image

Mapambano Dhidi ya Maadui wa Dola ya Kiislamu

1.

Mapambano Dhidi ya Maadui wa Dola ya Kiislamu

Mapambano Dhidi ya Maadui wa Dola ya Kiislamu
Katika miaka yote kumi ya kipindi cha Madinah,Mtume(s.a.w) alipambana mfululizo na maadui wa Dola ya Kiislamu. Mtume(s.a.w) mwenyewe akiwa Amir Jeshi na kamanda mkuu aliongoza vita 27, vikubwa 7 na vidogo 20 katika kipindi hicho cha miaka kumi. Maadui wakubwa waliopambana na Waislamu katika kipindi cha Madinah ni:1. Makafiri wa kabila la Kiquraish.
2.Wanafiki.
3.Mayahudi.
4.Makabila mengine ya Waarabu.
5.Warumi (wakristo).Makafiri wa Kabila la Qiquraish

Pamoja na vitimbi vyao vikubwa walivyovifanya Makka dhidi ya Mtume(s.a.w) na Waislamu, Makuraysh waliamua kuwafuatilia Waislamu Madinah kuendeleza vitimbi vyao kama vifuatavyo:Kwanza, walimuandikia barua kiongozi wa wanafiki, ‘Abdullah bin Ubayyi, ili amfukuze au kumuua Mtume(s.a.w) na kumtishia vita endapo hatatekeleza:

“Kwa kumpa mtu wetu(Muhammad) hifadhi (ya kiasiasa) tunakutaka kwa jina la Allah ima umuue au umfukuze Madinah lau sivyo, tutakushambulieni, tutakumalizeni na kuwateka wake zenu.”19Pili, Maquraish waliyatishia vita makabila yaliyokuwa yakiishi kati ya Makka na Madinah ili yasije silimu na kuyachochea yawe dhidi ya Waislamu.Tatu, Bwana mkubwa wa Maquraish, Kurz bin Jabir na wenzake walikuja kwa siri, Madinah, na kupora mifugo ya ngamia, mbuzi na kondoo na kukimbia nayo Makka.Nne, mabwana wakubwa wa Maquraish, Habbar bin ‘Aswad na Nafii bin Qays walimchocha chocha mikuki, bibi Zaynab bint Muhammad(s.a.w) alipokuwa akihamia Madinah kumfuata baba yake. Bibi huyu aliyekuwa mja mzito aliathirika sana na ikawa ndio Sababu ya kifo chake.

Hujuma kama hizi za Maquraish za kuhatarisha usalama wa Waislamu na uchumi wao zilikithiri na ikawa ndio Sababu ya Waislamu kuruhusiwa rasmi na Mola wao kuingia vitani dhidi ya maadui zao.Wameruhusiwa (kupigana) wale waliopigwa, kwa Sababu wamedhulumiwa.Na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia. (22:39)Na piganeni nao (makafiri) mpaka yasiweko mateso (nyinyi kuteswa na wao kwa ajili ya dini kama wanavyokuteseni sasa); na dini iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.Lakini wakiacha, basi hakika Mwenyezi Mungu anayaona wanayoyatenda. (8:39)Ruhusa hii iliwafanya Waislamu walijizatiti kivita kupambana na maadui zao hawa na wengine wote walioibuka baadaye.Mtume(s.a.w) na jeshi lake alipambana na Maquraish katika vita vikubwa vya Badr, Uhud na Ahzab. Waislamu walipata ushindi mkubwa katika vita vya Badr pamoja na udhaifu waliokuwa nao ukilinganisha na nguvu ya jeshi la Maquraish. Ushindi wa Badr ni bishara njema kwa Waislamu wa zama zote kuwa watapata ushindi dhidi ya maadui wa Dini ya Allah(s.w) pale watakapojizatiti kwa kadiri ya uwezo wao kupambana na maadui hao huku wakitegemea msaada kutoka kwa Allah(s.w).(Kumbukeni) mlipokuwa mkiomba msaada kwa Mola wenu, naye akakujibuni kuwa: “Kwa yakini Mimi nitakusaidieni kwa Malaika elfu moja watakaofuatana mfululizo (wanaongezeka tu)(8:9)
Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya ila iwe bishara (habari ya furaha) na ili nyoyo zenu zitue kwayo. Na hakuna msaada (wa kufaa) ila utokao kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu (na) Mwenye hikima. (8:10)
Na Mwenyezi Mungu alikunusuruni katika (vita vya) Badri, hali nyinyi mlikuwa dhaifu. Basi mcheni Mwenyezi Munguili mpate kushukuru (kila wakati kwa neema zinazokujieni).(3:123)

