Mafunzo Yatokanayo na mambo Aliyofanya Mtume (s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu
Kwanza, ili tuweze kusimamisha Uislamu katika jamii hatunabudi kuanzisha na kuendeleza vituo vya harakati, misikiti ikiwa ndio vitovu.
Mafunzo Yatokanayo na mambo Aliyofanya Mtume (s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu
Kwanza, ili tuweze kusimamisha Uislamu katika jamii hatunabudi kuanzisha na kuendeleza vituo vya harakati, misikiti ikiwa ndio vitovu. Kila palipo na fursa nzuri ni muhimu kuibadili misikiti iliyopo na kuifanya vituo vya harakati. Lakini ichukuliwe tahadhari kubwa ili tusije tumbukia kwenye kosa la kuvamia misikiti ya watu kabla ya kufikia kipindi cha kuikomboa β Fat-h-Makka.
Pili, hatunabudi kujenga mshikamano wa Waislamu kwa njia ya kupendana na kuhurumiana na hasa kwenye matatizo na shida. Rejea udugu baina ya Answar na Muhajiriina. Hatunabudi kujenga mazingira na tabia ya kufanya kazi za bega kwa bega (za kitamasha) katika kuendeleza shughuli mbali mbali kwa ajili ya maendeleo ya Uislamu.
Tatu, hatunabudi kukaa vizuri na wasiokuwa Waislamu hasa wale wasiotupiga vita bayana.Tuwaheshimu, tuwatendee haki na tusiwatukanie miungu yao wala kuidhihaki dini yao. Tuwalinganie kwa hekima na tuwape changamoto ya hoja na mawaidha mazuri.
Waite (waite watu) katika njia ya Mola wako kwa hikima na mauidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora (siyo kwa kuwatukana wao au kutukana Dini yao. Kwa njia hii huwezi kumvuta mtu). Hakika Mola wako ndiye anayemjua aliyepotea katika njia yake, naye ndiye anayewajua walioongoka. (16:125)
Nne, hatunabudi kuwajua vema maadui wa Uislamu na Waislamu na kuzijua vyema hila na mbinu zao katika kuuhujumu Uislamu. Kila Muislamu anatakiwa awe msalama kwa kumjua ni nani adui wa Uislamu, yuko wapi na anafanya nini dhidi ya Uislamu.
Tano, kila Muislamu mwanamume hanabudi kuwa mkakamavu na jasiri aliyetayari kuingia vitani ili kuihami Dini ya Allah(s.w).
Basi waandalieni (wawekeeni tayari) nguvu mziwezazo (silaha), na mafarasi yaliyofungwa tayari (mipakani), ili kwazo (nguvu hizi) muogopeshe maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, (mnaowajua) na pia (maadui zenu) wengine wasiokuwa wao, msiowajua nyinyi (lakini) Mwenyezi Mungu anawajua. Na chochote mtakachokitoa katika njia ya Mwenyezi Mungu (kama hii misaada ya vita vya Jihadi) mtarudishiwa kamili wala hamtadhulumiwa. (8:60)
Sita, ili tuweze kusimamisha Uislamu katika jamii yetu, hatuna budi kuimarisha uchumi wetu.Uchumi ndio raslimali kuu ya kusimamishia Uislamu katika jamii. Kila kitu cha kimaendeleo kinahitaji matumizi ya mali. Hatunabudi kuhuisha na kuimarisha ukusanyaji na ugawaji wa Zakat na Sadaqat kijamii.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) π2 Kitabu cha Afya π3 kitabu cha Simulizi π4 ai web app π5 Simulizi za Hadithi Audio π6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Watu wa Mji Waliomuua Muislamu kwa Kuwa Amewasadikisha Wajumbe wa Allah(s.w)
Katika Suratul Yassin Allah(s.
Soma Zaidi...Maana ya Funga ya ramadhani kisheria na Aina za funga
Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga.
Soma Zaidi...tarekh 09
KULELEWA NA BABU YAKE:Mzee βAbdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana.
Soma Zaidi...Jinsi tukio la Karatasi lilivyotokea wakati wa Mtume siku chache kabla ya kifo chake
Tukio la kartasiTukio la βkartasiβ lililonakiliwa katika vitabu vya Muslim na Bukhari kuwa siku tatu kabla ya kutawafu Mtume (s.
Soma Zaidi...Mafunzo yatokanayo na hijrah ya mtume na maswahaba wake
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...