Baada ya kupigwa kura juu ya nani awe mlezi wa Maryam, Nabii Zakaria akachaguliwa kuwa mlezi wa Maryam.
Baada ya kupigwa kura juu ya nani awe mlezi wa Maryam, Nabii Zakaria akachaguliwa kuwa mlezi wa Maryam. Allah(s.w) akaikubali ile nadhiri na dua ya mama yake Maryam.
Basi Mola wake akampokea (mtoto) kwa mapokezi mema na akamkuza kwa makuzi mema, na akamfanya Zakaria awe mlezi wake. Kila mara Zakaria alipoingia chumbani(kwa Maryam) alikuta vyakula pamoja naye. Akauliza: βEwe Maryam! Unapatawapi hivi? Akajibu: βHivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila kutarajia(3:37)
Aya hizi zinatuonesha kuwa Maryam alikuwa katika malezi mema na uangalizi wa karibu toka kwa Nabii Zakaria(a.s) kiasi cha kuepusha mazingira ya ufuska yasimfikie.Allah(s.w) aliweka maandalizi haya mapema ili atakapoleta muujiza wake kwa Maryam kuzaa mtoto bila ya kuwa na mume isionekane kuwa alikuwa mzinifu, bali iwe ni dalili ya kuwepo Allah(s.w) mwenye nguvu na uwezo wa kila kitu.
Kutokana na mazingira hayo na hifadhi ya Allah(s.w) Maryam akakua vyema na kupata hadhi ya kuwa mwanamke bora kuliko wanawake wote:
βNa (kumbuka) Malaika waliposema: βEwe Maryamu! Kwa hakika Mwenyezi Mungu amekuchagua na kukutakasa na kukutukuza kuliko wanawake wa ulimwengu (wote).(3:42)
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w sehemu ya 16. Hapa utajifunza maandalizi wa mjadala wa ndoa hizi.
Soma Zaidi...Katika Suratul Buruj, kumetajwa kisa cha makafiri waliowatesa wafuasi wa Mitume waliotangulia kabla ya Mtume Muhammad(s.
Soma Zaidi...Sura na historia ya Mtume Muhammad s.sa. w, sehemu ya 5. Hapa utajifunza kuhusu kuzaliwa kwa Mtume.
Soma Zaidi...Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Historia na shida ya Mtume Muhammad S.A.W, sehemu ya 12. Hapa utajifunza kuhusu kutokea kwa vita vya al fijar.
Soma Zaidi...Maandalizi ya Hijra ya Mtume (s.
Soma Zaidi...