MTUME(S.A.W) KULINGANIA UISLAMU MAKKA

Historia ya harakati za Mtume(s.

MTUME(S.A.W) KULINGANIA UISLAMU MAKKA

MTUME(S.A.W) KULINGANIA UISLAMU MAKKA

Historia ya harakati za Mtume(s.a.w) za kuhuisha na kusimamisha Uislamu katika jamii yake zimegawanyika katika vipindi viwili – kipindi cha Makka na kipindi cha Madinah. Kipindi cha Makka kilichukua muda wa miaka kumi na tatu(13) kuanzia pale Mtume(s.a.w) alipoanza kupokea wahayi wa kwanza wa Qur’an mpaka alipoondoka kuhamia Madinah. Kipindi cha Madinah kilianza pale alipopokelewa Madinah na Answar mpaka mwisho wa uhai wake. Kipindi hiki kilichukua muda wa miaka kumi (10).



Mazingira ya Makka na Madinah yalikuwa tofauti. Hivyo hata mbinu za kuhuisha na kusimamisha Uislamu zilitofautiana. Pia hata mbinu za wapinzani wa Uislamu zilitofautiana.

Kuanza Kulingania kwa Siri

Baada ya Mtume(s.a.w) kupewa amri ya “simama uonye (watu)” aliamua kuanza kulingania kwa siri. Bila ya kutangaza hadharani kuwa yeye sasa ni Mtume wa Allah(s.w), alianza kumuendea mtu mmoja mmoja katika wale waliokuwa karibu naye kifamilia na kirafiki. Mtume(s.a.w) alianza kuutangaza Utume wake



kwa mkewe Khadija na watoto kisha kwa wale waliokuwa chini ya ulezi wake, ndugu yake, Ally bin Abu-Talib na huru wake, Zaid bin Harith. Baada ya hapo Mtume(s.a.w) aliwaendea rafiki na jamaa zake wa karibu na kuwafikishia ujumbe wa Utume. Miongoni mwa rafiki zake waliokuwa karibu ni Abubakar(r.a). Rafiki zake nao waliufikisha ujumbe wa Uislamu kwa familia zao na rafiki zao wa karibu kiasi kwamba ujumbe ulitambaa chini kwa chini mpaka ukaingia takriban katika kila nyumba ya wakazi wa Makka.



Katika kipindi hiki cha kufikisha ujumbe kwa siri, kilicho dumu kwa miaka mitatu, Mtume(s.a.w) alikuwa akikutana na Waislamu kwa siri katika nyumba ya Bwana Arqam bin Abi Arqam iliyojulikana kwa jina maarufu, “Darul-Arqam”.



Mtume(s.a.w) alikuwa anakutana na waumini Darul-Arqam ili kuwafundisha Uislamu na kuwapa waumini maelekezo ya namna ya kuutekeleza katika maisha ya kibinafsi na ya kijamii. Alikuwa akiwasomea aya za Qur-an alizokuwa anashushiwa kila mara na kuwaelekeza namna ya kuzitekeleza katika maisha yao ya kila siku. Kila Muislamu wakati ule aliujua Uislamu na kuutekeleza vilivyo katika maisha yake ya kila siku. Kwa mujibu wa Hadith, iliyo simuliwa na Ibn Masu’ud(r.a), kila Muislamu aliisoma Qur-an kwa lengo la kuifanya mwongozo wa maisha yake ya kila siku.



