika pango Thaur kwa siku tatu kabla ya kuanza safari ya kuelekea Yathrib (Madinah).

 

  1. Walipanga kutumia njia ya uficho isijulikana na mtu ya kuelekea kusini badala ya njia ya kawaida ya kuelekea kaskazini.

 

  1. Walimkodi bedui mweledi wa njia ile atakayewaongoza mpaka Yathrib kwa dinari 300.

 

  1. Abubakar (r.a) alinunua ngamia wawili kwa ajili ya safari yake na Mtume (s.a.w).

 

  1. Abubakar (r.a) alimchukua bint yake Asma kwa siri ili kumuonyesha pango lilipo na awe anawaletea chakula muda watakapo kuwa pangoni.

 

  1. Pia Abubakar (r.a) alimwagiza mchunga mbuzi wake awe anachungia karibu na pango ili awapatie maziwa.

 

  1. Abubakar (r.a) pia alimpa jukumu kijana wake Abdullah kuwaletea taarifa za mjini kwa yatakayojitokeza baada ya wao kuondoka. 

 

 

 

 

 

 

 

 


Baada ya kufariki (kutawafu) Mtume (s.a.w), Waislamu walikubaliana kuanzisha Kalenda ya mwaka wa Kiislamu ‘Al-Hijrah’ (A.H) ianzie siku ile aliyohama (hijra ya) Mtume (s.a.w) kwenda Madinah

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1499

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰2 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰3 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰4 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana: