Sifa au vigezo vya dini sahihi

Dini sahihi anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

  1. DINI SAHIHI ANAYOSTAHIKI KUFUATA MWANAADAMU.

Kulingana na umbile lake, mwanaadamu daima hutamani kuishi kwa furaha na amani ili kufikia lengo la kuumbwa, na hapo ndipo inambidi kuchagua dini (njia sahihi ya maisha) kati ya Uislamu, Ukafiri, Ushirikina au Utawa itakayomtimizia malengo yake. 

 

  1.  Sifa au Vigezo Vya dini sahihi

Dini sahihi ni ile inayomuwezesha mwanaadamu kuishi kwa furaha na amani ya kweli hapa Duniani na Akhera, na ni lazima iwe na sifa zifuatazo;

 

  1. Dini sahihi lazima ieleze ukweli juu ya maumbile;

Ni lazima ieleze ukweli juu ya mwanaadamu, lengo la kuumbwa kwake, hadhi/nafasi yake, dhima/kazi yake na maumbile yanayomzunguka na viumbe vyote vilivyo hai na visivyo hai, na hatima ya kila kitu.

 

  1. Dini sahihi ni lazima iwe na kanuni na sheria zinazoendana na maumbile yote;

Kanuni na sheria za dini sahihi ni lazima ziwe sambamba na kanuni za kimaumbile ili kuepusha mgongano wowote wa kimahitajio wa kimwili na kimazingira pia.

 

  1. Ni lazima itosheleze mahitajio ya mwanaadamu ya kimwili na kiroho;

Pia ni wajibu kwa dini sahihi kuelekeza na kutosheleza hisia za mwanaadamu pindi anapokuwa na hali ya furaha au hali ya majonzi, namna ya kukabiliana nazo ili kubakia katika lengo lake la kuumbwa (maisha).

 

  1. Dini sahihi pia lazima iwe ni mfumo wa maisha uliokamilika;

Dini sahihi haina budi kuwa na utaratibu kamili wa kila kipengele na Nyanja ya maisha ya kila siku kiuchumi, kisiasa, kiafya, kiutamaduni, kisheria, kielimu, n.k.

 

  1. Pia dini sahihi ni lazima iwe na ibada maalum zinazombakisha mwanaadamu katika maadili na hadhi yake;

Ni wajibu kwa dini sahihi kuwa na muongozo wa kumuinua na kumbakisha mwanaadamu katika mwenendo mzuri wa kiroho (kiutu) unaoweza kuustawisha mwili na kuleta mahusiano mazuri ya kiutu yasiyo na chuki, husuda, tamaa, kiburi, vurugu, n.k.

 

  1. Dini sahihi haina budi kuwa ya walimwengu wote na ya nyakati zote;

Ili kufikia lengo la kuumbwa mwanaadamu, dini sahihi ni lazima iwe inawahusu watu wa aina zote (wote), isiwe na jina la mtu au mahali na isiwe na mipaka ya kijiografia, rangi za watu, mahali, nyakati, n.k.

 

  1. Dini sahihi ni lazima iainishe na kusimamia haki zote za mwanaadamu;

Ni wajibu kwa dini sahihi kutoa na kusimamia haki, hukumu na adhabu kwa usawa na uadilifu kwa watu wote kibinafsi na kijamii bila upendeleo na ubaguzi wowote wa kirangi, taifa, nasaba, cheo au hadhi.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 3044

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

tarekh 07

KUPASULIWA KWA KIFUA MTUMEWAKATI AKIWA MTOTO.

Soma Zaidi...
Mtume Muhammad s.a. w amelewa na Baba yake mdogo

Historia na sura ya Mtume Muhammad, sehemu ya 10.

Soma Zaidi...
Maana ya Funga ya ramadhani kisheria na Aina za funga

Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga.

Soma Zaidi...
Allah(s.w) Amnusuru Ibrahim (a.s) na Hila za Makafiri

Pamoja na kudhihirikiwa na ukweli wa udhaifu wa miungu wa kisanamu, watu wa NabiiIbrahiim(a.

Soma Zaidi...
Mikataba ya aqabah

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
tarekh 4

KUANGAMIZWA KWA JESHI LA TEMBOTukio la pili ni lile tukio la tembo, na ilikuwa hivi:- Kiongozi mmoja wa kiyemeni aliyetambulika kwa jina la Abrah aliona waarabu kutoka maeneo mbalimbali wanafunga misafara kuelekea Makkah kwa lengo la kwenda kuhiji.

Soma Zaidi...