Baada tu ya Mtume(s.
Baada tu ya Mtume(s.a.w) na Waislamu kurejea Makka kutoka kule Shi’b Abu Talib, Abu Talib na Bibi Khadijah walifariki ikiwa ni mwaka wa 10 baada ya Utume sawa na mwaka 620 A.D. Umuhimu wa wawili hawa kwa Mtume na Waislamu unafahamika. Japo kuwa Abu-Talib hakusilimu, alijitoa muhanga kumlinda na kumhifadhi Mtume(s.a.w) kutokana na shari za Makafiri wa Makka. Mchango wa bibi Khadijah, mke wa kwanza wa Mtume(s.a.w), unafahamika. Tangu mwanzo wa Utume, bibi Khadijah alikuwa kiliwazo kikubwa cha Mtume(s.a.w). Alimfariji Mtume(s.a.w) kwa kila gumu lililomfika na alijitahidi kwa hali na mali kumsaidia Mtume(s.a.w) katika kazi yake. Kutokana na kipigo cha vifo hivi, Mtume(s.a.w) aliuita mwaka ule wa 10 B.U (620 A.D) “Ani al- Huzn” – mwaka wa huzuni.
Baada ya kufariki Abu-Talib na Bi Khadijah Maquraish walizidisha jeuri zao dhidi ya Mtume(s.a.w) na Waislamu kanakwamba wanamuambia Mtume(s.a.w), “Ni nani atakayekusaidia sasa”. Mtume(s.a.w) alipoona kuwa Makka imechafuka kiasi hicho, aliamua kwenda mji wa Taif kuwalingania Uislamu watu wa huko, Banu Thaqif na Banu Khawaizin, kabila la Bibi Halima, mama yake Mtume(s.a.w) wa kunyonya. Alitarajia kuwa kutokana na uhusiano wake na watu wa kabila hilo, watampokea vizuri atakapokwenda huko. Baada ya siku 10 kupita tangu afariki Bibi Khadijah, Mtume(s.a.w) alifunga safari ya kwenda Taif akiongozana na Zaid bin Harith. Alipowasili Taif aliwaendea wakuu wa mji ule na kuwafahamisha lengo la safari yake. Wakuu hawa walimpuuza na kumvunja sana moyo. Aliamua kuwaendea watu wa kawaida lakini nao pia walimpuuza. Hata hivyo, Mtume(s.a.w) hakukata tamaa, bali aliendelea kuwalingania Uislamu watu wa mji ule.
Walipoona Mtume(s.a.w) haondoki pamoja na kumkatisha tamaa kiasi hicho, wakuu wa mji ule walitoa amri kuwa watu wampige mawe popote watakapomuona mpaka aende zake. Watu walipopata amri ile, waliwaelekeza watoto na wahuni wa mji wampige Mtume(s.a.w) mawe mpaka aondoke. Bila ya huruma walimpopoa Mtume(s.a.w) mawe na kumsindikiza nayo kwa umbali wa maili mbili. Zaid alijitahidi sana kumkinga Mtume kwa mwili wake lakini haikusaidia kitu kwani wote walibubujikwa na damu mwili mzima kuanzia kichwani hadi miguuni.
Wale watoto na wahuni wa mji walipoacha kuwapiga na kurudi zao, Mtume(s.a.w) na Zaid walikaa kujipumzisha katika shamba la
‘Utbah bin Rabi’ah. ‘Utbah na ndugu yake walipomuona Mtume katika hali ile walimhurumia na wakamtuma mtumwa wao kuwaletea Mtume vishada vya zabibu na vyakula vingine. Yule mtumwa alimsaidia Mtume(s.a.w) juu ya safari yake na juu ya ujumbe wake. Yule mtumwa alisilimu baada ya kupata maelekezo yale kutoka kwa Mtume(s.a.w) na Bwana wake alijuta sana kwa nini alimtuma pale. Katika hali ile ya udhaifu, Mtume(s.a.w) alimuomba mola wake dua ifuatayo:
“Ya Allah! Kwako nashitakia udhaifu wa nguvu zangu na udhalilifu wangu katika macho ya watu. Ewe mwingi wa Rehema na Huruma kuliko wote wenye huruma! Wewe ndiye Bwana wa wanyonge na wewe ndiye Bwana wangu. Ni kwa watu gani umenipeleka? Kwa adui asiye na huruma anayenikunjia uso au kwa mgeni uliyempa uwezo juu ya jambo langu hili? Sijali lolote kunitokezea isipokuwa naomba ulinzi wako. Naomba hifadhi ya nuru ya uso wako – nuru iangazayo mbinguni na kuondosha aina zote za giza na nuru iongozayo na kudhibiti mambo yote ya hapa duniani na akhera. Naomba uninusuru na ghadhabu zako au kutokuwa radhi na mimi. Sina budi kuondosha Sababu ya wewe kutokuwa radhi na mimi ili hatimaye uwe radhi na mimi. Hapana nguvu wala uwezo ila kutoka kwako” (Sahihi – Muslim).
