Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
- Hii ilikuwa ni baina ya Mtume (s.a.w) na watu wanaotoka nje ya mji wa
Makkah hasa waliokuja kuhiji msimu wa Hija.
- Mtume (s.a.w) alikutana na kikosi cha kwanza kabisa cha watu sita (6)
kutoka Madinah (Yathrib) wa kabila la Khazraj, baada ya kuwafikishia
ujumbe wa Uislamu, walisilimu na wakaahidi kuufikisha kwao Madina.
- Mwaka uliofuata, 621 A.D, kikundi kingine cha waislamu 12 (2 Aus na
10 Khazraj) walikutana na Mtume (s.a.w) kwa siri eneo la ‘Jaratul
‘Aqabah’ na kuweka mkataba wa kwanza wa ‘Aqaba na kukubaliana
yafuatatayo;
- Mtume (s.a.w) aliwapa mwalimu wa kuwafundisha Uislamu, ‘Mus’ab bin
Umair.
- Mwaka uliofuata, 622 A.D.walimjia Mtume (s.a.w) waislamu 75
(wanawake 2) wakiongozwa na mwalimu wao, ‘Mus’ab na kufunga
Mkataba wa pili wa ‘Aqabah sehemu ile ile kwa kukubaliana kuwa;
- Mtume (s.a.w) aliwachagulia viongozi 12 (9 Khazraj na 3 Aus) na watu
watakaokuwa chini ya kila kiongozi, na wanaume wote walimpa Mtume
(s.a.w) mkono wa bai’at kwa maana ya utii wao kwake.
- Baada ya kikundi hicho kurejea na kufika Madinah salama, ndipo Mtume
(s.a.w) aliwatangazia waislamu wote wa Makkah kuhamia Madinah.
- Na takriban baada ya miezi miwili hivi, Waislamu wote wenye uwezo wa
kuhama walishahamia Yathrib (Madinah) kwenda kujiimarisha zaidi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mayahud Mwanzoni Mayahud walipoona kuwa Waislamu wanafunga siku ya Ashura pamoja nao na wanaelekea Qibla cha Baitul- Muqaddas pamoja nao hawakuonyesha chuki ya dhahiri dhidi ya Mtume(s.
Soma Zaidi...(i) Utukufu wa mtu katika Uislamu hautokani na nasaba, rangi,kabila,utajiri ila uwajibikaji kwa Allah(s.
Soma Zaidi...