Dola ya kiislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
- Msikiti ulikuwa ndio Ikulu, mahakama, kituocha jeshi, ukumbi wa bunge (shura), n.k. Qur’an (3:95), (2:150).
- Ulikuwa kituo muhimu cha kiharakati katika kusimamisha na kuendeleza Uislamu. Rejea Qur’an (22:40), (2:114), (72:18) na (9:19).
- Mtume (s.a.w) aliwapatanisha kabila la Aus na Khazraj Madinah waliokuwa na uadui wa muda mrefu baina yao. Qur’an (3:103).
- Mtume (s.a.w) pia aliwaunganisha udugu imara kati ya Muhajirina wa
- Makkah na Answaar wa Madinah na kuwa ummah mmoja. Qur’an (8:75).
- Pia aliimarisha uchumi kwa kuunganisha ummah wa Kiislamu na kuwa kitu kimoja. Qur’an (59:8-9).
- Mtume (s.a.w) alijieleza katika mkataba huo kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na ndiye kiongozi mkuu wa Dola ya Kiislamu.
- Mkataba uliainisha vipengele vya amani na wajibu wa kila kundi kati ya makabila ya Mayahudi na Waarabu washirikina wa Madinah na Dola ya Kiislamu Madinah.
- Uliainisha nafasi, majukumu na wajibu wa waumini katika Dola.
- Mkataba uliainisha uhuru wa kila mtu kuabudu kwa mujibu wa imani na dini zao.
- Makabila na koo tatu za Kiyahudi zenye nguvu zilizokuwa pembezoni mwa mji wa Madinah yalikuwa;
- Mtume (s.a.w) aliteua washauri wake wakuu katika kuendesha Dola ambao Walikuwa Abu Bakr (r.a), Umar bin Khattab (r.a), Uthman bin Affan (r.a), Ally bin Abu Twalib (r.a) na Hamza bin Abdul-Muttalib (r.a).
- Aliteua waandishi maalumu wa kuandika na kutunza mikataba, takwimu, kumbukumbu na nyaraka zote za Dola ya Kiislamu Madinah.
- Mtume (s.a.w) aliwaanda na kuwahimiza waislamu kuwa wakakamavu na hodari katika shabaha, mieleka na kutumia silaha.
- Kila Muislam alikuwa mpiganaji na mpelelezi dhidi ya maadui wa waislamu na Dola ya Kiislamu. Rejea Qur’an (4:71).
- Aliunda na kuweka vikosi vya doria na ulinzi kuzunguka mipaka ya Dola ya Kiislamu Madinah. Qur’an (8:26).
- Mtume (s.a.w) aliwahimiza waislam kufanya kazi kwa bidii ili kujiimarisha Kiuchumi na kuendeleza Dola.
- Utoaji wa Zaka, Sadaka na mapato mengine yalihimizwa na kukusanywa Kijamii na kuboresha huduma za jamii.
Rejea Qur’an (22:41).
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Makafiri wa Kithamud hawakuishia tu kwenye kuukataa ujumbe wa Nabii Salih(a.
Soma Zaidi...(i) Suratul- βAlaq (96:1-5)βSoma kwa jina la Mola wako aliyeumba Aliyemuumba mwanaadamu kwa βalaq.
Soma Zaidi...Sura na historia ya Mtume Muhammad s.a. w sehemu ya 11
Soma Zaidi...