image

Uteuzi wa Uthman bin Al-'Afan khalifa wa Tatu baada ya Mtume

Uteuzi wa Uthman bin Al-'Afan khalifa wa Tatu baada ya Mtume

Uchaguzi wa Uthman bin Afan


Uchaguzi wa Uthman bin Affan Kuwa Khalifa wa Tatu Uislamu sio dini iliyofungwa katika mabano bali ina sifa ya kwenda na wakati kwa maana kuwa maamuzi yake ilimradi yamo katika mfumo wa Uislamu yanakubalika. Hali ilivyokuwa wakati alipotawafu Mtume(s.a.w) imetofautiana na ile ya wakati alipotawafu Abubakar. Wakati wa kifo cha Abubakar, Umar alikuwa amejitokeza kuwa ndiye Khalifa bila upinzani lakini wakati wa kifo cha Umar hali ilikuwa tofauti. Walikuwepo watu wengi wenye sifa zinazolingana hivyo alichokifanya Umar ni kuteua jopo la wagombea sita wa ukhalifa ambao walikuwa Uthman, Ali, Saad bin Waqqas, Talha, Zubair na Abdur-Rahman bin Auf.26 Agizo lingine alilotoa ni kuwa katika muda wa siku tatu baada ya kifo chake wawe wameshaamua wao wenyewe nani miongoni mwao awe
Khalifa.


Jopo hili lilikaa kwa muda mrefu bila kufikia uamuzi ndipo Abdur-Rahman bin Auf aliposhauri kuwa kati yao mmoja ajitoe ili aweze kutoa uamuzi. Alipokosa jibu alijitoa mwenyewe na akaanza kazi ya kutafuta maoni ili kukamilisha uteuzi. Talha hakuwepo hivyo wagombea walibaki wanne. Imetokea kuwa Ali alimpendekeza Uthman na Uthman alimpendekeza Ali. Zubair na Saad walimpendekeza Uthman. Baada ya kushauriana na Maswahaba wengine na kwa kuzingatia muda wa siku tatu Abdur-


Rahman bin Auf alitoa uamuzi asubuhi ya siku ya nne na kumtangaza Uthman kuwa ndiye Khalifa. Abdur-Rahman bin Auf (r.a.) alianza kumpa bai’at (mkono wa ahadi ya utii) na kutambua Ukhalifa wake ndipo Waislamu waliokuwa msikitini wakafuatia na kwa namna hii Uthman akawa Khalifa wa tatu. Talha aliporudi Madinah, Uthman alimshauri achague moja kati ya mawili, achukue nafasi ya Ukhalifa au ampe mkono wa ahadi ya utii. Talha alikubali kumpa mkono wa ahadi ya utii.


Utaratibu huu pia umo katika mkondo wa Uislamu na ni aina ya tatu ya utaratibu unaokubalika wa kupata viongozi katika Uislamu.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 338


Sponsored links
πŸ‘‰1 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     πŸ‘‰3 Madrasa kiganjani     πŸ‘‰4 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰5 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

HISTORIA YA NABII HUD(A.S) NA WATU WA 'AD
Baada ya Nuhu(a. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Sulaiman(a.s)
Kutokana na histoira ya Nabii Sulaiman (a. Soma Zaidi...

Kazi alizokuwa akizifanya Mtume Muhammad s.a.w kabla ya utume.
Historia na sifa ya Mtume Muhammad s.a.w , sehemu ya 14. Hapa utajifunza kuhusu kazi alizozifanya Mtume s.a.w Enzo za ujana wake kabla ya utume. Soma Zaidi...

Msimamo wa Nabii Hud(a.s) Dhidi ya Makafiri wa Kaumu Yake
Pamoja na kwamba alipingwa na nguvu za Dola ya makafiri wa kaumu yake, Mtume Hud(a. Soma Zaidi...

Hitimisho juu ya Historia ya maimam wanne
Soma Zaidi...

Mji wa Makkah na kabila la kiqureish
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Historia ya Watu wa Mahandaki ya Moto.
Katika Suratul Buruj, kumetajwa kisa cha makafiri waliowatesa wafuasi wa Mitume waliotangulia kabla ya Mtume Muhammad(s. Soma Zaidi...

MTUME MUHAMMAD (S.A.W)ANAKUTANA NA BAHIRA (MTAWA WA KIYAHUDI)
KUKUTANA NA BAHIRA (MTAWA) WA KIYAHUDIMzee Abu talib alikuwa ni mfanya biashara, hivyoslikuwa akimchukuwa kijana wake kwenda kwenye biashara. Soma Zaidi...

Mafunzo yatokanayo na upinzani wa maquraish dhidi ya uislamu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mtume alipoanza kulingania uislamu na changamoto alizokumbana nazo kutoka kwa maadua wa uislamu
7. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII SULEIMAN
Soma Zaidi...

Vipengele vya mkataba wa Hudaibiya na faida zake katika Ukombozi (ufunguzi) wa mji wa Makkah
Soma Zaidi...