Mara baada ya dua yake alimjia Jibril (a.s) na baada ya kumpa salamu alisema:
“Allah anajua yote yaliyotokea kati yako na watu hawa. Anamtuma Malaika wa milima kuwa chini ya amri yako”.10
Mara tu baada ya Jibril(a.s) kumaliza ujumbe ule, Malaika muhusika alisimama mbele ya Mtume na kusema:
“Ee Mtume wa Allah, niko chini ya utumishi wako (niko tayari kukutumikia utakavyonituma). Kama unataka naweza kuvigonganisha vilima viwili vilivyoutazama mji huu na watu wote ndani yake wahiliki au unaweza kuamua adhabu yoyote unayotaka wapate.” 11
Mtume(s.a.w) aliye rehema kwa viumbe alijibu:
Hata kama watu hawa hawatakubali Uislamu, ninategemea kwa Allah kuwa watatokea watu katika kizazi hiki watakaomuabudu Allah na kupigania Dini yake”.12
T
ukio hili la Taif linatuonesha jinsi Mtume(s.a.w) alivyokuwa Rehema kwa viumbe na mvumilivu katika kazi yake. Pamoja na kufanyiwa ukatili mkubwa kiasi kile na watu wa mji wa Taif, bado hakuwalaani au kuwataka waangamizwe, bali bado alikuwa na tamaa kuwa watatokea watu wazuri katika kizazi chao watakaokuwa Waislamu na kuipigania Dini ya Allah(s.w) inavyostahiki.
Mafunzo Yatokanayo na Kufariki Bibi Khadija, Abu Twalib na Tukio la Taif
Kufariki kwa Bibi Khadija na Abu Twalib na tukio la Taif tunajifunza yafuatayo:
(i) Hatuna budi kutambua na kulipa fadhila angalau ya kihali (appreciation) kwa kila mtu aliyetoa mchango wa kuusukuma mbele Uislamu.
- Mtume(s.a.w) katika maisha yake yote hakusahau mchango wa Bibi Khadijah na pia hakusahau mchango wa ami yake katika kuuhami Uislamu pamoja na kwamba hakusilimu. Kwa kuwaenzi mwaka walio fariki akauita “Amul-al-Huzn”(mwaka wa huzuni)
(ii)Hatuna budi kutafuta fursa zitakazo pelekea kuulingania Uislamu kwa wepesi, Mtume(s.a.w) alienda Taif kutumia fursa ya udugu wa kunyonya. Mtume(s.a.w) alinyonyeshwa na Bibi Halima wa ukoo wa Saad kutoka mji wa Taif katika kabila la Bani Khawaizin.
(iii)Tuwe na subira na kumuelekee Allah(s.w) tunapokumbana na misukosuko katika mchakato wa kulingania na kusimamisha Uislamu katika jamii. Mtume(s.a.w). Pamoja na madhila yaliyomfika hakukata tamaa bali alimuelekea Mola wake na kuleta dua ile.
(iv)Tujiepushe na kuwalaani watu na kutaka waangamizwe kutokana na jeuri zao dhidi ya Uislamu, kwani asaa baada ya muda wanaweza, kwa rehema za Allah(s.w) kubadilika na kuufia Uislamu au kizazi chao kikaibukia kuupenda Uislamu na kuusimamisha katika jamii.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 816
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio
👉2 kitabu cha Simulizi
👉3 Madrasa kiganjani
👉4 Kitau cha Fiqh
👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6 Kitabu cha Afya
Maryam Apewa Habari ya Kumzaa Isa(a.s)
Baada ya maandalizi hayo ya kimalezi pamoja na hifadhi ya Allah(s. Soma Zaidi...
Ujumbe wa Nabii Ibrahiim(a.s) kwa Mfalme Namrudh
Soma Zaidi...
HISTORIA YA NABII MUSA NA HARUNA
Soma Zaidi...
Waliomuamini Nabii Nuhu(a.s)
Waliomuamini Nuhu(a. Soma Zaidi...
Tamko la suluhu baada ya vita vya Siffin
Soma Zaidi...
Mafunzo yatokanayo na kuanzishwa kwa dola ya uislamu madinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Njama za Kumuua Nabii Yusufu(a.s)
Kwa tabia zake njema Yusufu(a. Soma Zaidi...
Sababu za makafiri wa kiqureish kuupinga ujumbe wa uislamu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
HISTORIA YA MAISHA YA MTUME S.A.W KABLA YA UTUME
MAISHA YA MTUME (S. Soma Zaidi...
NAMNA MTUME(S.A.W) ALIVYOSIMAMISHA DOLA YA KIISLAMU MADINAH
Safari ya Mtume(s. Soma Zaidi...
tarekh 09
KULELEWA NA BABU YAKE:Mzee ‘Abdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana. Soma Zaidi...
HISTORIA YA MTUME ILYASA(A.S)
Mtume Ilyasa ni mmoja wa Mitume waliotumwa kupitia kizazi cha Bani Israil. Soma Zaidi...