HISTORIA YA MTUME ZAKARIA(A.S) NA YAHYA(A.S)
Zakaria(a.
HISTORIA YA MTUME ZAKARIA(A.S) NA YAHYA(A.S)
Nabii Zakaria(a.s) ni miongoni mwa mitume wa Bani Israil (Mayahud) na anatokana na kizazi cha Nabii Sulaiman(a.s). Alikuwa mwangalizi mkuu wa nyumba ya Ibada na alikuwa anapta riziki yake kwa kazi ya useremala.
Zakaria(a.s) Kumlea Marymam na Kuomba Mtoto Mwema Zakaria(a.s) alichaguliwa na ukoo kumlea Maryamu, mama yake Nabii Issa(a.s). Alimlea vyema katika malezi ya kiislamu.
Katika kumlea Marymu, Zakaria(a.s) siku moja alishangaa kumkuta Maryam binti Imraan na vyakula mezani ambavyo hakumpa yeye, ikabidi amuulize:-
“.........Ewe Maryam! unapta wapi hivi ? Akasema: Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu” (3:37)
Jibu hili la Maryamu lilimsisimua na kumuhamasisha Mzee Zakaria kiasi cha kumfanya naye amuelekee Mola wake na kumuomba mtoto mwema atakaye mrithi katika ucha-mungu na kusimamisha Dini ya Allah(s.w) katika jamii. Zakaria(a.s) alimuelekea Mola wake na kulalama.
Akasema: “Mola wagu. Bila shaka mifupa yangu imekuwa dhaifu na kichwa kinawaka (kinan’gara) kwa mvi,wala sikuwa mweye bahati mbaya (mwenye kukhasirika) Mola wangu, kwa kukuomba wewe. Na hakika mimi nawahofia jamaa zangu baada yangu(kuharibu Dini). Na mke wangu ni tasa. Basi nipe mrithi (anijie) kutoka kwako. Atakaye nirithi na kuwa na kuwarithi(wazee wake wengine)kizazi cha Ya‘aquub. Na umfanye, Mola wangu mwenye kukuridhisha”(19:4-6)
Yahya(a.s) Jibu la Dua ya Mzee Zakaria(a.s)
Dua ya Zakaria(a.s) ilijibiwa kwa kubashiriwa kupata mtoto, Yahya (Akaambiwa): “Ewe Zakaria! Tunakupa habari njema ya (kuwa utazaa)mtoto, jina lake ni Yahya: Hatujafanya kabla yake aliye na jina namna hilo.” (19:7)
Yahya(a.s) Kupewa Utume
Alizaliwa mtoto Yahya na kupewa utume akingali mtoto na akainukia kuwa mtu mwema kwa wazazi wake na kwa walimwengu wote kwa ujumla. Alijitoa muhanga kwa ajili ya kulingania Dini ya Allah(s.w).
“Ewe Yahya! kishike kitabu (hiki unachopewa) kwa hima kubwa.” Na tulimpa hikima angali mtoto. Na (tukamfanya ni) huruma kutoka kwetu, na utakaso na akawa mcha-Mungu. Na mwema kwa wazazi wake wala hakuwa jeuri ,asi. Na amani ilikuwa juu yake siku aliyozaliwa na siku aliyokufa na siku atakayofufuliwa hai.(19:12-15)
Nabii Zakaria na Yahya(a.s),wote waliuliwa na Mayahud.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 kitabu cha Simulizi 👉3 Simulizi za Hadithi Audio 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Maandalizi ya Kimafunzo aliyoandaliwa Mtume Muhammad
(i) Suratul- ‘Alaq (96:1-5)“Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba Aliyemuumba mwanaadamu kwa ‘alaq.
Soma Zaidi...Maana ya kusimamisha uislamu katika dini
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Hatua na Mambo (Taasisi za Kisiasa) za msingi alizotumia Mtume (s.a.w) katika kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah
Kuanzishwa kwa Dola ya Kiislamu Madinah.
Soma Zaidi...MTUME MUHAMMAD (S.A.W) AANALELEWA NA BABU YAKE MZEE ABDUL-ALMUTALIB AKIWA NA UMRI WA MIAKA SITA (6)
KULELEWA NA BABU YAKE:Mzee ‘Abdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana.
Soma Zaidi...