Nabii Lut(a.
Nabii Lut(a.s), kama Mitume wengine walivyofanya aliwanasihi watu wake wamuamini Allah(s.w) na wamche ipasavyo na waogope adhabu yake ambayo ikimfika mtu hapana awezaye kuizuia au kuiondosha.
(Wakumbushe) alipowaambia ndugu yao, (Nabii) Lut: โJe, hamuogopi?โ โBila shaka mimi kwenu ni Mtume muaminifu.โ โBasi Mcheni Mwenyezi Mungu na nitiini.(26:161-163)
โWala sikutakini ujira juu yake; ujira wangu hauko ila kwa (Mwenyezi Mungu) Mola wa walimwengu wote.โ โJe, mnawaingilia wanaume katika viumbe (vyake Mwenyezi Mungu)!โ โNa mnawacha alichokuumbieni Mola wenu katika wake zenu? Kweli nyinyi ni watu mnaoruka mipaka (mliyowekewa).โ(26:164-166)
Na (wakumbushe) Lut alipowambia watu wake: โJe, mnaufanya uchafu, na hali mnaona?โ Mnawaingilia wanaume kwa matamanio mabaya badala ya wanawake? Hakika nyinyi ni watu mfanyao ya ujinga kabisa. (27:54-55)
Pamoja na nasaha hizi nzuri zilizoambatana na hoja madhubuti, hawakumuamini Lut(a.s) ila watu wachache tu. Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu. (51:36)
Pamoja na Nabii Lut(a.s) kuwanasihi kwa maneno ya hekima na hoja zilizo wazi, watu wake hawakuwa tayari kabisa kuacha maovu yale.
Naapa kwa umri wako! Hakika wao walikuwa katika ulevi wao (wa maovu); wanahangaika ovyo. (15:72)
Walishakuwa walevi wa machafu hayo na walipania kumfukuza Nabii Lut na wale walioamini pamoja naye ambao huchukia ubaladhuli huo.
โBasi haikuwa jawabu ya watu wake ila kusema: Wafukuzeni wafuasi wa Lut katika mji wenu, hao ni watu wanaojitakasa, (basi wasikae na sisi wachafu)โ (27:56)
โWakasema: Kama usipoacha, ee Lut (kutukataza haya), bila shaka utakuwa miongoni mwa wanaofukuzwa (katika nchi hii).โ (26:167)
Umeionaje Makala hii.. ?
Tukirejea Qurโan (11:36-48) na (23:26 -29) tunapata maelezo juu ya mchakato wa kuangamizwa makafiri na kuokolewa waumini katika kaumu ya Nabii Nuhu(a.
Soma Zaidi...Historia na sura ya Mtume Muhammad, sehemu ya 10.
Soma Zaidi...Njaa ilitokea na ikawa hapana sehemu nyingine yoyote yenye chakula ila Misri.
Soma Zaidi...Katika vita vya Uhudi waislamu walikufa wengi kulinganisha na makafiri. Lakini makafiri walikimbia uwanja wa vita baada ya kuzidiwa. Je ni nanibalishindwa vita vya Uhudi kati ya waislamu na makafiri?
Soma Zaidi...