(Alikunusuruni katika vita vya badr) ulipowaambia Waislamu: “Je! Haitakutosheni Mola wenu atapokusaidieni kwa Malaika elfu tatu watakaoteremshwa?” (3:124)
Hamkuuwa nyinyi lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaua; na hukutupa wewe (Mtume ule mchanga wa katika gao la mkono wako), ulipotupa (ukawaingia wote machoni mwao); (hukufanya wewe haya) walakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyeutupa, (yaani ndiye aliyeufikisha katika macho yao wote yakawa yanawawasha kuliko pilipili, wakenda mbio) Alifanya haya Mwenyezi Mungu ili awape walioamini hidaya nzuri itokayo kwake. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye asikiaye na ajuaye. (8:17)Pamoja na udhaifu wa baadhi ya Waislamu walioonyesha kwa kuhalifu amri ya Mtume(s.a.w) katika vita vya Uhud bado Waislamu baada ya kurudi katika twaa ya Mtume(s.a.w) waliwashinda Maquraish na kuwarejesha Makka mbio mbio.Katika vita vya Ahzab, maquraish walikusanyana na makundi mengine ya maadui wa Uislamu ili kuunda nguvu kubwa itakayo wafuta Waislamu na Uislamu kwenye uso wa dunia. Waislamu walifanya jitihada kubwa ya kujihami kwa kuchimba handaki kubwa kuzunguka mji wa Madinah. Angalia ramani ya uwanja wa vita vya Handaq.Maadui kwa uwezo wa Allah walishindwa kulivuka lile handaki, wakabakia wakiwazingira Waislamu kwa takriban mwezi mmoja. Baadaye Allah(s.w) alileta majeshi yake ya mbinguni na ardhini kuwanusuru Waislamu. Allah(s.w) anatukumbusha:
Enyi mlioamini! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yenu; lilipokujieni jeshi; basi tukatuma upepo dhidi yao na majeshi msiyoyaona; na Mwenyezi Mungu amekuwa ni mwenye kuyaona mnayoyatenda. (33:9)
Hali ngumu ya Ahzab, iliwafanya Waislamu kuwa imara na wagumu zaidi kwa maadui zao:Na Waislamu (wa kweli) walipoyaona majeshi (ya makafiri yamewashambulia hivyo), walisema, “Haya ndiyo Aliyotuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (kuwa tutapata misukosuko, kisha tutashinda). Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wamesema kweli;” na (jambo hili) halikuwa zidishia ila imani na utii. (33:22)Hivyo Maquraish hawakuwa na uwezo tena wa kukabiliana na Waislamu na hatimaye wenyewe waliomba suluhu iliyopelekea kupatikana kwa mkataba wa amani wa Hudaybiya uliopelekea kuwashinda Maquraish na kupatikana “Fat-h Makkah”..                   

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 412


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

HISTORIA NA VISA VYA MITUME, MANABII NA WATU WEMA WALIOTAJWA KWENYE QURAN
Soma Zaidi...

tarekh 06
MAISHA YA UTOTONI YA MTUME S. Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME DAUD(A.S).
Nabii Daudi(a. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Lut (a.s)
(i) Tujitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuondoa maovu katika jamii kwa mikono yetu na ikiwa hatuwezi tuyakemee kama alivyofanya Nabii Lut(a. Soma Zaidi...

Sifa au vigezo vya dini sahihi
Dini sahihi anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

HISTORIA YA KUPASULIWA KWA KIFUA AU TUMBO CHA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) AKIWA MTOTO KWA BI HALIMA
KUPASULIWA KWA KIFUA MTUMEWAKATI AKIWA MTOTO. Soma Zaidi...

Mjadala juu ya ndoa ya Mtume Muhammad s.a.w na bi Khadija.
Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w sehemu ya 16. Hapa utajifunza maandalizi wa mjadala wa ndoa hizi. Soma Zaidi...

Watu waliovunja amri ya kuheshimu siku ya Jumamosi.
Katika zama za kale Mayahudi walikatazwa kufanya kazi siku ya Jumamosi. Soma Zaidi...

Maswali kuhusu Quran
Quran (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Bara arabu enzi za jahiliyyah, jiografia ya bara arabu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Njama za Mayahudi Kutaka Kumuua Nabii Isa(a.s)
Njama za kutaka kumuua Nabii Isa(a. Soma Zaidi...

Kuhajiri Waislamu wa Makka Kwenda Madinah
Baada ya mikataba miwili ya ‘Aqabah na baada ya Waislamu 75 kufika Yathrib salama, Mtume(s. Soma Zaidi...