image

Uchaguzi wa Abubakari kuwa Khalifa wa kwanza baada ya kufariki Mtume Muhammad (s.a.w)

Uchaguzi wa Abubakari kuwa Khalifa wa kwanza baada ya kufariki Mtume Muhammad (s.a.w)

Utangulizi


Kifo cha Mtume(s.a.w) kiliacha pengo la kiongozi wa Dola ya Kiislamu. Muhammad(s.a.w) ni Mtume wa mwisho na hakuwa na naibu wake kama Haruna(a.s) alivyokuwa naibu wa Musa(a.s). Isitoshe, Mtume(s.a.w)hakuacha usia wowote wa nani awe kiongozi baada yake, sio kwa kauli wala maandishi. Hivyo ilibidi waislamu wazibe pengo la uongozi kwa kufuata utaratibu wa kuchagua viongozi wa Dola kwa kuzingatia mwongozo wa Qur’an na Sunnah. Kiongozi aliyechaguliwa kuchukua nafasi ya Mtume(s.a.w) aliitwa Khalifa wa Mtume yaani kiongozi anayeongoza kwa niaba ya Mtume(s.a.w). Katika Historia ya Uislamu makhalifa waongofu waliongoza Dola ya kiislamu nyayo kwa nyayo kama alivyofanya Mtume(s.a.w) ni wanne wafuatao:


(1) Abubakar bin Qahafu(r.a) - 11-13AH(632-634)



(2) Umar bin Khattab (r.a) - 14 - 24A.H(634 - 644 A.D)


(3) Uthman bin Affan (r.a) - 24 - 36 A.H (644 - 656 A.D)


(4) Ali bin Abu Twalib(r.a) - 36 - 41 A.H (656 - 661 A.D)



Uchaguzi wa Abubakar Kuwa Khalifa



Mara tu habari za kutawafu kwa Mtume(s.a.w) zilipoenea maswahaba waliokuwa wajumbe wa shura wakati wa uhai wa Mtume(s.a.w) walisahau wajibu wao wa kudhibiti pengo la uongozi lililojitokeza. Hali hii iliwapa nafasi Answar kukutana kwenye ukumbi wa “Thaqifah Bani Saidah” na kuanza kuzungumzia uongozi. ‘Umar na Abubakar walipopata taarifa hii nao walienda


kujiunga katika ukumbi huo. Wakati huo huo bani Hashim nao walikuwa wanakutana nyumbani kwa Fatma bint Muhammad kuzungumzia ukhalifa. Pale “Thaqifa Bani Saidah” mjadala mrefu ulipita, wapo waliotaka khalifa atoke upande wa Answar, wapo waliotaka khalifa atoke upande wa Muhajirina na wapo waliopendekeza kuwe na khalifa na naibu khalifa. Hatimaye walikubaliana kuwa pawe na khalifa mmoja ndipo Abubakar akampendekeza ‘Umar bin Khattab upande wa Muhajirina na Saad bin Ubaidah upande wa Answar. Wote kwa pamoja (‘Umar na Saad) wakasema hawana kifua cha kusimama katika jambo la ukhalifa badala ya Abubakar. Baada ya kauli hii ‘Umar alimpendekeza Abubakar na akampa mkono wa ahadi ya utii (Ba’iyah). Ndipo wote waliokuwepo kwenye ukumbi ule wakampa Abubakar mkono wa ahadi ya utii.


Siku ya pili jambo hili lilipelekwa msikitini kupata ridhaa ya Waislamu wote. Takriban watu thelathini na tatu elfu (33,000) walimkubali Abubakar awe khalifa na kumpa mkono wa ahadi ya utii. Lakini Ali bin Abutalib aliendelea na kikao cha ukoo wa bani Hashim na hakuwepo msikitini wakati Abubakar amepewa Ba’iyah na Waislamu 33,000 waliokuwemo. Ali alichukua miezi kabla ya kumpa khalifa Abubakar ahadi ya utii.


Abubakar alipewa ofisi ya ukhalifa kwa kufuata misingi ya Uislamu ya watu kumchagua kiongozi kwa kuzingatia sifa stahiki. Abubakar alistahiki kuchukua nafasi ya ukhalifa kwa sifa zifuatazo:


Kwanza, alikuwa na sifa zote za kiongozi wa Dola ya Kiislamu. Sifa hizi ni: Ucha-Mungu, ujuzi wa Qur-an na Sunnah, siha nzuri na tabia njema. Sifa zote hizi alikuwa nazo Abubaka(r.a)


Pili, Abubakar alikuwa karibu na Mtume(s.a.w) pengine kuliko swahaba yoyote. Hili linadhihirika zaidi katika msimamo wake wa kufuata hatua kwa hatua kila ambalo Mtume(s.a.w) amelifanya au kuliruhusu katika uhai wake alipokuwa akiendesha Dola ya


