image

Mtume(s.a.w) Kulingania Uislamu Siku za Hija

Baada ya Mtume(s.

Mtume(s.a.w) Kulingania Uislamu Siku za Hija

Mtume(s.a.w) Kulingania Uislamu Siku za Hija

Baada ya Mtume(s.a.w) kupewa amri ya kuutangaza Uislamu kwa wazi, alitumia kila fursa aliyoipata katika kufikisha ujumbe wa Allah(s.w) kwa watu. Alianza na jamaa zake wa karibu, Maquraish, wakasilimu wachache na wengi wao wakawa maadui wakubwa dhidi yake na Uislamu. Pamoja na upinzani mkubwa uliokuwepo, Mtume(s.a.w) na Waislamu hawakukata tamaa bali walijaribu kutumia kila fursa iliyopatikana kuufikisha ujumbe wa Uislamu kwa kila ambaye haujamfikia na kuendelea kuwaasa wale uliowafikia lakini hawajaukubali. Katika kutumia fursa, Mtume(s.a.w) aliamua kutumia msimu wa Hija, kufikisha ujumbe wa Uislamu kwa watu wa mbali na Makka.Tukumbuke kuwa Ibada ya Hija, pamoja na kupotoshwa mafundisho yake, ilikuwa utamaduni wa Waarabu uliodumu tangu wakati wa Nabii Ibrahim(a.s) pale alipoamrishwa:
Na (tukamwambia:) “Utangaze kwa watu habari za Hija, watakujia, (wengine) kwa miguu na (wengine) juu ya kila mnyama aliyekonda (kwa machofu ya njiani) wakija kutoka katika kila njia ya mbali; (22:27)Hata hivyo, Maquraish hawakumuachia Mtume(s.a.w) kutumia fursa hii. Wakuu wa Maquraish walikutana “Dar-al- Nadwa” kuweka mikakati ya kuwazuia wageni (mahujaji) kukutana na Mtume(s.a.w). Waliamua kutuma wajumbe wasimame katika kila njia ya kuingilia Makka kuwatahadharisha wageni kuwa:“Mabwana wa Kiquraysh wametutuma kuwaambia kwamba huko Makka kuna mtu jina lake, Muhammad ambaye amezua Dini mpya ambayo wao hawaikiri kuwa ni Dini; na mtu huyo kapewa ufasaha wa kuzungumza usiokuwa na mfano. Humvuta mtu mara moja kwenye Dini yake kiasi cha kumsikiliza tu. Basi Maquraish wanakuhadharisheni na kumsogelea, licha ya kumsikiliza maneno yake. Akitaka kukusemezeni, mfukuzeni na zibeni masikio yenu. Lau kuwa hayo anayosema yangelikuwa kweli, wao wangelikuwa wa kwanza kumfuata, kwani wao wanamjua zaidi kuliko nyinyi.”14Kila mahujaji walipokuja Mtume(s.a.w) alichukua fursa ile na kuingia kila hema la kila kabila na kuwalingania Uislamu. Lakini hakupata mapokezi mazuri kutokana na ile ilani iliyotangulizwa na wajumbe wa Maquraish. Kila alipojaribu kuzungumza nao walimpuuza. Kila akisema humzomea, hujifunika nguo usoni na kuziba masikio yao ili wasimuone wala kumsikia ili wasije kutekwa na maneno yake yenye mvuto wa kichawi. Na anapofika mwisho wa mazungumzo yake humuambia:“Jamaa zako wanakujua zaidi, nao hawakukufuata. Basi hii ni alama kubwa ya kuwa wewe ni mwongo. Wala sisi hatutaacha Dini ya wazee wetu kwa Sababu yako? Abdul-Muttalib mbona hakuwaambia watu kuwa Dini hii (ya wazee) ni uwongo? Ingekuwa kweli Allah anataka kuleta Mtume, angelipewa Walid bin al-Mughira, Bwana wa Maquraish wote au angelipewa Urwa, Bwana wa Banu Thaqif wote. Unafikiri angelikuletea wewe yatima wa Abdul-Muttalib?”15Pamoja na mikakati hiyo ya makafiri wa Makka ya kuzuia watu wasiingie Dini ya Allah(s.w), palitokea watu ambao hawakutosheka na ile ilani ya Maquraish, bali waliamua kumsikiliza Mtume(s.a.w) na kujionea wenyewe ukweli wa mambo. Katika mwezi wa Rajab, mwaka wa 11 B.U. sawa na Oktoba 620 A.D walikuja kuhiji Makka watu sita (6) kutoka Yathrib (Madinah), katika kabila la Khazraj. Yathrib wakati huo ilikuwa ikikaliwa na Mayahud na makabila mawili ya Waarabu, Aus na Khazraj. Makabila ya Aus na Khazraj yalihasimiana na yalikuwa katika vita baina yao kwa muda mrefu. Kwa bahati nzuri Mtume(s.a.w) alipita Jamaratul-‘Aqabah, katika mji wa Minaa, akakutana na hao watu sita wa Yathrib. Baada ya Mtume(s.a.w) kuwafikishia ujumbe wa Uislamu na baada ya kuwajibu maswali yao waliyomuuliza, wale watu sita walisilimu wote na wakamuahidi Mtume(s.a.w) kuwa watajaribu wawezavyo kufikisha ujumbe wa Uislamu kwa wenzao wa Yathrib. Walitekeleza ahadi yao na watu wengi wa Yathrib walisilimu.

                              

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 195


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Historia ya Luqman mtu aliyesifika kuwa na Hikma
Luqman ni katika watu wema kabisa waliopita zama za nyuma. Soma Zaidi...

Vita vya Uhud na sababu ya kutokea kwake, Mafunzo ya Vita Vya Uhud
Vita vya Uhudi. Soma Zaidi...

Upinzani Dhidi ya Dola ya Kiislamu Wakati wa Makhalifa
Soma Zaidi...

Historia ya Dhulqarnain
Dhulqarnain sio jina la mtu bali cheo, maana yake ikiwa: “Mwenye Pembe Mbili”. Soma Zaidi...

Historia ya kujengwa kwa Alkabah (Maka)
Kama tulivyoona katika maisha ya Mtume Ibrahim(a. Soma Zaidi...

Historia ya Kuzuka Imani ya Kishia waliodai kuwa ni wafuasi wa Ally
Soma Zaidi...

Maana ya Funga ya ramadhani kisheria na Aina za funga
Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga. Soma Zaidi...

Mtume Muhammad s.a. w akutana na Bahira
Sura na historia ya Mtume Muhammad s.a. w sehemu ya 11 Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII DAUD
Soma Zaidi...

Mawazo Tofauti Kuhusiana na Uchaguzi wa Abubakar
Soma Zaidi...

Mfumo wa ulinzi na usalama katika fola ya uislamu madinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Daud(a.s)
Kutokana historia ya Nabii Daud (a. Soma Zaidi...