Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Kama ilivyoamrishwa swala, funga, zakat na hijja, Neno “kutiba” (mmelazimishwa) limetumika katika jihad kama lilivyotumika katika kufunga, kulipa kisasi na faradh zingine pia za kutekeleza Uislamu.
Rejea Qur’an (2:216), (2:183), (2:178,180) na (22:78).
Kutekeleza faradh kama swala, funga, zaka na hija na ibada zingine za sunnah za binfsi, itakuwa sio sababu ya msingi ya kupata msamaha na pepo ya Mungu, mpaka jitihada ya dhati katika kupigania Uislamu katika jamii ifanyike.
Rejea Qur’an (4:74), (9:111), (61:10-13), (2:154), (3:169-171), (3:142), (3:157), (2:214) na (9:16).
Mitume wametumwa kusimamia haki na uadilifu katika jamii kwa kutumia miongozo ya vitabu vya Allah (s.w) na pia chuma (silaha) kimeteremshwa ili mitume na waumini wakitumie katika kusimamia haki na uadilifu ndani ya jamii.
Rejea Qur’an (57:25).
Mwenyezi Mungu (s.w) ametubainishia kuwa chochote tutakachokipenda au tutakachokifanya nje na lengo la kusimamisha Uislamu katika jamii hatakuwa na radhi juu yetu. Rejea Qur’an (9:23-24).
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Sira na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 17. Historia ya Bi Khadija na familia yake.
Soma Zaidi...KULELEWA NA BABA YAKE MDOGOBaada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake.
Soma Zaidi...“Kwa yakini katika (kisa cha) Yusufu na ndugu zake yako mazingatio mengi kwa wanaouliza (mambo wapate kujua)”.
Soma Zaidi...