Kiislamu. Usahibu wa Mtume(s.a.w) na Abubakar umetajwa katika Qur-an kuhusiana na tukio la pangoni Thaur, wakati wa kuhajir Mtume:



Kama hamtamnusuru (Mtume), basi Mwenyezi Mungu alimnusuru walipomtoa wale waliokufuru; alipokuwa (mmoja tu na mwenziwe) wa pili wake, (peke yao); walipokuwa wote wawili katika pango; (Mtume) alipomwambia sahibu yake: “Usihuzunike, kwa yakini Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi.” Mwenyezi Mungu akamteremshia utulivu wake, na akamnusuru kwa majeshi msiyoyaona, na akafanya neno la wale waliokufuru kuwa chini; na neno la Mwenyezi Mungu ndilo la juu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayeshinda na ndiye Mwenye hikima. (9:40)


Tatu, Abubakar ndiye aliyeteuliwa na Mtume(s.a.w) kuongoza swala kwa niaba yake alipokuwa anaumwa karibu na kutawafu kwake. Katika siku hizo ambazo Abubakar aliteuliwa kuwa Imamu kwa niaba ya Mtume(s.a.w) ilitokezea siku moja akachelewa akaswalisha Imamu mwingine (aliswalisha ‘Umar bin Khattab). Mtume(s.a.w) aliposikia sauti isiyo ya Abubakar aliuliza juu ya Imamu (Abubakar) ambaye hakuwepo. Mtume hakupendezwa na akasema: “asiswalishe mtu mwingine ila Abu Qahafu (Abubakar). Baada ya hapo akaitwa Abubakar lakini wakati huo Imamu (‘Umar) alikwisha maliza swala. Mtume(s.a.w) aliamuru swala ile irudiwe nyuma ya Imamu Abubakar(r.a)


Nne, Abubakar alikuwa mtu mashuhuri anayekubalika, mtaratibu, mwenye istiqama na Ikhlas, mpevu wa uoni na mwenye uamuzi na alikuwa mfuasi wa Mtume(s.a.w) wa nyayo kwa nyayo.


Sifa zote hizi ukichanganya na umri wake, kwa wale waliokuwa kwenye ukumbi wa Thaqifa Bani Saidah hapana aliyemzidi kiumri, utaona kuwa Abubakar alistahiki kuwa Khalifa na hakuwa na upinzani kisifa.


Pia hutuba ya Abubakar aliyoitoa katika kupokea Ukhalifa nayo inaumuhimu wake katika kuonyesha wajibu wa kiongozi wa Dola ya Kiislamu, pale aliposema:


“Enyi watu mmenichagua niwe mdhamini wenu ingawa mimi sio bora kuliko wengi miongoni mwenu. Nikiwa sahihi nitiini. Nikipotoka nirekebisheni kwani ukweli ni uaminifu na uwongo ni kutoaminika. Aliyedhaifu atakuwa na nguvu mbele yangu mpaka nishindwe kumpatia haki zake Insha-Allah na mwenye nguvu mbele yangu atakuwa dhaifu mpaka alipe haki za wengine Insha- Allah. Allah huteremsha Nakama kwa watu walioacha Jihad katika njia yake. Vile vile Allah huteremsha maafa kwa watu ambao hufanya maovu”.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1415


Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

HISTORIA YA NABII AYYUUB(A.S)
Ayyuub(a. Soma Zaidi...

Njama za Mayahudi Kutaka Kumuua Nabii Isa(a.s)
Njama za kutaka kumuua Nabii Isa(a. Soma Zaidi...

Hija ya kuaga kwa mtume, na hutuba ya mwisho aliyotowa mtume katika hija
Mwaka mmoja baada ya msafara wa Tabuuk Bara Arab zima ilikuwa chini ya Dola ya Kiislamu. Soma Zaidi...

Kuibuka kwa kundi la khawarij baada ya vita vya Siffin
Soma Zaidi...

MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KULELEWA NA BABA YAKE MDOGO MTUME (ABU TALIB)
KULELEWA NA BABA YAKE MDOGOBaada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake. Soma Zaidi...

tarekh 5
KUZALIWA KWA MTUME (S. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII LUTI
Soma Zaidi...

Mafunzo yatokanayo na mkataba wa aqabah katika kuandaa ummah
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Khalid Ibn al walid katika vita vya Muta
Yiomyokea khalid Ibn al walid katika vita vya Muta Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII LUT(A.S) NA WATU WA SODOMA NA GOMORA
Mtume Lut(a. Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME YUNUS(A.S)
Nabii Yunus(a. Soma Zaidi...

Adam na Hawah Kushushwa Ardhini
Soma Zaidi...