Wengi waliosilimu katika kipindi hiki cha awali walikuwa watumwa, maskini, vijana na wale wasiokuwa maarufu katika jamii. Kilichowafanya hawa watu wa mwanzo kusilimu haraka haraka bila ya kusita, ni ule ukaribu wao na Muhammad(s.a.w) ambao uliwawezesha kuifahamu vyema tabia yake tukufu. Walimfahamu kuwa alikuwa mwaminifu mno na hawakuwahi kamwe kumsikia akisema uwongo. Kwa ukweli wake na uaminifu uliopea, walimuita “As-Sadiq Al-Amin” (Mkweli Mwaminifu) hata kabla ya kutangaza ujumbe wa Uislamu. Pia, hata kabla ya kuanza kutangaza ujumbe wa Utume wake, alikuwa mpole na mwenye kuwahurumia mno wanyonge hasa watumwa na maskini. Hivyo, alipowatangazia hao rafiki zake na jamaa zake wa karibu kuwa yeye ni Mtume wa Allah, wote waliitikia wito wake wakasilimu isipokuwa wale waliokuwa na matatizo yao ya ubinafsi kama ami yake, Abu-Lahab.


Mafunzo:

Kutokana na Mtume(s.a.w) kuanza kulingania ujumbe wa Uislamu kwa siri, tunajifunza yafuatayo:

Kwanza, baada ya kuukiri Uislamu na kuutekeleza kimatendo, hatunabudi kuufikisha Uislamu huo kwa familia zetu, rafiki na jamaa zetu wa karibu. Hawa watakuwa wepesi kutusikiliza na kutufuata kwa kuwa wanatufahamu vyema. Tabia njema ni nyenzo muhimu sana.



Pili, ni muhimu kuwa wasiri na waangalifu katika hatua za mwanzo mwanzo za kuuhuisha Uislamu katika jamii ili maadui zetu wasije kutuzima kabla ujumbe haujasambaa kwa watu wengi. Baada ya miaka mitatu ya Mtume(s.a.w) kutangaza ujumbe kwa siri, takriban katika kila familia ya wakazi wa Makka palikuwa na mtu aliyesilimu.Jambo hili liliwaudhi na kuwahuzunisha sana wakuu wa jamii ya Kiquraish.



Tatu, kuujua Uislamu vilivyo kwa kila Muislamu ni jambo muhimu sana. Hata katika kipindi hiki cha kutangaza ujumbe kwa siri, Mtume(s.a.w) hakuacha kuwakusanya Waislamu kisiri siri katika kituo cha Darul-Arqam kuwafundisha Uislamu na kuwapa maelekezo ya utekelezaji wake katika maisha ya kila siku. Uislamu hautoweza kusimama katika jamii iwapo wanaojiita Waislamu watakuwa wameridhika kuishi kwa kufuata upepo kama bendera. Waislamu wa kufuata mkumbo (norminal Muslims) mara nyingi hutumiwa na maadui na kuupiga vita Uislamu na Waislamu bila kujitambua. Aidha, Waislamu wa mkumbo mara nyingi huwa rahisi kukumbwa na propoganda za maadui wa Uislamu. Vile vile Waislamu wa aina hii ni rahisi kuathiriwa na mila na desturi za makafiri.



                   

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 2285

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Maandalizi ya Kimafunzo aliyoandaliwa Mtume Muhammad

(i) Suratul- ‘Alaq (96:1-5)“Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba Aliyemuumba mwanaadamu kwa ‘alaq.

Soma Zaidi...
Nani alikuwa ni Sahaba wa kwanza kufariki akiwa Shahidi

Sahaba wa kwanz akufariki akiwa shahidi, alifariki kwa sababu ya mateso aliyoyapata kutoka kwa Makafiri wa ki Quraysh

Soma Zaidi...
HISTORIA YA BANI ISRAIL

Nabii Musa na Harun walikuwa na kazi kubwa mbili; kwanza, kuwakomboa Bani Israil kutokana na dhuluma waliyokuwa wakifanyiwa na Firaun na Serikali yake, na pili, kuwarudisha kwenye nchi yao takatifu ya Palestina.

Soma Zaidi...
Mafunzo yatokanayo na mkataba wa aqabah katika kuandaa ummah

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
vita vya ahzab, sababu ya kutokea vita hivi na mafunzo tunayoyapata

Vita vya Ahzab- Maquraish waliungana na mayahudi, wanafiki na makabila mengine ya waarabu baada ya kuona kuwa wao peke yao hawawezi kuufuta Uislamu.

Soma Zaidi...