Uchaguzi wa Ali bin Abu Twalib kuwa Khalifa wa nne na chanzo cha Makundi katika Uislamu

Uchaguzi wa Ali bin Abu Twalib kuwa Khalifa wa nne na chanzo cha Makundi katika Uislamu

Uchaguzi wa Ali bin Abu Twalib kuwa Khalifa wa nneMkondo wa historia ya Kiislamu juu ya utaratibu wa kuingia kwenye mamlaka umechukua sura mpya, pale alipouliwa Khalifa wa tatu na wapinzani, na kundi hili la wapinzani likamtaka Ali awe ndiye Khalifa wa nne. Kwa hali ilivyokuwa naye akakubali kuchukua nafasi hiyo. Jambo hili lilipelekwa msikitini na wapo waliokubali Ukhalifa wa Ali bila masharti, wapo waliokubali kwa sharti kuwa wahalifu waadhibiwe na wapo waliokataa kumpa mkono wa ahadi ya utii miongoni mwao ni Muhammad bin Muslimah, Usamah bin Zaid, Hassan bin Thabit, Ka'ab bin Malik, Abu Said Khudri, Numan bin Bashir, Zaid bin Thabit, Mughirah bin Shubah na Abdullah bin Salama.27 Wengine waliokataa ni ndugu na jamaa wa ukoo wa Uthman. Baadhi ya waliokataa Ukhalifa wa Ali walihamia Syria. Kwa ujumla uchaguzi wa Ali(r.a) uliwagawa waislamu kwenye makundi manne yafuatayo:(i) Wafuasi wa Uthman (Uthmanis), ambao walitaka dola iwaadhibu wauwaji. Watu wengi wa msimamo huu walikuwa wakazi wa Syria na Basra. Wasiria walimtaka Muawiyah ndiye awe Khalifa na sio Ali. Lakini Wabasra walitaka awe Talha au Zubeir.


(ii) Marafiki wa Ali (Shian-i-Ali). Watu hawa hawakumuona kuwa Uthman angefaa kuwa Khalifa. Hivyo wakajiita wenyewe Shia-i-Ali (marafiki wa Ali) watu wa mji wa Kufa (Wakufa/Kufans) na Wamisri ndio waliokuwa na msimamo huu. Inaaminika kuwa kundi hili ndilo lililomuua Uthman.


(iii) Mashibah: Watu hawa walikuwa kwenye Jihad wakati Uthman anauliwa. Hawakuwaunga mkono Uthmanis wala Shias.


(iv) Ahli-Sunnah wal Jamaah: Kundi hili lilikuwa lenye maswahaba wengi na lilienea Dola yote ya Kiislamu. Hawa wanasema tunawapenda wote Uthman na Ali. Wote ni Maswahaba waongofu. Kama kuna aliyefanya makosa ni kutokana na ijtihada, yake. Tunafuata Sunnah za Mtume na Sunna za Jamaa waongofu yaani kundi la Maswahaba.28


Utaratibu huu, ingawa kuna baadhi ya wanachuoni wanaoukubali lakini hauhitaji mjadala wowote, ni wazi kuwa hauna nafasi katika Uislamu. Kwa hakika watu wa Madina walikuwa na khofu na kundi hili la wauwaji hivyo kukubali kwao ule Ukhalifa wa Ali kwa mfumo ule yawezekana ni matokeo ya woga tu na siyo hiyari yao. Majibu ya Zubeir na Talha walipoulizwa na mjumbe wa Gavana wa Basra katika msafara wa Bibi Aisha kwa nini wanavunja Ahadi ya utii kwa Khalifa walisema. 'Ba'iyah ilifanywa mbele ya ncha ya upanga na ahadi ya kuwaadhibu wauwaji.29


Inawezekana pia hata kule kukubali kwa Ali kuwa Khalifa kunatokana na woga kwa sababu walipomtaka mara ya kwanza awe Khalifa kabla ya hao wauwaji kumuua Khalifa Uthman alikataa.30 Si hivyo tu lakini alipoona wanamsonga kutaka kumshirikisha katika mzozo wao alihama Madina na kwenda Ahjar sehemu maili chache kutoka Madina.31 Ingawa pia tukio hili linaonekana kumuweka Ali mahali pabaya.


