Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
- Mtume (s.a.w) alitumia kila aina ya fursa iliyopatikana katika kuufikisha
ujumbe Uislamu kwa watu wengine.
- Mtume (s.a.w) alifikisha ujumbe wa Uislamu kwa watu na makabila mbali
mbali kwa siri na dhahiri kutokana na uadui wa Maquraish dhidi yake.
- Mtume (s.a.w) alitumia mikataba kwa kuandaa ummah wa kiislamu kutoka
sehemu mbali mbali hasa mji wa Madinah (Yathrib) kama ifuatavyo;
- Hii ilikuwa ni baina ya Mtume (s.a.w) na watu wanaotoka nje ya mji wa
Makkah hasa waliokuja kuhiji msimu wa Hija.
- Mtume (s.a.w) alikutana na kikosi cha kwanza kabisa cha watu sita (6)
kutoka Madinah (Yathrib) wa kabila la Khazraj, baada ya kuwafikishia
ujumbe wa Uislamu, walisilimu na wakaahidi kuufikisha kwao Madina.
- Mwaka uliofuata, 621 A.D, kikundi kingine cha waislamu 12 (2 Aus na
10 Khazraj) walikutana na Mtume (s.a.w) kwa siri eneo la ‘Jaratul
‘Aqabah’ na kuweka mkataba wa kwanza wa ‘Aqaba na kukubaliana
yafuatatayo;
- Mtume (s.a.w) aliwapa mwalimu wa kuwafundisha Uislamu, ‘Mus’ab bin
Umair.
- Mwaka uliofuata, 622 A.D.walimjia Mtume (s.a.w) waislamu 75
(wanawake 2) wakiongozwa na mwalimu wao, ‘Mus’ab na kufunga
Mkataba wa pili wa ‘Aqabah sehemu ile ile kwa kukubaliana kuwa;
- Mtume (s.a.w) aliwachagulia viongozi 12 (9 Khazraj na 3 Aus) na watu
watakaokuwa chini ya kila kiongozi, na wanaume wote walimpa Mtume
(s.a.w) mkono wa bai’at kwa maana ya utii wao kwake.
- Baada ya kikundi hicho kurejea na kufika Madinah salama, ndipo Mtume
(s.a.w) aliwatangazia waislamu wote wa Makkah kuhamia Madinah.
- Na takriban baada ya miezi miwili hivi, Waislamu wote wenye uwezo wa
kuhama walishahamia Yathrib (Madinah) kwenda kujiimarisha zaidi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Dini sahihi anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Katika Suratul Buruj, kumetajwa kisa cha makafiri waliowatesa wafuasi wa Mitume waliotangulia kabla ya Mtume Muhammad(s.
Soma Zaidi...Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Tumeona katika historia yake kuwa Nabii Ibrahiim(a.
Soma Zaidi...KULELEWA NA BABA YAKE MDOGOBaada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake.
Soma Zaidi...