Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Nuhu(a.s)


(i) Tuanze kulingania kwa Tawhiid – kumjua Allah(s.w)fika na kumuabudu ipasavyo.(ii) Tulinganie kwa kutumia hoja na mbinu mbalimbali kulingana na mazingira na wakati.(iii) Tutumie hoja kuonesha udhaifu wa hoja za makafiri dhidi ya Uislamu.(iv) Tusimchelee yeyote au chochote katika kulingania na kusimamisha Dini ya Allah(s.w).(v) Tulinganie Uislamu kwa kutaraji malipo kutoka kwa
Allah(s.w)pekee.(vi) Waumini hawana budi kushikamana pamoja katika kulingania na kusimamisha Uislamu katika jamii.(vii) Mlinganiaji awe na subira na kutowakatia tamaa wale anaowalingania – Nabii Nuhu(a.s) alilingania miaka 950 na kupata wafuasi wachache sana bila ya kukata tamaa.(viii) Mlinganiaji amuombe Allah(s.w) na kutegemea msaada kutoka kwake.(ix) Hatanusurika mtu muovu na adhabu ya Allah(s.w) kutokana na nasaba yake na Mitume wa Allah(s.w) na watu wema.(x) Hatima ya makafiri ni kuhiliki katika maisha ya dunia na akhera.
“Wala wale waliokufuru wasifikiri kwamba wao wamekwi shatangulia (mbele, Allah hawapati), la, wao hawatamshinda (Mwenyezi Mungu). (8:59).(xi) Hatima ya waumini wanaharakati ni kuwashinda maadui zao hapa ulimwenguni na kupata pepo huko akhera.(xii) Kushindwa na kuhiliki kwa makafiri wenye nguvu kubwa za kijeshi na kiuchumi na waumini wachache na dhaifu kijeshi nakiuchumi ni alama ya kuwepo Allah(s.w) aliyoahidi kuwatawalisha katika ardhi waumini wanaharakati.(Qur-an 24:55).(xiii) Siku zote wanaoongoza katika upinzani ni viongozi wa kikafiri(matwaghuti).(xiv) Hatuna mtu atakaye epukana na ghadhabu za Allah(s.w) na kupata pepo kwa amali njema alizofanya mtu mwingine hata akiwa na unasaba au urafiki wa karibu kiasi gani. Mtoto na mke wa Nuhu(a.s) waliangamia kutokana na matendo yao maovu.(xv) Hakuna mtu atakaye adhibiwa kwa maovu ya mwingine na huku akiwa ni muumini mtenda mema. Mkewe Firaun ni miongoni mwa wanawake wema waliotajwa katika Qur’an.