Utaratibu wa kuingia katika uongozi wa dola ulizidi kuharibika alipouwawa Ali na mwanae mkubwa, Hassan akateuliwa kuwa Khalifa wa tano. Lakini Muawiyah alipopata habari hizi aliivamia Iraq. Hassan nae kwa upande wake alimteua Qays kuongoza majeshi ya kupigana na Muawiyah. Kulitokea uvumi kuwa Qays ameuwawa na hali hii ilipelekea majeshi ya Khalifa kumgeukia mwenyewe. Hassan alielewa hali ilivyokuwa mbaya hivyo alisalimu amri kwa Muawiyah, akaacha Ukhalifa kwa makubaliano kuwa atapofariki amuachie nduguye, Hussein ukhalifa. Baada ya makubaliano haya na Muawiyah, Hassan alirudi Madinah lakini aliuliwa kwa sumu aliyolishwa na mmoja wa wake zake kutokana na ushawishi wa Yazid.32 Huu ndio ulikuwa mwisho wa Hassan mjukuu wa Mtume.


Taratibu zote hizi ni za kupora madaraka kama alivyofanya Muawiyah ingawa alishinda kivita, kuwekeana makubaliano na watoto wa Ali, Hassan kuwa atamwaachia madaraka Hussein baada ya kufa kwake, na utaratibu wa kurithishwa, taratibu zote hizi, hazikubaliki katika Uislamu ingawa mfumo huu wa mwisho ndiyo uliyotumika katika utawala wa Banu Umaya, Banu Abbasi na Fatimiya.
                   
Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 233


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

NI IPI FAMILIA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) NA NI IPI NASABA YAKE, UKOO WAKE NA KABILA LAKE
FAMILIA YA MTUME (S. Soma Zaidi...

Mapambano ya Dola ya kiislamu dhidi ya maadui wa kikristo (warumi) wakati wa Mtume
Soma Zaidi...

KATU USITAMANI MAUTI (KIFO) YAANI KUFA, HATA UKIWA NA MARADHI AMA UKIWA MCHAMUNGU UKIWA NI MUOVU MTENDA MADHAMBI MAKUBWA NA MADOGO
Soma Zaidi...

KUKUSANYIKA KATIKA DUA
KUKUSANYIKA KATIKA DUA. Soma Zaidi...

Quran haikuchukuliwa kutoka kwenye biblia
Soma Zaidi...

MAFUNZO YA SWALA: NGUZO ZA SWALA, SHARTI ZA SWASL, FADHILA ZA SWALA, HUKUMU YA MWENYE KUACHA SWALA
Soma Zaidi...

Kuepuka mabishano na madhara ya kugombana
16. Soma Zaidi...

Vipengele vya Mikataba ya 'Aqabah na faida zake katika kuimarisha uislamu Maka na Madina
Katika Hija iliyofuatia katika mwaka wa 621 A. Soma Zaidi...

Aina za talaka, sharti zake na taratibu za kutaliki katika uislamu
Maana: ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa baina ya mume na mke mbele ya mashahidi wawili kwa kuzingatia sheria ya Kiislamu. Soma Zaidi...

fadhila za kusoma quran
Fadhila na umuhimu wa kusoma quran 1. Soma Zaidi...

Namna ya Kutayamam hatua kwa hatua, suna zake nguzo za kutayamam na masharti ya kutayamam
Soma Zaidi...

HISTORIA YA UANDISHI WA HADITHI
Historia fupi ya uandishi wa Hadith za Mtume (s. Soma Zaidi...